Sonko Bibo
JF-Expert Member
- May 24, 2019
- 1,181
- 1,839
Wasalaam tena,
1. Ninyi ambao mlijitoa kuwatunza watoto wa wanaume wengine — bila kinyongo, bila malalamiko — lakini mwisho wa safari mkalipwa dharau, kejeli na masimango...
Pongezi nyingi kwenu.
Msingeweza, lakini mlijaribu. Dunia inaweza kusahau, lakini dhamira zenu zinastahili heshima.
2. Ninyi ambao mlisimama kama nguzo kwa wanawake waliowaahidi tu “nakupenda, sitakuacha, tutazaa pamoja,” mkakutana njiani, mkakuta watoto tayari wapo...
Hamtukana, hamkatai, mkawapokea, mkawapenda, mkawafungulia wake zenu biashara kubwa — hata kwa kodi za maeneo ambayo hata kwa kurunzi ya Mungu huwezi kuona faida.
Pengine ilikuwa ni juhudi zenu za kuwadhibiti wasije wakaliwa na wanaume wasioendana na hadhi yenu.
Lakini wakatumia mwanya wa biashara kujiuza na kuchafua hadhi yenu.
Mwisho wakanawa mikono, wakawaona ninyi si wapenzi tena bali "masponsa."
Pongezi kwenu.
3. Ninyi mliojitahidi kwa moyo wote kuwasomesha wake zenu, kuwaendeleza kielimu, kuwajengea ndoto mpya ili msaidie hata kutokomeza umasikini ukweni...
Mkitegemea mkifika kwa wakwe mnakuta mazingira ya heshima, hadhi, na mabadiliko.
Lakini mlisahau kwamba wale wakwe walishapokea mahari zaidi ya mara mbili kutoka kwa wanaume waliowatangulia, ambao waliamua kuondoka kwa sababu zao.
Pengine walikuwa na uwezo mkubwa zaidi — lakini wakasema: "Haya mambo ni shobo, haya ni mateso."
Pongezi kwenu.
Wengine wataongeza na kuchangia nyama.
Kwa sasa, pongezini wanaume waliowahi kujitoa kwa upendo wa kweli, wakapambwa kwa upotevu wa kweli.
By: SONKO