Mikopo si jambo rahisi kama watu wengi wanavyofikiria.
Nilichukua mkopo na kuanzisha biashara nikiwa na matumaini makubwa. Hata hivyo, nilitumia fedha nyingi kwenye maandalizi, biashara haikufanikiwa kama nilivyotarajia, na baadaye nikapatwa na majanga yaliyoteketeza hata mtaji uliokuwa umebaki.
Kwa sasa sina kazi, lakini bado ninawajibika kulipa marejesho ya mkopo kila mwezi. Ni presha kubwa sana. Kila siku ni mawazo, msongo wa mawazo na hofu. Wakati mwingine nahisi kukata tamaa kabisa. Natafuta kazi kila sehemu lakini sipati.
Nimegundua kuwa msongo wa mawazo (depression) ni jambo la kweli. Unapokuwa na madeni, huna kipato, na huoni njia ya kutoka, maisha yanakuwa magumu sana.
Ninaendelea kutafuta kazi na fursa nyingine kwa matumaini kwamba siku moja hali itabadilika, lakini kwa sasa siwezi kuficha kwamba ninapitia kipindi kigumu sana. Sijui nifanye nini.