HOJA Mkopo unanitesa sana, si jambo rahisi kama wengi wanavyofikiria

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Kama mtu unakazi ya uhakika.
Chukua mkopo jenga makazi bora kwa familia.
Ukiisha chukua tena fungua biashara tena kwa asilimia ndogo tu ikifanikiwa jaza fungu lote lililobaki.

Tatizo watu huwa wanaharaka sana.
Pole sana maumivu yako niliwahi kupitia nikachukua mkopo nikanunua shamba hekari 15 na kulisafisha naanza project tu ikagundulika pale kuna mgogoro serikali imemuuzia muwekezaji siku nyingi. Flesh tu nikaacha nikaendelea kupambana japo moyo uliuma hasa kwa aliyeniunganisha hilo eneo nilimuamini kumbe alikuwa anajua anataka nikwame tu
 
Pole sana Mkuu. Katika vitu ambavyo sitokaa nimshauri mtu afanye kimojawapo ni hicho kwani kwangu naona kama ni mateso makubwa sana mnapitia.

Ila endelea kuuliza uliza huenda wataalamu wapo wanaoweza kukusaidia.

Mikopo inasaidia kukuza biashara na kufanikisha jambo lako kwa haraka. Mikopo inakuwa mibaya pale unapoutumia nje ya lengo lililokusudiwa. Mfano unachukua mkopo ununue gari la kutembelea hapo bila kujipanga lanzima uuchukie mkopo.
 
Pole Gentleman hizo do changamoto za Maisha sasa, kwenye biashara suala la utapeli na kuzulumiwa lipo nje nje.
 
Huyu ni mjinga sana

Kachukua mkopo hana hata mia, mkopo huo huo ndo kafanyia maandalizi ya biashara na ndo kafanyia biashara yenyewe

Huwa tunatuchukua mkopo kwa ajili ya kwenda kuendeleza biashara zetu, siyo kwenda kununua masofa
Acha kumtusi unatakiwa kumpa darsa siku nyingine ajue cha kufanya..kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa
 
Pole sana mkuu kwa changamoto.
 
Niliwahi kubadili namba za simu kisa madeni oya usiombe mpaka nakuja kuclear nikajifunza kwa sasa sitaki mikopo ya kuumiza.
 
Pole sana, kama collateral si nyumba ya familia usilipe iuzwe utanunua nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…