Uchaguzi 2020 Mkono wa beberu Amsterdam, wapinzani kushindwa kuungana umesababisha CCM kukosa upinzani madhubuti

Uchaguzi 2020 Mkono wa beberu Amsterdam, wapinzani kushindwa kuungana umesababisha CCM kukosa upinzani madhubuti

Kejuu

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2020
Posts
645
Reaction score
906
Ndugu Watanzania wenzangu.

Kipekee napenda kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kuiona tena siku ya leo.

Baada ya kuangalia na kutathimini mwenendo wa kampeni zinazoendelea kwenye vyama vyote, huku nikirejea kampeni za 2015, ni dhahiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu, 2020, Chama Cha Mapinduzi (CCM) hakina upinzani madhubuti. Kama kichwa cha uzi huu unavyosomeka, zifuatazo ni sababu zilizopelekea kwa CCM kukosa upinzani madhubuti katika uchaguzi wa mwaka huu.

Mkono wa beberu Bob Amsterdam. Kwa mara ya kwanza watanzania tumeshuhudia CHADEMA ikiwa na ushirika wa wazi kabisa na mabeberu, na tumediriki hata kusema sasa chama hiki kimekengeuka na kuwa chama cha mabeberu. Ushirika huu umesababisha chama hiki kujitia doa ambalo litakuwa gumu sana kulisafisha labda kwa kuomba msamaha kwa wananchi. Chadema kilikuwa chama cha upinzani pendwa sana na wananchi tangu kuundwa kwake na muasisi wake Mzee Mtei.

Kilikuwa kinasifika kwa sera zake za kupambana na ufisadi ambao ulikuwa ni mtaji wake mkubwa sana, lakini mwaka 2015, kilianza kupoteza dira baada ya kumkaribisha Mh Lowassa amabaye kilimwita fisadi kwa miaka mingi na kumfanya kuwa mgombea uraisi. Baada ya uchaguzi uamzi huu ulikigharimu sana chama hiki, na kupoteza dira yake kabisa.

Aidha, ushirikia wa beberu Amsterdam na timu yake ndani ya Chadema kwenye uchaguzi huu, naamini utakuwa umefanya baadhi ya watanzania makini, na wazalendo kukisusa chama hiki kwa kitendo chake hiki cha ukibaraka ambao hatujawahi kuushuhidia katika chaguzi zetu na huu siyo utanzania kabisa. Kwa wanaomjua vizuri Mh. Mbowe wa 2015 chini ya Mh. Lowassa, siyo Mbowe wa 2020 chini ya Mh. Tundu Lissu. Kuna uwezekano Mbowe ameshapiga mahesabu yake na inaonyesha anaona giza nene kwa hatima ya Chadema kwenye uchaguzi huu chini ya Mh. Tundu Lissu.

Wapinzani kushindwa kuungana. Jambo hili limesababisha CCM kukosa upinzani madhubuti kama ilivyokuwa chini ya Lowassa 2015 ambayo ilikuwa Magufuli vs Lowassa, ulikuwa ni uchaguzi wenye mvuto sana na upinzani mgumu sana kwa CCM. Hapa limetimia neno lisemwalo umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Mwaka huu ndugu zetu hawa ni dhaifu haijawahi kutokea. Kushindwa kuungana huku kumesababishwa na kutanguliza maslahi binafsi ya vyama vyao.

Wakati wapizani watakuwa wakizigawana kura zao wenyewe, CCM itakuwa na kura zake imara zisozitikiswa, na mwaka huu CCM wapo wamoja sana tofauti na ilivyokuwa mwaka 2015, ambayo ilikuwa na mpasuko na ikapelekea Lowassa kutimuka na wapiga kura wengi sana waliopigia upinzani.

Nahitimisha kwa kusema, mkono wa beberu Bob Amsterdam na wapinzani kushindwa kuungana umesababisha CCM kukosa upinzani madhubuti katika uchaguzi huu, 2020 na inaenda kushinda kwa kishindo kikubwa sana. Kitendo hiki cha CHADEMA kuwa na ushirika na mabeberu kimekitia doa sana chama hiki na athari hii imeanza kuonekana wakati wa uchaguzi huu na itaendelea kuonekana mpaka pale watakapotubu mbele za watanzania, maana huu siyo utanzania.

Asante sana,
Nawasilisha,
Kejuu
 
Hakika.

Screenshot_2020-08-31-12-51-05-1.jpg
 
Unaota wewe
Ulisikiliza nondo za dakika 45 ITV.
Kuunganisha vyama vya upinzani Kuna mitego mingi sana. Hakuna Jambo linalofanywa na TUNDU LISSU kwa bahati mbaya. Kile kichwa sawa na akina Kalamaganda kuburi 50.
 
Yaani CCM hoja zenu mnavyozitoa ni kama nye ni wasomi tu nchi hii na mnawasilisha kwa wajinga ambao hawajui kusoma wala kuandika ,kumbe mnawaambie wasomi wenzenu kuliko nye na mnaonekana vituko tu
 
Wasahau kabisa, MH Mgombea wa Chadema, Mungu asante nyingi Kwa kumponya mwenzetu na asante Kwa Chama chake kumpa dhamana ya kupeperusha bendera Yao kuomba nafasi ya uraisi ambayo pia hapati

Watu ni wepesi Sana kusahau, Nakumbuka salamu yake mh akiwa Kenya Kwa matibabu, alimuuliza mmoja wa wale walioenda kumsalimu kuwa,umewaacha Watanzania wakiwa katika Hali ipi?

Kiongozi huyo, alimhakikishia kuwa, Watanzania Kwa umoja wao, wabakuombea Dua Ili upone na urejee katika harakati za kuitetea nchi yako

Mgombea huyu Akasema, Mmmh, Watanzania na Tanzania ni Taifa la waomba Mungu!

Binafsi nikili kwamba, Kwa tukio lile la mh Kuumizwa, nilikuwa naamini kwamba, Amani Tanzania ni lazima iyumbe!

Amani imeendelea kuwepo mpaka Mtanzania Mwenzetu amerudi na kuungana na Watanzania wenzake

Mbali na kuendelea kuhamasisha mandamano yasiyo na haki, Watanzania wamepuuza na watampuuza,

Nataka kusemaje, Tanzania sio taifa la kuwaamrisha watu wake kama mtu atakavyojisikia, akiamuka Tu Asubuhi Akasema sasa, twende barabarani tukazuwie magari yasipite Ili Hali magari hayo yanapita barabarani Kwa mjibu wa Sheria

Maana yake ni kwamba, ukitaka kuyazuwia magari yasipite, Fuata utaratibu wa Sheria kuyazuwia

Sasa, huyu Beberu na walioko nyuma yake bwana Bob Amsterdam, wajue hili ni Taifa tofauti Kabisa, ambalo bado wenye haki Mbele za Mungu wangali wakiishi na kuongea na Mungu wao!

Na tuendelee kuwaomba watu wote, viongozi wote wa Kiserikali, wawe ni watenda haki! Watende haki Kwa watu wote, Ila hao wanaodhani kwamba, Taifa letu wanaweza kutuwekea kiongozi wao wakitarajia kupata kitu katika Taifa letu, Mungu atawaadhibu wao pamoja na wafuasi wao hapa nchini

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu wabariki wagombea wetu wa uraisi, wabunge na madiwani, hasa wale wenye mapenzi mema na Taifa letu
 
Unaota wewe
Ulisikiliza nondo za dakika 45 ITV.
Kuunganisha vyama vya upinzani Kuna mitego mingi sana. Hakuna Jambo linalofanywa na TUNDU LISSU kwa bahati mbaya. Kile kichwa sawa na akina Kalamaganda kuburi 50.
WATU WALISHAAMUA MIAKA MITANO ILIYOPITA KUWA RAIS NI MAGU HAYA MENGINE NI KUTUMIZA WAJIBU WA KATIBA
 
WATU WALISHAAMUA MIAKA MITANO ILIYOPITA KUWA RAIS NI MAGU HAYA MENGINE NI KUTUMIZA WAJIBU WA KATIBA
Mkuu, uliona mkutano wa tl shy, tbr na Dom? Hii ni salamu tosha kwa tl, watz hawataki ukibaraka hata kidogo. Kazi za Magu watu wanazijua na wanatamani akimaliza miaka hii 5, aongezewe mingine.
 
Tuna itamani sana hiyo sapraiz ila maandalizi hayakukaa sawa mkuu...

Tujiandae awamu ijayo...

Awamu hii tusingizie tumeibiwa kura..
Waache waendelee kuota Ila saplaiz inakuja hawato amini tokea nchi kupata uhuru
 
Upinzani ni mkubwa sana angalia jinsi magu alivyohaha kuomba kura Bariadi leo ndio utajua kazi ipo.
 
Tuna itamani sana hiyo sapraiz ila maandalizi hayakukaa sawa mkuu...

Tujiandae awamu ijayo...

Awamu hii tusingizie tumeibiwa kura..
Kura zitaibiwa ila bado itabidi wautangazie umma wa tz ukweli wa mambo make hata ccm wenyewe wapo wengi tu nao hawatoi kura zao kwa ccm kwahiyo wanasubiria tu siku wakamalize kazi
 
Tatitizo la kutokwenda na wakati. Lissu ashafafanua, mataga mnakosa la kuandika mbona ccm wepesi hivi
 
NA TUNDU LISSU KAIACHA FAMILIA YAKE UNELGIJI HALAFU ANAKUJA KUTUTIBULIA MAISHA YETU HUKU?

WATAKALISHWA CHINI OCTOBA 28
 
Umeandika HEKAYA ndefu , nakujibu kifupi tu.
Mwaka 2019 Serikali ya kidhalimu ya CCM ilitunga sheria ya Uchaguzi, inataka kama mnaungana kutoa taarifa kwa msajili, na sababu za kujiunga, na msajili ana mamlaka ya kukubali ama kukataa, na anaweza kuwakatalia hata siku moja tu kabla ya siku ya uchaguzi/kuwasilisha majina ya wagombea.
 
Unaota wewe
Ulisikiliza nondo za dakika 45 ITV.
Kuunganisha vyama vya upinzani Kuna mitego mingi sana. Hakuna Jambo linalofanywa na TUNDU LISSU kwa bahati mbaya. Kile kichwa sawa na akina Kalamaganda kuburi 50.
Mbona makinikia walimgaragaza?
 
Kwanini mgombea wa ccm hastahili kupewa tena kura zetu?

Sababu za kutompa kura zetu mgombea wa ccm ni hizi zifuatazo.

1. Mauaji ya raia wasio Na hatia,

2. Umeendesha nchi kikabila na kikanda,

3. Umeshiriki katika ufisadi wa kununua ndege nk kama sio kweli tupe mikataba ya ununuzi.

4. Umewatesa sana waliokukosoa mfano hai TUNDU LISU na MDUDE CHADEMA.
 
Angalieni hayawani mwingine huyu!
Sasa Kama maccm si wezi wa kura kwanini Mkapa alionyesha hadharani kukosa imani na hao wahuni wa tumeccm? 😳

1599235200636.jpeg


Nani mwizi wa kura?
Lijuakali said it all
 
Back
Top Bottom