Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Mkopo NMB: Nimekopa 9 mil , nakatwa 250,000 kila mwezi kwa miaka 6 nitarejesha 18 mil !

Status
Not open for further replies.
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya

Iko namna hii, Algebra hii na wala sio Albadiri

Kakopa 9m, malipo kila mwezi 250k , muda ni miaka 6 (mwaka 1=miezi 12, zidisha 6mara 12 unapata 72)

Hivyo, fanya namna hii, 250k mara 72=18milioni.

Na hizi bado hajaweka chaji nyingine za kibenki zinazoweza kukaribia mawe kumi

Ila kwa riba ya 100 asilimia naamini hii NMB ya kipekee (wanafanya usury)
 
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya
Acha utoto.

Mwaka una miezi 12 kwa maana miaka 6 ina miezi 72 yaani miezi 12 +12+12+12+12+12 = 72.

Sasa hiyo miezi 72 kila mwezi wanachukua 250000.
Kwa hyo itakuwa

250000 ×72=18000000.

Kwa hyo ni 18MILIONI.

Yaani sawa sawa jamaa ana shida ya 8M alafu akaenda benki akaambiwa atoe hiyo alokuwa na shida nayo 8M

Mikopo inarudisha nyuma sana.
Namuomba Mungu anilinde nisikope kabisa
 
Iko namna hii, Algebra hii na wala sio Albadiri

Kakopa 9m, malipo kila mwezi 250k , muda ni miaka 6 (mwaka 1=miezi 12, zidisha 6mara 12 unapata 72)

Hivyo, fanya namna hii, 250k mara 72=18milioni.

Na hizi bado hajaweka chaji nyingine za kibenki zinazoweza kukaribia mawe kumi
Mie naona nisawa kwa kuwa unatoa kidogokidogo,hata haiumi
 
inatemea waenda kufanya biashara gani,kama biashara inatoka sioni tatizo maana hiyo milioni tisa inaweza kuzaa milioni mia tatu kwa huo mda
 
Huu ni uongo eti umekopa mil9 kwamiezi 6x250,000=ni 1,500,000 hio mil 18 kwa hesabu ipi mkuu au umejichanganya

Sasa hapo umeandika nini, hadi kuita mwenzako muongo..... rudi shule au kubali ulipoteza muda wako tu.
 
Hii nchi kuna mambo mengi ya msingi sana hayapewi kipao mbele mana hayana madili kama ilivyo miradi mikubwa ambayo bila shaka Kuna wachache wananufaika nayo sana kwa niaba ya wengi.
Wenzetu Waarabu wana mfumo wao wa mikopo isiyo na riba wakifuata misingi ya dini ya kiislam.
Waafrika tumefuata mifumo hiyo ya mariba makubwa makubwa lakini yanazidi kutupa umaskini na watu wengi wanashindwa kulipa hasa wafanyabiashara mana riba ni kubwa sana wanaolipa kwa urahisi ni wafanyakazi na wanasiasa ambao Mara nyingine wanaahidiana kusaidiana kulipa alimradi watumikie siasa na kampeni au kuhama vyama.

Sisi tunafuata mifumo yote ya kifedha ya nchi za magaharibi lakini wakitoa ushauri wanaitwa mabeberu.
Sijui Link waafrika tutakua na mifumo wetu wa kifedha.

Waafrika sijui tulilogwa na nani?
 
Mie naona nisawa kwa kuwa unatoa kidogokidogo,hata haiumi

...hata mimi naona hivyo, kwa kuwa anatoa kidogokidogo, tena kila mwezi (siku 30 au masaa 40 ya kazi) basi kila saa la kazi anatoa pesa ndogo tu inayokaribia mia nane
 
Kama una biashara nzuri kweli uchukue hiyo fedha . Lakini kama ni biashara ya kusadikika achana nayo kwa itakutia umasikini zaidi.
Na wengi unadhani wana biashara hasa hawa wafanyakazi yani hapo utakuta kaenda kununua gari au kaenda kujenga nyumba tena ni ya kukaa tu wala sio kupangisha na kanunua makochi na TV
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom