Itumbukize kwenye shimo la choo halafu vuta ile kamba utakuwa ume i flashAnaejua kuflash simu za mkopo anisaidie, nangamia mwenzenu!
Tatizo kubwa watu huwa hawasikii na siku hizi, mkopo unachukuliwa kama grant!Pole sana, tulishakatazwa kuchukua mkopo kwaajili ya kuanzisha biashara ila kuiendeleza!
…
Mungu akuone na akutetee Mkuuu katika changamoto unayoipitiaa mkuuMikopo si jambo rahisi kama watu wengi wanavyofikiria.
Nilichukua mkopo na kuanzisha biashara nikiwa na matumaini makubwa. Hata hivyo, nilitumia fedha nyingi kwenye maandalizi, biashara haikufanikiwa kama nilivyotarajia, na baadaye nikapatwa na majanga yaliyoteketeza hata mtaji uliokuwa umebaki.
Kwa sasa sina kazi, lakini bado ninawajibika kulipa marejesho ya mkopo kila mwezi. Ni presha kubwa sana. Kila siku ni mawazo, msongo wa mawazo na hofu. Wakati mwingine nahisi kukata tamaa kabisa. Natafuta kazi kila sehemu lakini sipati.
Nimegundua kuwa msongo wa mawazo (depression) ni jambo la kweli. Unapokuwa na madeni, huna kipato, na huoni njia ya kutoka, maisha yanakuwa magumu sana.
Ninaendelea kutafuta kazi na fursa nyingine kwa matumaini kwamba siku moja hali itabadilika, lakini kwa sasa siwezi kuficha kwamba ninapitia kipindi kigumu sana. Sijui nifanye nini.
Pole sana Mkuu. Katika vitu ambavyo sitokaa nimshauri mtu afanye kimojawapo ni hicho kwani kwangu naona kama ni mateso makubwa sana mnapitia.Anaejua kuflash simu za mkopo anisaidie, nangamia mwenzenu!
Bila kusahau njia mbadala ya marejesho. Siyo kutegemea Biashara hiyo ndiyo ikupatie marejesho tuUlitakiwa upate elimu ya mkopo kabla hujachukua..!!
Mkopo sio wa kuanzishia biashara.
Pesa za mkopo ni kwaajili ya kuongezea uhitaji wa bidhaa unazouza au unazozalisha kwa wateja..!!
Huwezi kuendelea katika Biashara bila kitu inaitwa mkopo.Ninasema tenha mkopo mkopo mkopo
Sio wakuchukua iwe unaendeleza biashara au unaanza biashara kwa namna yoyote ile wakuuu hakuna technical mistake mkopo ni hatari kwa maslahi
Mfano mdgo una biashara ya 5M
Ukachukua mkopo wa 2M Kuendeleza biashara jumla ya mtaji ni 7M rejesho kwa mwezi ni 190000 kwa miez 12 ni sawa na 2.28M ukirejesha na hapa naweza kuwa nimekadiria vibaya matokeo yake sasa yako hivi.
Katika mtaji mama kuna asilimia zitatoka tu kutoka 5M sitashangaa unapomaliza mkopo umebaki na 4M kwann nasema hivi
1.ukikopa unatakiwa kurejesha mkopo ,na duka linahitaji ufunge mzigo ili bidhaa ziendelee kuwepo ,ila unakuta unataka kufunga mzigo na rejesho limekaribia ukiangalia mzunguko wa biashara umepoa unalazimika kutunza ile fedha ili usikose rejesho ,kumbuka dukani bidhaa zinakudai
Matokeo yake utaanza kukosa wateja kutokana na kukosa bidhaa kulinda pesa ya rejesho.
Kumbuka:Biashara yoyote kuna msimu wa matzo na wa biashara nikimaanisha kuna Nyakati unakaa wateja hakuna na kuna Nyakati ukifika katika biashara hutamani uondoke kazini ,sasa mkopo huwa hautambui hiko kitu kipindi biashara inakua ngumu mara nyingi hauwezi kufunga mzigo ila unabaki ukikusanya fedha kwaajili ya rejesho matokeo yake mkopo utanyonya mtaji ,na kipindi cha biashara kinapofika mtaji umepungua na fedha ya kuongeza bidhaa huwezi kupata maan bidhaa muhimu wateja wanazo zitaka hazipo .
2.Ajali za biashara, hapa nizungumzie zile changamoto za majanga ya asili mkopo hautambui hilo na itakubidi ulipe kwa namna yoyote omba sana ukichukua mkopo lisijitokeze janga ndio utajua mkopo haufai Bank na taasisi zozote za kifedha hazitambui kitu kinaitwa hasara kwa mteja ila zinajitazama zenyewe
Kwa ushauri tu mkopo haufaiii
N:B. linda ulichonacho kitakulinda piah.
Sauti kuu kutoka NMR
Inaonesha Yanga mwenzangu si mfanyabiashara.Pole sana Mkuu. Katika vitu ambavyo sitokaa nimshauri mtu afanye kimojawapo ni hicho kwani kwangu naona kama ni mateso makubwa sana mnapitia.
Simu nayo ni ya kikutesa? rudisha ulipo nunua waambie umeshindwa mwendoAnaejua kuflash simu za mkopo anisaidie, nangamia mwenzenu!
Yanga mwenzangu unaniangusha bana. 😂Inaonesha Yanga mwenzangu si mfanyabiashara.
Hapo si ndio anakuwa amekula hasara Mkuu.Simu nayo ni ya kikutesa? rudisha ulipo nunua waambie umeshindwa mwendo
Wataiuza kwa mwingine then atapewa kiasi flani kupoza maumivu by the way vitu vingine sio lazima kukopa kama simu na vitu luxuriousHapo si ndio anakuwa amekula hasara Mkuu.
Yaani nikimaanisha atakosa simu na hela aliyokuwa ameanza kuilipa kidogo kidogo.
Ooh! Kumbe ndo ipogo hivyo.Wataiuza kwa mwingine then atapewa kiasi flani kupoza maumivu
Nimekuelewa ila wewe ndiye hujanielewa. Nina maana, huwezi kuwa mfanyabiashara bila kuwa na mikopo.Yanga mwenzangu unaniangusha bana. 😂
Umeielewa Quote yangu lakini?
Mikopo inatesa sana! Niliwahi kukopa pesa kidogo tu lakini mpaka mshipa wa hisia zote ukakata😂Mimi mikopo sitaki hata kuisikia nimeshawahi kupoteza gari kwa kushindwa kufanya marejesho , ni bora kubaki na shida zangu nichovye tonge la ugali kwenye maji nile ilimradi nabaki na amani yangu , ukikwama tafuta njia zengine za kujinasua kuliko kukimbilia kwenye mikopo unakuwa unajichimbia shimo zaidi
Na atakuwa alichukua kwenye vicoba, bank si lazima wampe terms na ushauri hakupewa? Yani ukiwa unakopa una calculte kwanza kichwanai utalipaje, how comes yeye kajilipua namna hii? Au ndio risk taker😅Huyu ni mjinga sana
Kachukua mkopo hana hata mia, mkopo huo huo ndo kafanyia maandalizi ya biashara na ndo kafanyia biashara yenyewe
Huwa tunatuchukua mkopo kwa ajili ya kwenda kuendeleza biashara zetu, siyo kwenda kununua masofa
Kuna sehemu walimshauri vibaya! Kukopa ni process sio jambo la ghafla hivi..Tatizo kubwa watu huwa hawasikii na siku hizi, mkopo unachukuliwa kama grant!
Kabla ya kuchukua mkopo wa kibiashara, lazima uhakikishe una vyanzo mbadala vya kulipa marejesho. Siyo Biashara itoe marejesho.