Mkristo ni Mungu. Bila kuamini hivyo huwezi kuwashinda miungu watu na miungu yao

Mkristo ni Mungu. Bila kuamini hivyo huwezi kuwashinda miungu watu na miungu yao

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Sio mara ya Kwanza Mungu kuwafanya wanaomufuata Mungu.

Ili Musa amvae Farao ambaye kwa kimisri alikuwa anahadhi ya muungu alimfanya kuwa mungu kwa farao.

Kuna watu ni miungu, kuna miungu mingi, ukiwaface kama binadamu watakushinda, lazima uvae cheo chako cha umungu ili uwe juu yao.

Biblia inasema hivyo.
Zaburi 82:6
Mimi nimesema, Ndinyi miungu, Na wana wa Aliye juu, nyote pia.

Unapompokea Yesu, unafanyika mtoto wa Mungu. Mtoto huwa anaDNA za baba. Hivyo unakuwa na vinasaba vya kiungu vinavuoweza kukusaidia kukabili vimiungu na vimiungu watu vinavyokuzunguka.

Bila kuamini hivyo utatawaliwa na miungu na miunguwatu.

Ni hayo tu.
 
Nakazia huko mwishoni, unapompokea Yesu, ana boost ule uungu wako uliozaliwa nao na kuwa active, unakuwa juu zaidi huku ukiishi katika Neno (yeye mwenyewe)

Waefeso 6:10-20
Hapa ukisoma utajua kuwa hatutakiwi kupigana kwa namna ya mwilini, bali ya rohoni.

Siku hizi wanaojielewa wanajitwaalia utukufu kwenye kila kitu, kazi, biashara, mahusiano, elimu, umaarufu, n.k.

Sass usipokuwa makini, hautoboi ng'oo,

Ndio wanasema maskini hata apewe bilioni moja, baada ya Muda tuu itaisha, ila tajiri hata umpe elfu kumi, atajua kuizalisha mpaka impe utajiri.
 
Back
Top Bottom