HOJA Mkopo unanitesa sana, si jambo rahisi kama wengi wanavyofikiria

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Ulichukuwa mkopo kuanza biashara au kuendeleza biashara? (Hapa kuna technical mistake)
 
Hapa umetoa darasa kwamba watu wanapochukua mkopo wasitumie pesa ya mkopo kwenye maandalizi badala yake waitumie kwenye biashara yenyewe ili hela itakayorudi km faida ndio wafanye maandalizi
Mara nyingi mikopo ni ya kuendeleza kilichopo.
Ni bora ufungue Banda la chips,ulistady mwelekeo wake,ndipo ukope!
 
Ninasema tenha mkopo mkopo mkopo
Sio wakuchukua iwe unaendeleza biashara au unaanza biashara kwa namna yoyote ile wakuuu hakuna technical mistake mkopo ni hatari kwa maslahi

Mfano mdgo una biashara ya 5M
Ukachukua mkopo wa 2M Kuendeleza biashara jumla ya mtaji ni 7M rejesho kwa mwezi ni 190000 kwa miez 12 ni sawa na 2.28M ukirejesha na hapa naweza kuwa nimekadiria vibaya matokeo yake sasa yako hivi.

Katika mtaji mama kuna asilimia zitatoka tu kutoka 5M sitashangaa unapomaliza mkopo umebaki na 4M kwann nasema hivi

1.ukikopa unatakiwa kurejesha mkopo ,na duka linahitaji ufunge mzigo ili bidhaa ziendelee kuwepo ,ila unakuta unataka kufunga mzigo na rejesho limekaribia ukiangalia mzunguko wa biashara umepoa unalazimika kutunza ile fedha ili usikose rejesho ,kumbuka dukani bidhaa zinakudai
Matokeo yake utaanza kukosa wateja kutokana na kukosa bidhaa kulinda pesa ya rejesho.
Kumbuka:Biashara yoyote kuna msimu wa matzo na wa biashara nikimaanisha kuna Nyakati unakaa wateja hakuna na kuna Nyakati ukifika katika biashara hutamani uondoke kazini ,sasa mkopo huwa hautambui hiko kitu kipindi biashara inakua ngumu mara nyingi hauwezi kufunga mzigo ila unabaki ukikusanya fedha kwaajili ya rejesho matokeo yake mkopo utanyonya mtaji ,na kipindi cha biashara kinapofika mtaji umepungua na fedha ya kuongeza bidhaa huwezi kupata maan bidhaa muhimu wateja wanazo zitaka hazipo .

2.Ajali za biashara, hapa nizungumzie zile changamoto za majanga ya asili mkopo hautambui hilo na itakubidi ulipe kwa namna yoyote omba sana ukichukua mkopo lisijitokeze janga ndio utajua mkopo haufai Bank na taasisi zozote za kifedha hazitambui kitu kinaitwa hasara kwa mteja ila zinajitazama zenyewe
Kwa ushauri tu mkopo haufaiii

N:B. linda ulichonacho kitakulinda piah.
Sauti kuu kutoka NMR
 
Hem tuambie waliofanikiwa wenye biashara kubwa wao walifikaje juu bila mikopo?
 
Brooo unafeli wapi, hakuna mtu ambaye hana Mkopo, Watu tuna mikopo na tunaduda tu. Unajipa pressure kisa Mkopo
 
Kipindi kigumu hupitii wewe pekee yako, mimi mwenyewe nilikuwa na rejesho la milioni 49, now limebaki 16M ivi na siwazi, nafikia hatua sina hata Mia. Ugumu wa maisha sio kwako tuu kila mmoja ana msalaba wake gentleman.
 
Kipindi kigumu hupitii wewe pekee yako, mimi mwenyewe nilikuwa na rejesho la milioni 49, now limebaki 16M ivi na siwazi, nafikia hatua sina hata Mia. Ugumu wa maisha sio kwako tuu kila mmoja ana msalaba wake gentleman.
Nimeshare screen shoot yangu ili ujione hauko pekee yako mwenye madeni, mkopo wangu huu niliuchukua nikiwa na miaka 26 now nina miaka 30. nataka niwakope tena, usiwe na chanzo kimoja cha biashara
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2026-07-07 at 08.31.43.jpeg
    18.6 KB · Views: 28
Pole sana, tulishakatazwa kuchukua mkopo kwaajili ya kuanzisha biashara ila kuiendeleza!

Tafuta kazi yoyote huku ukitafuta unayoitaka, ili uwe unapunguza deni depression itakumaliza!
Mimi mikopo sitaki hata kuisikia nimeshawahi kupoteza gari kwa kushindwa kufanya marejesho , ni bora kubaki na shida zangu nichovye tonge la ugali kwenye maji nile ilimradi nabaki na amani yangu , ukikwama tafuta njia zengine za kujinasua kuliko kukimbilia kwenye mikopo unakuwa unajichimbia shimo zaidi
 
Pole sana, tulishakatazwa kuchukua mkopo kwaajili ya kuanzisha biashara ila kuiendeleza!

Tafuta kazi yoyote huku ukitafuta unayoitaka, ili uwe unapunguza deni depression itakumaliza!
Huyu ni mjinga sana

Kachukua mkopo hana hata mia, mkopo huo huo ndo kafanyia maandalizi ya biashara na ndo kafanyia biashara yenyewe

Huwa tunatuchukua mkopo kwa ajili ya kwenda kuendeleza biashara zetu, siyo kwenda kununua masofa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…