Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

SEHEMU YA 29

Kumbukumbu za nyuma ziliuteka ubongo wangu,…nikakumbuka yaliyotokea huko nyuma, yaliyompata huyu msamaria mwema, tena kwa ajili yangu, akafikia hadi kufungwa na wazazi wangu, …nikaapa kuwa siku nikikutana naye, nitajitahidi nifanye lolote kumlipa fadhila zake, sasa nitamlipa nini, …na nilishamsahau, nikujua hayupo tena duniani…na siku hiyo, ndio nikakutana naye, nikiwa na docta mtoto wa watu akiwa ni mpenzi wangu…je nilifanya nini, angalia mitihani hii ya maisha…

***********

Nakurejesha nyuma kipindi nikiwa binti mdogo, wa miaka kumi na tano,…kipindi hicho ndio nilimuona kijana mmoja mara kwa mara akiwa anakuja kuonana na mzee mmoja aliyekuwa mlinzi wa nyumba yetu. Yeye kiumri alikuwa mkubwa kuliko mimi…nikaanza kuzoeana naye tu..
Kuna kipindi baba yake alikuwa akitulimia shamba, basi na yeye anakwenda kumsaidia baba yake mimi, nikawa nafika shamabi kuchukua matunda, nawakuta wakiwa wawili, nawapatia chochote, mwanzoni sikuwa naongea naye sana, kutokana na hali ilivyokuwa wakati huo. Wazazi walikuwa wakali hawakupenda kabisa nizoeane naye, au kuwa karibu naye,…

Kila huyo mvulana akija, nilimgundua akiniangalia sana, na ikitokea tukikutanisha macho anayakwepesha kwa haraka na kujifanya kama alikuwa haniangalii, ikawa kama mchezo fulani wa utu-rika,.. na tukajikuta tunamezoeana kinamna hiyo, lakini sio ile ya ukaribu ya kukaa pamoja na kuongea.

Ni ikaja muda hata mimi nikikaa nyumbani, namuwaza yeye, fikiria ni mtoto wa mkulima, mfanyakazi wetu tunaweza kusema wa ndani…lakini mimi sikulijali hilo, nilimuona sawa na wavulana wengine. Sio kwamba nilikuwa na tabia mbaya, ya kuwa na mazoea na wavulana, hapana..ila nilijali sana usawa na utu, hata nikiwa msichna mdogo.

Basi kwa ile hali ya kunyanyapaliwa na wazee, kuwa wakifika wanakuwa na sehemu yao, hawaruhusiwi kuingia ndani, sikulipenda hilo kabisa, nikaona lazima nifanye jambo, la kuwasaidia hawa watu wawili…nilimjali sana huyo baba yake, alikwua na tabia nzuri tu,…huruma na upendo,.

Basi…huyo kijana akifika, ninajua wapi nikae ili aweze kupita na kuniona, kwa haraka nikakuwa na zawadi yoyote ya kumpa, chakula au matunda,…maji ya baridi ili wakinda sahamba wapate kuyatumia yeye na baba yake..na nilijithidi sana wazee wangu wasiweze kuona hayo…

Lakini ikatokea tukio, liloharibu kila kitu, na baada ya tukio hilo, tukaachana na familia hiyo sisi baadaye tukahama na kuja kuishi Dar, ambapo baba yangu alihamishia kampuni yake, na huko kijijini tukawa hatufiki mara moja moja tu. Na sikuweza kuwaona tena. Tukio hilo kwakweli liliniumiza sana kiasi kwamba niliwaona wazazi wangu kama ni watu wasio na utu-wema.

*************


‘Kwanini hukunitafuta, ulipoachiwa kutoka jela...?’ nikamuuliza, nikikatiza mawazo yangu ya kumbukumbu za huko kijijini….

‘Kwanini nikutafute..ulitaka niendelee kuumia, maana mimi ningelisemaje kwako, ..hebu nijishushe hapo, baada ya tukio lile, ningelionekana na wewe tena, si ndio ningepeleka tena jela nikafie huko.., nakumbuka niliwahi kuandika barua kuja kwako, lakini sikuwahi kupata majibu...’akasema.

‘Barua,…. hahaha..nani ana mipango ya barua siku hizi, ulindika hiyo barua kuja kwangu ukampa nani..mbona sijawahi kuona barua yako yoyote,...?’nikamuuliza, niliona kama ananitania tu.

‘Basi nahisi kuna mtu alikuwa akizipokea na kuzichana, mimi niliandika, nyie si mna box la barua, na kuna mtu alisema anakuja huko kwenu , nikampa barua, lakini nikajua umeshatekwa na familia yako, na huenda hata wewe hutaki hata kuniona tena, kwa jinsi watu walivonivumishia ubaya....’akasema akitikisa kichwa kusikitika .

‘Kwanini usingelinipigia, angalau hata simu...?’ nikamuuliza

‘Nikupigie simu!!! Hahaha…, simu hiyo ningeliipata wapi, huko kijijini, hivi unayafahamu maisha yetu yalivyokuwa...anyway, hayo yameshapita na wewe una mume wako, ...naona nisikupotezee muda, ...’akasema na kutaka kuondoka, mimi nikamshika mkono asiondoke.

‘Nimeshakuambia yule sio mume wangu, ni mchumba wangu, hatujaoana bado…Sikiliza, ..ahadi yangu ipo pale pale…’nikasema na hapo akaniangalia kwa macho yenye kushangaa.

‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ akaniuliza

‘Ahadi yangu ya kufanya lolote ilimradi niwe nimelipa fadhila zako, najua inaweza isikidh haja, lakini angalau na mimi niwe nimfanya jambo kwako la utu wema..sasa mimi nataka tuje tuongee tena nione nitakufanyia nini…’nikasema, na nikaona kama ananywea, hakuridhika na maneno yangu hayo.

‘Hapana, mimi sihitajii msaada wako, sitaki kuwa mfanyakazi wenu, au ….kuwategemea nyie tena, hapana…hilo sitaki, …’akasema

‘Najua ni kwanini unasema hivyo, ila mimi natamani zile siku zirejee tena, kiukweli mimi sijaolewa, na sisemi hivyo kwasababu kuwa nataka uwe ...mpenzi wangu, hapana mapenzi hayalazimishwi, na…mimi na mchumba wangu hatujafikia huko, bado kuna mipango mimi, yeye na mimi pia, lakini mimi ninaweza kufany ajambo la kukusaidia ukafika mahali, usilipuuzie hilo..’nikasema

‘Hilo la kukutana kuongea tena, ni wewe, kama huogopi huyo mpenzi wako, sitaki kuja kuwaharibia mahusiano yenu, ikawa ndio sababu ya kufichua yale yaliyopita, sipendi hilo kabisa,…’akasema

‘Kiukweli unanidai sana, mengi umenifanyia, lakini sijaweza kulipa chochote kwako, kwangu mimi naona ni deni, na nataka uwasamehe wazazi wangu, hata bila ya wao kufahamu, na hilo naweza kufanya nionavyo mimi, niamini tu,…usijali kabisa kuhusu hisia za wazazi wangu, nafahamu ni kwanini wanafanya hivyo,....’nikasema

‘Hahaha, hapana , niliapa kuwa sitaajiriwa kwa watu kama mfanyakazi wa upendeleo, mimi nataka nihangaike kivyangu…sawa nashukuru kwa kuonana nawewe, mengine tuyaache kama yalivyo, vipi maisha na mchumba wako, katulia siku hizi..?’ akaniuliza

‘Mchumba wangu hana matatizo, ni mzungu kwakweli, muhimu nimuambie ukweli tu, hata akiniona tunaongea, yeye atadai nimuambie wewe ni nani, na ni hivyo, sina shaka naye, ila hayo hayana msingi, wewe sifikiria wako langu la kukuwezesha, unalionaje hilo…’nikasema

‘Mhh…sivyo nitakavyo, najua hutanielewa, ndio maana nasema tuyaache tu, yabakie kama yalivyo, kwa maana mimi nilikufanyia nini kikubwa, ni kawaida tu, na yaliyotokea hadi wazazi wako kufanya hivyo, ni…naweza kusema hata mzazi mwingine huenda angelifanya hivyo…’akasema

‘Hapana lile tukio lilikuwa kubwa, na kiukweli nakiri wazazi wangu walikosea, sana,..maana hawajui ulivyofanya, uliweza kuniokoa mikononi mwa wabakaji, mijitu mikubwa, na wewe ulikuwa sio umbile lako kabisa, ukapigana na wao kufa na kupona, hawakuliona hilo.

Kiukweli mimi..sitalisahau hilo kamwe, nilikuona kama mtu maalumu sana kwenye maisha yangu ndio maa niliahidi siku nikikutana nawe, nitafanya lolote lililondani ya uwezo wangu, ili na wewe uone kuwa nakujali…...’ nikamwambia.

‘Mhh…nilishaipata hiyo zawadi inatosha., wewe wasalimie wazazi wako na mchumba wako, mungu akipenda tutakuwa tunaonana, lakini nisingelipenda wafahamu kuwa tumekutana nafahamu watakavyojisikia, huenda ikaja dhahama kubwa zaidi ya ile…japokuwa sasa nimekuwa mkubwa siogopi, nafahamu haki zangu...’akasema

‘Jamani ina maana hujatusamehe tu…’nikasema

‘Usijali sana ndio ubinadamu ulivyo,..nilishawasamehe mbona…kwa hivi sasa nimeliona hilo, kuwa yale waliyoyafanya wazazi wako walikuwa na maana kwao, kwa ajili ya kulinda heshima ya familia yenu, na walitaka kutoa fundisho kwa jamii, na nasikia familia yenu imekuwa ikiogopewa sana,..ni sahihi, yamepita yapite.

‘Tatizo wewe hufahamu jinsi gani niliumia...lakini ikafika mahali nikasema basi tena, mungu ndiye atakupeni yale yote mliyotutendea wewe na baba yako, na nikatubu sana kwa niaba ya wazazi wangu…kiukweli baba yako nilimuona kama baba yangu mkubwa...sikupenda kumuita babu, kama walivyozoea kumuita wengine, mimi ninajua kuzeeka kwake haraka ni kutokana na hali ya maisha, umri wake haupo mbali na umri wa baba yangu, …mimi nilipenda kumuita baba mkubwa.....’nikasema.

‘Nashukuru kusikia hivyo, ni wewe tu ulikuwa tofauti na wengine, sijui kwanini wazazi wako, walikuja kutuchukia hivyo..niliona kabisa hawakupenda, hata nikukaribie..na nahisi ilipotokea lile tukio, ndio wakaonyesha hisia zao dhidi yangu. Ni sawa, labda nisiwalaumu sana, maana huenda hata sisi tungelikuwa kwenye hiyo hali tungelifany ahivyo hivyo..hata hivyo nawashukuru wazazi wako, kwani pamoja na hilo tukio lakini walitusaidia sana kimaisha...’akasema.

‘Mimi nilikutafuta sana, lakini sikutaka wazazi wangu walifahamu hilo, nilitaka kukulipa fadhila zako, niliahidi moyoni kuwa nikija kuonana na nawewe, nitafanya lolote na nimekkuona naomba usilipinge ombi langu....’nikamwambia.

‘Mimi sihitaji msaada wenu, ….’akasema

‘Hapana ni lazima nifanye wema wowote, nakumbuka kama isngelikuwa ni wewe..sijui ingelikuwaje, na….’hapo tena ndio lile tukio likazama kwenye ubongo wangu nikawa naliona lilivyotokea….

**********

Ilionekana wazo hao vijana watukutu, walikuwa wakinivizia siku nyingi, na siku hiyo gari la baba lilichelewa kuja kunichukua shuleni, nikaamua kutembea na wenzangu, na kwa vile shule ilikuwa mbali, wenzangu wakawa wametawanyika kila mmoja na njia yake, ikafikia mahali nimebakia peke yangu, na ghafla ndio nikavamiwa na vijana wanne, na kunibeba juu kwa juu.

Walinibeba juu kwa juu, hadi vichakani, na wakaanza kunivua nguo, na ukumbuke nilikuwa binti mdogo tu, nasoma sekondari..nilikuwa binti, nimeshavunja ungo, lakini sikuwa na mawazo hayo kabisa, na sikujua ni kitu gani kitakuja kunitokea,..japokuwa nilifahamu kuwa wanatka kunifanya kitu kibaya.

Nilijitahidi kupigana lakini sikuweza kufurukuta kwa vijana hawa wenye nguvu zaidi yangu, na kabla hawajafanya lolote mara akatokea mtu, kijana..machozi yalishatanda usoni sikumuone vyema, akawa anapigana nao, akiwa na kigongo hivi kama rungu, alipambana nao kiume mpaka anakuja kuwazidi nguvu, ilikuwa ni kwa msaada wa mungu tu maana wote walikuwa wakibwa zaidi yake…ikafikia muda, ikabidi wakimbie, baada ya kusikia kelele za watu, wakikaribia eneo hilo..na yule kijana akapiga ukelele kuomba msaada. Wale vijana wakakimbia huku wakilaani kuwa watahakikisha wananifanyia hivyo, siku yake...

Sikuweza kuongea nililia hadi nyumbani, nikiwa nimechafuka, nguo zimechanwa, nnipo kama nudu uchi…na huyo kijana alinsiindikiza hadi nyumbani, nikawahadithia wazazi wangu, na wao kwa haraka wakaifahamisha polisi na hawo vijana wakaanza kutafutwa lakini hawakupatikana kwa siku hiyo hata ya pili yake. Walihama kabisa, kijini hapo.

Cha ajabu wazazi wakaongea na polisi wakaja kumshikilia huyo kijana kuwa atakuwa anawafahamu hawo watu, na alitakiwa kuwataja, na aliposhindwa kuwataja, wakamshitakia kuwa ni muhusika wa tukio hilo, ..wanasema walivyomuhoji, alivyojieleza inaonekana kama analifahamu hilo tukio na yeye alikuwa mwenza wao, japokuwa alikana kabisa.

Baadae akafunguliwa mashitaka, na yote hayo wakati yanaendelea mimi nilikuwa sifahamu kinachoendelea kwani ilibidi niondoke hapo kijijini kwa usalama wangu, kwa vile walitishia kuwa ni lazima watanifanyia tena..ikabidi baadae wazazi wangu wanihamishe kabisa kwenda kusomea sehemu nyingine.

Nilikuja kusikia kuwa kijana huyo kafungwa, na nilikuja kufahamu hilo baada ya muda, mtu alishahukumiwa kufungwa..kwani vijana wale waliofanya hivyo hawakuweza kupatika,ila mmoja wao alipatikana na alipofika mahakamani, akadai kuwa kijana huo alikuwa mmoja wa wenzao, walipanga wote, kulifanikisha hilo, nay eye ndiye alitoa maelekezo jinsi gani wanaweza kumpata huyo bint.

Baba wa huyo kijana akawa anafika mara kwa mara kwa wazazi wangu kuomba kijana wake asamehewe, lakini haikusaidia kitu, na alichoambulia ni kufukuzwa kazi...hayo yote nilikuja kuyafahamu baadaye, na nilipolifahamu hilo nikawaambia wazazi wangu kama hawatamuachia huyo kijana aliyeniokoa basi mimi nitajiua...

Hilo nilidhamiria kweli…
 
SEHEMU YA 30

Wazazi wangu awali walifikiri natania, wakaja kunifuma nataka kunywa sumu, na walipoona hivyo, ndio baadaye wakaenda kuongea na polisi na baadae mahakama, kuwa kijana huyo aachiwe, wao wameshamsamehe..ili ifanyike maongezi, wanayojua wao wenyewe na ndio kijana huyo akaachiwa, hata alipoachiwa sikuweza kuonana naye tena wala baba yake, kumbe waliamua kuhama kabisa hapo kijijini, na baadae hata wazazi wangu wakahamia Dar, ndio ikawa mwisho wa kuonana na huyo jamaa hadi hii leo ndio nakutana naye…

***********.

‘Kwakweli sitaweza kusahau wema wako huo, uliniokoa kwenye janga, huenda ningelikufa, …’nilimuambia siku tulipokutana naye tena.

‘Ile ni kawaida tu, mtu yoyote muadilifu angelifanya hivyo hivyo, na haina haja, kulipwa kwa kitendo kama kile, na sizani kama kuna kitu unaweza kunilipa kikazidi yale ya moyoni kwangu...’akasema na kuinama chini.

‘Una maana gani,ya moyoni mwako, yapi hayo..… ?’ nikamuuliza.

‘Mimi niliahidi siku ile ulipoleta chai na mkate, nilikuambia mimi nitakuja kukuoa, wewe uliona kama utani, nilimuambia hata baba, alinicheka sana,..nakumbuka hata wewe ukasema mungu akipenda,..ukimaanisha kuwa umekubali au sio…’akasema

‘Lakini yale yalikuwa ya ujanani, na niliongea vile kama maongezi tu, ulitaka mimi niseme nini pale, na ni mambo ya ujanani, hayana maana au sio…’nikasema

‘Hayana maana, ndio unasema hivyo, kwangu yalikuwa na maana sana, mimi nilikupenda na …samahani, nikisema hivyo, kuwa siku zote nimekuwa nikikupenda, na kutamani uwe mke wangu, usichukie, ila naelezea hisia zangu, najua ni ndoto za Alinacha, lakini ndio ukweli kutoka moyoni mwangu…’akasema

‘Aaah, hapana,…sawa nashukuru kwa kusikia hivyo, na…hata sijui niseme nini, naogopa, nitakuja kuuumiza , naomba unipe muda..’nikasema

‘Hapana nafahamu, huna haja ya kusema lolote, haiwezekani, mtu kama mimi kukuoa wewe, najua, ila sijui …’akasema

‘Kwanini unasema hivyo…utampata msichana mwingine kwani mimi ni msichana peke yake hapa duniani..’nikasema

‘Sijaona kama wewe, na wewe ndiye uliyeuteka moyo wangu, kama sio wewe basi, mimi naomba mungu nisioe tena, na nitaishi hivi hivi maisha yangu yote…sitaki shida…’akasema sasa akisimama kuondoka. Hapo nilibakia nikiwaza, sikujua kabisa mwenzangu kadhamiria hilo, na..kiukweli moyoni sikupenda kuja kumuudhi mtu kama huyu, ambaye naona kama ananidai …

Moyo wa huruma uliniingia, nikikumbuka yeye ndiye aliniokoa, vinginevyo sijui ingelikuwaje, na zaidi ya hayo, ananijali sana, kiukweli docta nampenda, na kwa vile pia yupo kwenye hadhi inayoendana na …tusema hivyo..lakini huyo nimetokea kumjali, na labda kuna upendo lakini sio kwa vile…sasa nifanyeje..ilinipa wakati mgumu sana, nikijua kuna wazazi wangu, ambao hawatalisikiliza hilo kabisa

Basi siku hiyo akaondoka, na hatukuweza kukutana kwani nikifika naambiwa katoka, nikimpigia simu hapokei.

************

Baada kama ya mwezi hivi tukaja kukutana tena, tukaongea mengine , hakupenda kuliongelea hilo tena, nikajua keshakubali ukweli, kwahiyo hilo halipo tena, na huku kwa docta, naye kaanza kunisakama, anataka tuanze michakato ya ndoa..

‘Niambia, lile wazo langu vipi…?’ siku moja akaniuliza sikutarajia hilo swali.

‘Unajua, wewe unachukulia ndoa kama ni kitu rahisi hivyo, ujue mimi nina wazazi, na ndoa inakutanisha familia mbili, wakiwemo wazazi, sasa hebu jiulize, wazazi wangu wataliridhai hili,...je wewe umejiandaaje kuishi na mke, maana usije ukasema unanioa, kwa vile…’nikasema

‘Mimi nimeshajiandaa kwa hilo, sio kwamba nakuambia kwa vile…ninachumba na varanda nimepanga, nina kiwanja kijijini, urithi wa baba, nitauza seehmu nitajenga nyumba,…tutaweza kuishi tu..lakini sikulazimishi, maana kiukweli hutaweza kuishi maisha y akitajiri kihivyo...’ akasema.

Baada ya maongezi hayo, nikawaza sana, nikajiuliza sana, nifanye nini…maana sikuwa nimelichukulia kwa maana hiyo tokea awali,…nikaanza kujenga hisia za kumpenda tu…na huku kwa docta nikawa naharibu, ikawa siivani naye kwa kila anachokifanya.


‘Vipi kwani kumetokea nini, nakuona umebadilika sana siku hizi, kama kuna tatizo lolote niambie mimi nitakuelewa tu mpenzi, sitaki kabisa, kukulazimisha kwa lolote lile, umenielewa, sitaki nikuoe ukiwa hunitaki, unasikia, unieleze mapema…?’ akaniambia

‘Hakuna tatizo lolote!....’nikawa namwambia hivyo maana bado nilikuwa sijaamua moja kwa moja, nikijua kuwa wazazi wangu hawataweza kunikubalia kumuoa huyo

Nikawa sasa najenga ukaribu sana na huyo jamaa hadi docta akaja kugundua mwenyewe, na aliponiuliza nikamwambia ni rafiki yangu nakutana naye tu na hawezi kunizuia

‘Nimeshakuambia uwe muwazi kwangu, kama hupo na mimi , sawa, mapenzi hayalazimishwi, lakini nataka uwe muwazi, unanielewa, sitaki kupoteza muda wangu na mtu asiye na matarajia na mimi..’akasema

‘Sawa si unataka jibu, sipo na wewe,… nataka kufikiria zaidi, kama una haraka kuoa katafute mwingine....’nikamwambia hivyo, kiukweli ilimuumiza sana, na akavumilia kwa kipindi fulani, baadae akalifikisha kwa wazazi kuona kama wataweza kusaidia

Wazazi wangu waliposikia hivyo, hawakuamini…wakaamua kufanya uchunguzi ni nani kanighilibu, na baadae wakaja kugundua kuwa ni nani huyo ninayekutana naye mara kwa mara, na kipindi hicho nimeshamsaidia huyo jamaa hadi akapata kazi kwenye kampuni kubwa, na akaweza hata kujenga nyumba yake mwenyewe…nilitaka nifanye hivyo baadae…kama atampata mtu mwingine basi.

Lakini kumbe mwenzangu anajua kuwa nayafanya hayo kwa ajili ya maisha yetu ya baadae, kukapita kipindi kirefu hapo,…sio jambo la miezi, hapana ilichukua karibu miaka miwili hadi docta akakata tamaa na mimi....
.
Siku moja wazazi wangu wakanikalisha kikao, walikuwa wamekasirika kweli kweli..

‘Hivi wewe una akili kweli,..hivi wewe hujaona mwanaume, hadi umchague huyo mtu,..kama kweli nia yako ni kupata mwanaume mwingine zaidi ya docta, huyo hakufai, yule ni mlalahoi, mtoto wa mlinzi wetu...bwana shamba, asiye fanana kabisa na hadhi yako, mbona unataka kutuaibisha....kwanini unamkataa docta, msomi , familia yao ni ya kiheshima, matajiri.....’akasema baba.

‘Baba mimi sio mtoto mdogo, na sina lengo la kuwaabisha, mnakumbuka nilitaka kubakwa nikiwa kule kijijini, niliwaambia ni nani aliyeniokoa, ....mlifanya nini kwa huyo aliyeniokoa, ..badala yake mlikimbilia kumshika yeye ati alikuwa anawafahamu hawo watu waliotaka kunibaka, mkamfunga hata bila ya mimi kujua, kwa vile tu ni mtoto wa masikini..iliniuma sana na niliahidi kuwa ipo siku nikipata nafasi nitamsadia ili kulipa fadhila zangu kwake, na kutubu madhambi mliyoyafanya...’nikasema.

‘Kwahiyo malipo yake ndio hayo, kutudhalilisha sisi au sio...sikiliza, kama sisi ni wazazi wako, tunasema achana na huyo mtu, sisi ni wazazi wako tulijua ni nini tulichokifanya, wewe hukuona kilichotokea, baada ya kumshika yeye na kumfunga, kijiji pale tuliogopewa sana…, hakuna hata mtu aliyewahi kuichezea familia yetu tena....sisi tulifahamu ni nini tulichokifanya, kutoa fundisho kwa wengine....’akasema baba

‘Mtoe fundisho kwa mtu asiye na hatia,...kunikoa kwake ndio imekuwa taabu, kama asingelifanya hivyo nikabakwa, huenda ningelifikia kupoteza maisha au kuambukizwa magonjwa, mngelisemaje, ndio fadhila zeni hizo, wema wao ndio malipo yake hayo,hapana mlifanyavibaya sana…’ nikasema

‘Je na sisi tusingelifanya hilo, ikatokea tena, maana walidhamiria kweli kulifanya tena kukukomesha , na wale waliotoroka, walikamatwa wakiwa na mipango hiyo …walitaka hata kuja kuchoma nyumba na maeneo yetu..hujui kabisa yaliyokuwa yamepangwa …’akasema

‘Wazazi wangu hamuwezi kujua ubaya huo unaweza ukawageukia nyie wenyewe siku moja, …au ubaya huo uje utendwe kwa watoto wenu, ili iwe fundisho, ...hamjui kibao kinaweza kuwageukia nyie siku moja kwa tatizo jingine, hujafa hujaumbika...msijione kuwa nyie ni matajiri hamtaweza kupata shida, mung anaweza kuibadili hali bila kujua, kisa ni haya mnayoyaona ni madogo tu...’nikasema kwa sauti ya huzuni na mama akanionea huruma na kuniuliza

‘Kwahiyo ewe ulikuwa unatakaje, tukae kimiya tu, wakati wahuni walishaanza kuiingilia familia yetu, tulifanya vile kwa ajili ya kuilinda famila yetu, na tulipofanya hivyo ilisaidia. Na baadaye tulimtoa, na tukampa pesa za pole,...japokuwa mzazi wake alizikataa lakini baadaye akazichukua hali ilipozidi kuwa mbaya....ile ni kawaida kwa mzazi yoyote anayetaka kulinda familia yake...’akasema mama.

‘Mimi sitawaelewa kamwe, na mimi najua nafanya nini, itafikia mahali, nikiona kampata mtu wake, basi..lakini kwa hivi sasa sitaki kuolewa na docta…’nikasema,

‘Sasa unataka nini, maana huyo kijana keshasema anataka kukuoa,..lakini sisi kamwe hatutakubaliana na ndoa hiyo,…’wakasema

‘Baba mimi naona hatutafika popote kwa hili, ila nawaomba, ..kwa vile mimi ndiye niliyefanyiwa hilo, na namfahamu ni nani aliyenifanyia wema kwa kuniokoa, mniache tu, najua ni nini ninachokifanya, maana kwangu, alilonifanyia ni deni kubwa sana,..na.niliahidi kuwa nitamlipa fadhila zake, ....’nikasema.

‘Kwahiyo unataka kumlipa fadhila gani...?’ akauliza mama.

‘Hilo niachieni mwenyewe....sijaja kuwaomba chochote kwenu kwa ajili yake....’nikasema.

‘Achana na huyo mtu, kama unataka kumuona akiendelea na maisha yake, achana naye, na kama unataka akaishie jela, endelea naye....hatuwezi kukuona ukituzalilisha ....atapotea kama alivyopotea baba yake....’akasema baba.

‘Ina maana mnafahamu kuwa baba yake alifariki,,...?’ nikauliza kwa mshangao.

‘Tumeshakuambia achana na hiyo familia, vinginevyo utajua kwanini hukutusikiliza....’akasema baba, na mimi moyoni nikasema

‘Kama ni hivyo basi, nitakubali anioe, ili kuondoa kabisa hiyo dhana ya madaraja..najua wazazi wangu wamekosea, na hawataki kutubu, basi mimi nitatubu kwa niaba yao,na njia pekee ni kukubali kuolewa na huyu mtu basi…’nikapanga hivyo…

NB: Kisa ndani ya kisa….ndivyo kisa hiki kilikuwa …kama nawachosha mniambie..


WAZO LA LEO: Utofauti wetu wa hali za kiuchumi usiwe ni tija ya kutokujali utu wa mtu, utu wa mtu haununuliwi kwa pesa au mali, utajiri wako usiwe tiketi ya kudharau wengine, na kuwaoana hawana thamani, ukifanya hivyo,hutakuwa na amani katika maisha yako, kwani kilio cha hawo unaowatendea hivyo kitakuandama.
 
SEHEMU YA 31

‘Shemeji samahani nilikuwa nataka kukuuliza maswali kama hutojali...’ sauti hiyo ilinishitua kutoka kwenye dimbwi la mawazo ya maisha yangu yaliyopita.

‘Unaonekana upo kwenye mawazo mazito, pole sana, najua unavyojisikia lakini usijali mumeo atapona tu….lakini baada ya hili, nawashauri kwa nia njema tu mkae muone tatizo lipo wapi ….’Alikuwa ni docta ambaye alizoea kuniita shemeji.

Docta mara nyingi amekuwa mshauri wangu, hakujali yaliyopita kuwa tuliwahi kuwa wapenzi, hakujali, kuwa huyo mume wangu ndiye aliyefanya akanikosa mimi..ndio hapo unapoweza kumuona docta mtu alivyokuwa mtu wa peke yake.

Nikamwangalia machoni kabla ya kumjibu, na yeye kwanza akatabasamu, pili akaonyesha uso wa kushangaa, na kabla hajasema lolote zaidi nikasema.

‘Naomba usiniulize maswali ya kuzidi kuniumiza kichwa changu, maana leo imekuwa siku ya mikasa kwangu, hapa nilipo nina mawazo emngi sana....’nikasema.

‘Lakini, …mmh, naweza kusema haya yote umejitakia mwenyewe, usimlaumu mtu yoyote, wazazi walikuambia kuchia mimi mwenyewe, ..anyway, ...sitaki kurudi nyuma, lakini wewe mwenyewe unalitambua hilo...’akasema .

‘Ndio hayo siyataki kuyasiki, maana hayatanisaidia kitu,..nafahamu sana unamaanisha nini, lakini nikuambie ukweli, haya yanayotokea hayana msingi kabisa na mambo yetu ya nyuma, na unafahamu kabisa kwanini nilichukua uamuzi huo, na sitajutii kwa hilo...’nikasema.

‘Kulipa fadhila...eeh, haya endelea kulipa fadhila, kiukweli, mimi nimekuvulia kofia, upo tayari kuyaweka maisha yako, rehani…kwa sababu ya kulipa fadhila, na nini unakipata sasa, eeh, mimi nitaendelea kukusaidia tu, hilo nakuahidi …’akasema

‘Najua wewe na wazazi wangu mtasema hivyo sana, ..lakini hamjui ni nini kilicho moyoni mwangu, mume wangu nampenda na nilimpenda toka siku ile ya kwanza, nilipomuoana akiwa na hali yake hiyo hiyo ya umasikini..’nikasema

‘Sio kweli…uwadanganye wengine, lakini sio mimi…’akasema

‘Lakini kwanini unasema hivyo, mimi nimefanya kosa gani, kuwa eti kwa vile nimeolewa, mnayemuita wa daraja la chini au masikini,…hahaha, hebu niambie sasa hivi ana umasikini gani, mbona mpo sambamba kimaisha, ni hali ya kusaidiana na kuinuana,....’nikasema kama namuuliza.

‘Mimi sijakulaumu kwa uamuzi wako huo, lakini tabia za watu hazijifichi, zingine ni za kihistoria, hata ufanyaje ni kama vile wanavyosema, …mmh, kuwa kunguru hafugiki,.. na ndivyo maisha yetu yalivyo, misingi ya kizalia ni vigumu sana kuigeuza...unajaribu lakini ipo siku itatokea na tabia itajionyesha na kukuathiri...’akasema.

‘Tatizo lako wewe ni dakitari lakini ukifikia kwenye maswala haya unaacha udakitari wako pembeni, hutaki kuutumia hata katika mambo kama haya, kizalia kina nini na maswala ya mapenzi, ..kuacha kuolewa na wewe imekua ni nongwa, kwani huyo mkeo uliyempata humpendani...mbona mimi sijaingilia maisha yenu..?’ nikamuuliza.

‘Tuyaache hayo nataka kukuuliza mambo ya msingi, maana pamoja na yaliyotokea nyuma, bado nakuona wewe ni rafiki yangu, na mumeo ni rafiki yangu pia, ndio maana nilipogundua kuwa ndio yeye unayemtaka, sikutaka kupambana kwa vyovyote vile, niliona nikuachie tu, kwa vile ulinitamkia mwenyewe kuwa unampenda,..na ukaja kunitamkia kuwa mimi hunipendi tena…, nikaona kwanini ning’ang’anie mtu asiyekupenda,.....’akasema.

‘Uliza maswali yako bwana, sijasema kamwe sikupendi, nilikuambia sababu za uamuzi wangu, na unazifahamu sana ...’nikasema na yeye akaniangalia kwa muda, halafu akasema;

‘Nataka nikuulize maswali ya ndoa yenu,...’akasema

‘Kama ni maswali kuhusu ndoa yangu, ningelifurahi kama ungeyaacha kama yalivyo, kwani akili yangu haijatulia, siku ya leo imekuwa ni ya mitihani, tangia asubuhi, ni matatizo, ofisi matatizo..nyumbani matatizo, huko kwa rafiki yangu matatizo..’nikasema

‘Kwa rafiki yako kuna matatizo gani…?’ akaniuliza

‘Haya hebu niulize, tuyaache hayo, unataka kuniuliza kuhusu nini?’ nikasema nikijua ni yale yale ambayo mara kwa mara ananilaumu eti kwanini nilimkataa yeye nikaamua kuolewa na huyo rafiki yake.

‘Shemeji ...rafiki yangu…mpendwa…hahaha, wakati mwingine naogopa kuongeza maneni hapo..nikuambie kitu, iIli kuondokana na huko kuchanganyikiwa kwako ni bora ukajaribu kuyaongea hayo matatizo uliyo nayo kwa mtu anayeweza kukusaidia,..’akasema.

‘Hapana, mimi nakufahamu bwana, ...wewe na wazazi wangu siku zote mnaombea ndoa yangu ivunjike, hebu nikuulize, kwa mfano ndoa yangu ikivunjika utapata faida gani, maana wewe sasa una mke, utamuacha mkeo ili uje unioe mimi, au ndio mnataka kunikomoa...?’ nikamuuliza.

‘Hahaha..hivi wewe unafikiri mimi nachukia ndoa yenu, kuwa natamani ivunjike eti kwa vile ulinikataa, acha hiyo, mimi mumeo ni rafiki yangu,...unalifahamu hilo fika, na kama asingelikuwa ni rafiki yangu ningelipambana hadi nihakikishe nimekuoa, lakini niliona hakuna haja, kwanza umepata muda wa kumsaidi rafiki yangu ambaye katokea kwenye shida,....sitaki hata kumuongelea kuhusu maisha yake ya huko nyuma, na kwa kupitia kwako, nimeweza kulipa fadhila zangu pia...’akatulia.

‘Najua hilo mtalirudia kila siku...na hamtafanikiwa, maana sasa mnaishia kumuonea wivu, ana kampuni, ana maisha mazuri,..nini tena cha kumsuta , hakuna, iliyobakia sasa ni majungu, nashukuru kwa ushauri wako wa mara kwa mara sikatai, ila nisingelipenda unilaumu kwa uamuzi wangu huo...’nikasema.

‘Haya bwana, ngoja nikuulize hayo niliyotaka kukuuliza ili uone kuwa mimi najali sana ndoa yenu,...’akasema

‘Uliza, na nitakujibu,....lakini kama ni mambo ndani ya familia yangu,sitaki...’nikasema

‘Hebu niambie ukweli, mume wako alikuwa wapi, kwani watu walioona hiyo ajali wanasema mume wako alikuwa akiendesha gari kwa mwendo wa kasi sana...kama vile alikuwa akikimbizwa,au akikimbia jambo?’akaniuliza na mimi hapo nikashituka, nikikumbuka kuwa hata mimi nilifanya hivyo hivyo.

‘Unataka kusema nini hapo, kuwa mume wangu…ni mhalifu au…?’ nikamuuliza.

‘Nataka kujua kama unafahamu wapi mume wako alikuwepo leo hii, kabla ya hiyo ajali…kuna maswali mengi yanaulizwa, na yataulizwa na polisi pia, …?’ nikamuuliza

‘Kwani hawo watu wanasema alikuwa akitokea wapi...!?’ nikamuuliza huku nikiashiria kushangaa na sijui kwanini niliuliza swali hilo badala ya kujibu swali.

‘Shemeji mimi nakuuliza swali na wewe unaniuliza swali, kwani siku ya leo toka asubuhi, ...mliagana vipi, na mchana kutwa, hamkuwahi kuwasilina, hamkuonana, au kuambizana mnakwenda wapi, mnafanya nini....nafahamu unafahamu wapi alipokuwa akitokea au hufahamu?’ akaniuliza.

‘Sikiliza nikuambie, mimi na mume wangu tuna mishughuliko tofauti, kila mmoja akiamuka asubuhi anakwenda kwenye shughuli zake kivyake vyake, hakuna kufuatana..hayo ndio maisha yetu na sitaki uniulize kwanini maana hata mimi sijakuulizia kuhusu maisha yako wewe na mkeo, au sio…’nikasema.

‘Sio hivyo, ninachotaka hapa ni kuwasaidia, na wala sio kubomoa, na hata kama wewe ungeliona kwenye nyumba yangu kuna matatizo na kwa vile tunafahamiana, ungeliniuliza, ili uone kama unaweza kunisaidia au sio...’akasema.

‘Sijaomba msaada kwako, mimi na mume wangu tuna utaratibu wetu wa maisha na hatuna shida na hilo,, na haikuwa na umuhimu kuliulizia hilo, ni kama simuamini mume wangu..’nikasema.

‘Lakini mwenyewe kwa kauli yako hapa, umesema siku ya leo imekuwa na mitihani mingi,ukasema matatizo nyumba, matatizo kwa rafiki yako....hii inaashiria nini, kama sio mna matatizo wewe na mume wako, kwanini hutaki kusema ukweli nikaweza kusaidia, hata kiushauri tu...?’ akaniuliza.

‘Hatuna matatizo, na kama yapo ni ya kawaida tu , ya mume na mke..hayakuhusu, na kama yangelikuwa makubwa, ningekuuliza, mbona mara nyingi nakuuliza, au kuna jingine...’nikasema.

‘Sawa, bado hujanijibu swali langu, ....’akasema.

‘Swali lipi zilipendwa....?’ nikamuuliza na kucheka, yeye hakucheka, akasema;

‘Hebu niambie utaratibu wenu wa leo ulikuwaje, ..?’ akaniuliza na mimi nikamwangalia kwa makini, nikaona nisibishane naye sana nikamwambia;

‘Sisi utaratibu wetu ni kuwa, kwa vile kila mmoja ana kampuni yake, na ana mambo yake, tukiamuka kila mmoja ana hamsini zake, hatuaingiliani kabisa, wakati mwingine kama ni lazima ndio tunapeana taarifa, ...’nikasema.

‘Hiyo ni kwa ujumla je kwa leo ilikuwaje, ...?’ akaniuliza, na sikumuelewa ana maana gani, kwani maswali yake niliyaona kama ya polisi nikasema.

‘Ama kwa leo, nakumbuka aliniambia kuwa akitoka kazini anaweza kupitia kumona mke wa rafiki yake ambaye kajifungua, ...nakumbuka aliniambia kitu kama hicho, na sikuwa makini sana kumsikiliza maana nilikuwa na mambo mengine ya kikazi yalikuwa yamenitinga...’nikasema.

‘Mke gani wa rafiki yake, aliyejifungua…?..., alikwenda kumuona mzazi, au mume wa huyo mzazi, maana mimi nijuavyo mara nyingi mke akijifungua wanaokuwa karibu na huyo mzazi ni wanawake, kwahiyo ilitakiwa wewe uende naye....au nimekosea?’ akauliza

‘Kwahiyo unataka kusema nini hapo..?’ nikamuuliza
 
SEHEMU YA 32

‘Sitaki kusema kitu, ninachotaka ni ukweli ili niweze kusaidia,...kama ningelikuwa nataka kusema kitu, kwanini nikuzunguke, wakati wewe ni rafiki yangu, na mume ni rafiki yangu pia....’akasema.

‘Nakuuliza hivi kwa maelezo yako una maanisha nini kuhusu rafiki yako?’ nikamuuliza

‘Inawezekana hakuwa katokea kazini,....maana mimi nilimpitia na nikaambiwa kuwa ametoka mapema tu, kikao chao kilivunjika mapema, kuna mambo yalikuwa hayajakamilika, kwahiyo alitoka mapema ofisini kwake,...’akasema docta.

‘Mimi siwezi kujua mipangilio yake, na siwezi kutabiri kuwa alikuwa wapi, ...kama hakuwepo kazini, basi alikuwa kwenye shughuli nyingine nje ya kazini kwake, hilo linawezekana na hilo la kusema mzazi ni lazima muandamane na mke wako, halina mantiki yoyote kwangu…, wewe unachotaka hapa ni kujenga sababu ya kumuona mume wangu ana tabia mbaya....’nikamwambia.

`Shemeji lakini nakumbuka tulishaliongelea hili kabla, nilishawahi kuwakanya haya maisha yenu mnayokwenda nayo, ...sio mazuri kwa mke na mume, kiukweli kwa wanafamilia hilo sio jambo jema, hata kama mnaona kuwa huo ni usasa, au wengine wanasema ni uzungu...mimi siupendi. Mimi nawajali sana, kuliko unavyofikiria wewe....’akasema.

‘Nashukuru kama unatujali, na ningelishukuru kama unalosema linatoka moyoni na lina ukweli, kwani hata wazazi wangu wanasema hivyo hivyo, wakati walishatamka kuwa,....nikiendelea na mume wangu watahakikisha maisha ya mume wangu yanakuwa ni mashaka, na huenda akaishia jela...nikakumbuka kauli ya wazazi wangu wakisema;


‘Wazazi ni wajibu wao kumlinda mtoto wao, hata wewe ukifikia mahali pako, utasema hivyo hivyo kwa binti zako, hutapenda aende kuishi na mtu ambaye humuamini..’akasema.

‘Haya unatushauri nini Docta...’nikasema kwa dharau.

‘Mimi nasema hivi maisha hayo mnayoishi yana madhara yake hasa katika maisha yetu haya ya kiafrika,...miundo mbinu ni mibaya, hali za barabarani tunazijua wenyewe, usalama hauna uhakika, kwahiyo ni vyema kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na kila mmoja kumjua mwenzake yupo wapi na anafanya nini, kwani simu zina kazi gani?’ akaniuliza.

‘Unanichekesha kweli, ...yaani umefikia hatua ya kutudharau kiasi hicho...’nikasema

‘Lakini mwenyewe umesema kuwa kila mmoja ana mambo yake, na leo hukujua kabisa kuwa mume wako alikuwa na taratibu gani, za nje ya kiofisi....sasa utajuaje mwenzako yupo wapi, kama likitokea tatizo....’akasema huyo docta na mimi sikuwa nimemuelewa sana, nikamsikiliza tu aendelee kuongea.

‘Endelea doct-aah’ nikasema kwa dharau

‘Mimi siwapingi kwa utaratibu wenu huo wa maisha, lakini ni vyema mkajenga tabia ya kuambizana wapi mmoja anakwenda, sio kila mtu akirudi nyumbani yupo kwenye laptop yake ...kila mtu yupo bize, na kazi zake, mnasahau majukumu yenu ya ndoa...’akasema kama mzazi anayemuelezea mtoto wake aliyekosana na mkewe.

‘Umekuwa kungwi siku hizi au mwanandoa mzoefu, ...nyie mnajipa moyo kuwa ndoa yenu ipo safi eehe, haina matatizo au sio, unaiona ndoa yangu ndiyo yenye matatizo au sio....?’ nikamuuliza.

‘Mimi siwezi kujigamba kuwa ndoa yangu haina matatizo, yapo na kila ndoa ina matatizo yake, lakini yakizidi ni lazima tuambizane, ni mimi nawaasa, kama wewe ungeliniasha mimi ukiona utaratibu fulani sio mnzuri kwenye ndoa, hasa huo mnakwenda nao.’akasema na mimi nikahisi kukerwa na hayo maneno yake, niliona kama ananiingilia maisha yangu ya ndoa, japokuwa sikutaka kumkatiza, nikatulia tu.

‘Mimi kiukweli sifurahishwi na tabia hiyo, halafu rafiki yangu huyu, siku hizi anaonekana kunywa sana pombe, bila mpangilio, naufahamu unywaji wake, huu wa sasa ni ulevi, sio unywaji...’akasema na mimi hapo nikaa kimia tu.

‘Mimi nionavyo, ana tatizo, ana msongo wa mawazo, ...mimi kwasababu ya safari zangu za hapa na pale, sijaweza kukaa naye tukaliongelea hili kwa kina, ila kila muda nilipopata nafasi kidogo ya kuwa naye, nimemuona sio yule rafiki yule ninayemfahamu..hana raha, anaonekana anakerwa na jambo fulani..nahisi kuna tatizo ndani ya ndoa yenu..’akasema.

‘Wewe unahisi kuna tatizo kwenye ndoa yetu....kwani hiyo kuhisi imeanza leo?’ nikawa kama namuuliza

‘Ndio maana nataka tusaidiane kwa hilo,...kama kuna tatizo lolote niambie shemeji, hiyo dalili aliyo nayo rafiki yangu inatokana na msongo wa mawazo, shemeji jaribuni kukaa na kuliongelea hili nahisi kuna tatizo..ongeeni ambizaneni, ili muwewe kuishi kama wana ndoa, na sio wabia...’akaniambia huyo dakitari nikacheka kwa dharau aliposema `wabia...’

‘Eti eti unasema nini, ndio umefikia huko kuwa tunaishi kama wabia...dharau ya ajabu kabisa...’nikasema na kutulia

Nilitulia kwa muda bila kusema neno..hayo maneno ya mwisho yalinichefua,, hasira zikanikaba, maana sikuona tatizo lipo wapi, na sikupenda mtu aniingilie maisha yangu, hasa huyu, ambye alikuwa ni mpinzani mkubwa, kwa vile alitaka anioe yeye.

Mara akaja docta kutokea maabara, akapita na kuelekea kwa docta anayemuhudumia mume wangu, hakusema kitu.

‘Rafiki zilipendwa mimi sijui kama kuna tatizo kubwa kihivyo, kama yapo ni mambo ya kawaida ya mume na mke. …’nikasema

‘Una uhakika kweli na hilo unalolisema…?’ akaniuliza

‘Nikuambie kitu, yule ni rafiki yako, kama umeona kuna tatizo nenda ukamuulize yeye mwenyewe, umesikia sana...’nikasema huku nikionyesha kukerwa.

‘Shemeji ni sawa...sio kwamba nataka kuingilia maswala yenu ya ndani, hapana, ...na nafahamu kila tukiliongelea hili wewe unayaunganisha maswala haya na mambo yaliyopita, mimi nakuhakikishia kabisa sipo huko, nipo kwenye kuijali ndoa yenu,...’akasema.

‘Sawa, nimekuelewa…’nikasema, na aliona sitaki kuliongelea hilo, tukaa kimia kidogo baadae akasema;

‘Shemeji samahani nikuulize swali muhimu sana, nililokuwa nataka kukuulizia...usinielewe vibaya, na wala usilipeleke kwenye urafiki wetu wa zamani, ninachotaka kufanya hapa ni kujaribu kuangalia kama kuna tatizo maana nyie mnaweza msilione, lakini mimi kama docta ninaweza kuliona hata kama hujanielezea kwangu, nakuomba nikuulize maswali ya ndani ya ndoa yako, kama hutojali, ...’akasema.

‘Wewe uliza tu, sioni ajabu na maswali yako,..nitakujibu kama ninavyojua, ..lakini mimi siwezi kumjibia rafiki yako, yeye huenda anaweza akawa matatizo yake binafsi, lakini kama hajaniambai siwezi kuyajua,..kweli mimi ni mke wake, lakini kama mmoja atakuwa sio mkweli kwa mwenzake, basi hilo ni tatizo lake, na huwezi kukimbilia kumlaumu mke au mume, bila kujua undani wa maisha yao....’nikasema.

‘Shemeji sasa mimi nataka nijue undani wa maisha yenu,..niamini mimi, nina nia njema kwenu, kama mlivyoniamini siku ya ndoa yenu, kama rafiki mkubwa wa mume wako, kama rafiki yako mpenzi wa zamani, nataka niingie ndani ya ndoa yenu, nijaribu kuangalia undani wa ndoa yenu, kama kuna tatizo....tusaidiane’akasema.

‘Haya ....Unakaribishwa....ingia maana nimeshachoka kukuambia kuwa hakuna tatizo...sijui nikueleze vipi,..haya uliza hayo maswali ya ndani ya ndoa...’nikasema

‘Shemeji, je katika mambo ya unyumba mnashirkiana kama kawaida?’ akaniuliza swali lililonifanya nishituke na kugeuka kumwangalia usoni…huku uso umeonyesha kutahayari…

Na kabla sijamjibu, akaniuliza swali jingine,…

‘Na huko kwa rafiki yako kuna tatizo gani, je tatizo la huko kwa rafiki yako haliwezi likawa linaingiliana na matatizo mlio nayo nyie wawili,…?’ akaniuliza na mimi hapo nikabakia kimia, nikiendelea kumuangalia kwa uso uliotahayari….

‘Ukinijibu kwa uhakika…tunaweza kulitatua hili tatizo lenu, nina uhakika kuna tatizo, na...usipoangalia, utakuja kuniambia, je upo tayari kunijibu hayo maswali, tukasaidiana au..utaendelea kunificha,...?' akaniuliza

Nikainua uso na kumuangalia, ...na kabla sijamjibu, docta yule anayemuhudumia mume wangu akatokea....

NB: haya, mambo ndio hayo

WAZO LA LEO: Wakati mwingine unaweza ukawa na matatizo, lakini usijue kuwa una matatizo, wakati mwingine ndoa zinaweza zikawa na matatizo, lakini wanandoa wakajifanya hawana matatizo,…kila mtu akimtegea mwenzake, na kuona mwenzake ndiye anayestahiki kusema, au kulalamika…tukumbuke ndoa ni ya watu wawili, na wote wana dhima sawa ya kuona ndoa yao inasimama imara, tusijenge tabia ya kutegeana, kwani kukiharibika jambo, athari zitakuwa kwa wote, na familia yenu.
 
SEHEMU YA 33

‘Maswali gani hayo docta unayoniuliza, tulishawekeana mipaka kuhusu maswala ya ndoa yangu, na wewe ulishasema hutajaribu hata siku moja kuingilia ndoa yangu zaidi ya kusaidia kuijenga, au sio, sasa nikuulize…hayo maswala yako yanataka nini kwenye ndoa yangu, sipendi na sitaki, unanielewa…?’ nilikuta namuuliza kwa hamaki, lakini kabla docta hajasema lolote ndio akatokea huyo docta ambaye anamshughulikia mume wangu, na wote tukamsogelea.

Mimi nilikuwa sijamuona mapema hadi alipotukaribia…

‘Mpaka sasa hivi vipimo havionyeshi tatizo kubwa sana, matatizo yapo lakini sio ya kutisha,.tatizo ambalo limeonekana lipo kwenye uti wa mgongo, ambalo sio kubwa sana, ila inaweza ikachukua muda, kutegemeana na jinsi itakavyokuwa.., tutakuja kulijadili hili baadae,...'akasema docta

'Ila kwa hivi sasa itakuwa vigumu kwake kutembea, kuna athari hizo, lakini ni kwa muda,…na kuna vipimo vingine bado, havijawa sawa, ila kwa kifupi ndio hivyo…’akasema docta, na kabla hajaondoka docta huyu rafiki wa mume wangu akamsogelea wakawa wananong’ona kidogo.

Baadae yule docta akaondoka, na kutuacha tukitizamana, mimi nikamsogelea docta rafiki , nikamuuliza;

‘Ina maana mume wangu atakuwa hatembei tena, kwa muda gani …?’ nikauliza

‘Atatembea, ..ila kwa awali ni lazima atembelee kigari cha kukokota kwa mkono, hilo ni tatizo la muda, na kupona kwake kwa hivi sasa kwa haraka itategemeana na nyie wawili, hilo uwe makini nalo sana..’akasema

‘Kwa vipi..?’ nikauliza

‘Kwasababu pamoja na hayo, mawazo,…kutulizana kwa nafsi, kumliwaza na kumuondolea hofu, inategemeana na wewe ambaye mtakuwa naye karibu, ina maana hata kazi zako zingine inabidi uziache, ili asije akashikwa na msongo wa mawazo…’akasema

‘Mhh, sawa ni mume wangu hilo nalifahamu hata kabla ya kuambiwa, hata kama ni kuakia nyumbani siku zote mpaka apone nitafanya hivyo,..ila wasiwasi wangu, kama kaathirika utu wa mgongo mhh!!1…hata sijui nilitaka kuuliza nini…’nikasema

Pale nilizama kwenye mawazo, na wakati huo docta alikuwa akiongea na simu alipomaliza, akanisogelea na kuniangalia machoni kwa makini, halafu akasema;

‘Najua unawaza nini….lakini ndio hali halisi, …muhimu ni kujua huyo ni mwenzako, na kwa hivi sasa anahitajia ukaribu wako sana, kuliko wakati wowote, na nakuomba sana, usije kumkwanza kwa maswali mengi ya kumtia mashaka…’akasema

‘Maswali gani ya kumtia mashaka….mimi siwezi kuwa hivyo, mimi sio mtoto mdogo, najua wajibu wangu..?’ nikamuuliza na kusema;

‘Ndio maana nilitangulia kukuuliza yale maswali yangu ya awali, nilitaka uwe tayari kwa matokeo hayo, na nijue jinsi gani ya kukushauri, ili sije ikaendeleza tatizo…’akasema

‘Lakini kwanza nikuulize hayo matokea ya vipimo vyake yana athari gani zaidi, ok, mnasema atapona, je akipona, atapona kabisa au …?’ nikauliza nikiwazia mbali zaidi.

‘Kabla sijakujibu swali lako nakuomba unijibu yale maswali yangu , maana yana mingi mkubwa wa maisha yenu,…najua, na nilijua utakuja kuniuliza maswali kama hayo, ndio maana nilitaka uniweke wazi, …unelewe hapo,…’akasema

‘Mhh…’nikaguna hivyo

‘Sikiliza, unaniamini sio…mimi ni rafiki yako, na tulikuwa wapenzi, nakufahamu kama ninavyomfahamu rafiki yangu, nataka kusaidia,.. na nisipoweza kulisaidia hili , nitakuwa sijaweza kuwatendea nyie marafiki zangu haki, kwa vile nahisi kuna dalili fulani isiyo ya kawaida ndani yenu…’akasema

Mimi pale nikajikuta nimtulia na kuzama kwenye mawazo…kwanza nikijiuliza ni kwanini docta ameuliza maswali haya, ina maana labda mume wangu aliwahi kulalamika kwake kuhusu maisha yetu ya ndani..na hilo swali la pili,…hayo ni mambo yangu na rafiki yangu je huyu docta inawezekana anayafahamu, na kama anayafahamu kaambiwa na nani…maana mimi sijaongea na mume wangu kuhus hiyo siri yangu na rafiki yangu...

‘Unawaza nini…?’ akaniuliza, na sikumjibu, nikawa nimetulia tu, nikiendelea kuwaza;

Labda mume wangu aliwahi kuongea na rafiki yake kuhusu jinsi gani anavyotaka mtoto wa kiume, lakini hilo mbona halina msingi, sasa ni kwanini huyu mtu ananiuliza maswali haya… mahusiano ya kitandani yanamuhusu nini docta,..na sio kwamba anataka kuchokonoa ndoa yangu, ili iweje,… ni kweli nakiri kuwa nimekuwa mvivu wa hilo, lakini sio ....hapana, nahisi docta ana lake jambo, sitamkubalia …


‘Zilipendwa, hayo maswali yako yana jibu moja tu, kuwa hayo hayakuhusu kabisa, sijui kwanini unataka kuingilia maswala ya ndani ya ndoa ya mtu, unahisi sisi hatujui umuhimu wa ndoa,..au? au umetuona sisi ni watoto wadogo…au ….nashindwa kukuelewa….na nikuulize labda…huenda, mwenzangu alishawahi kuja kukulalamika lolote kwako,.....?’ nikamuuliza

‘Sikiliza mimi nayafahamu hayo yote kabisa,…’akasema

‘Kwahiyo kumbe alishawahi kukuambia, eeh, si ndio hivyo…?’ nikauliza nikipandisha sauti.

‘Sikiliza…nazungumzia kuhusu ndoa, na masharti yake ni kweli kuwa siri ya ndoa ni ya wana ndoa wenyewe…, ila mimi nimeuliza hayo maswali, sana sana sio kama docta, lakini pia kama rafiki yenu mpendwa, naweza kuhusika katika kuwasaidia, kwa nia njema kabisa, lakini kama utaona haina haja haya..sawa,lakini mimi sitachoka kuwasaidia…’akasema.

‘Mimi nakuuliza hivi, je rafiki yako aliwahi kuja kukulalamikia kuwa mimi simtimizii haki zake za ndoa, na ..hayo yanahusikanaje na hiyo ajali yake…kuwa alikuwa na mawazo hayo, hahaha, docta mengine naona hayahitajii udocta kuyafikiria, niambie ukweli, …?’ nikamuuliza.

‘Hajawahi kunilalamikia, hilo nikuambie ukweli, siwezi kukuficha , nikijua wewe ulikuwa mpenzi wangu, na sasa ni rafiki yangu, na tuliahidiana kuwa tutasaidiana kwa heri na shari, …mimi nataka kutimiza ahadi yetu hiyo sio zaidi ya hilo, suije kumfikiria mumeo vibaya, hajaniambia ....’akasema docta.

‘Kwahiyo hizo ni hisia zako tu,ambazo nahisi umezijenga tu, kwa vile....’ nikakatiza.

‘Hahaha,..eti kwa vile..malizia basi…! Sikiliza nikuambie..eeh, usiwe na dhana hiyo , narudia tena, nimekuuliza nikitaka kuwasaidia tu, kwasababu mimi siwezi kamwe kuingilia ndoa yenu,…kwanini nifanye hivyo, wakati nina mke tayari, ili iweje… na wakati wote nimekuwa nikiwasaidia,..leo kwanini iwe ni ajabu,… na maswali yangu hayo yamelenga katika kuwasaidia, kuna kitu nataka kukihakiki kwanza…’akasema

‘Zilipendwa, rafiki , mpenzi wa zamani… kiukweli swali lako hilo, linaingilia mambo yetu ya ndani ya familia siwezi kukujibu, kwani jibu lake lipo wazi...kama kungelikuwa na tatizo juu ya hilo, ningeshakuambia…eeh, na kama mimi ningelikuwa nimekiuka hayo, na nikawa sitimizi wajibu wangu kwake, yeye kama rafiki yako, angelikuja kwako kulalamika, kuwa nimekuwa mkaidi, je aliwahi kufanya hivyo, mbona unakwepa kunijibu hilo?’ nikamuuliza.

‘Hajawahi kufanya hivyo …hiyo dhana nimeiweka nikiwa na maana ya ujumuisho, kuwa mara nyingi, wanandoa wanaweza wakawa na matatizo kama hilo…, wakanyamaza, na wengine hasa wanaume wakalichukulia hilo kama kisingizio, kwa siri na kuanza kutoka nje ya ndoa, badala ya kulitafutia hilo tatizo ufumbuzi wake....’akasema.

‘Unasema hivyo ukiwa na maana gani, umeona dalili zozote kama hizo kwa mume wangu, kuwa anatoka nje ya ndoa?’ nikaumuuliza.

‘Nimesema kwa ujumla wake, nielewe hapo… sio kwa mume wako tu...nimesema kuna wanandoa wana matatizo kama hayo, na hawataki kuwa wawazi kwa wenza wao, na matokea yake, hasa wanaume, walio wengi, wanajikuta wakitafuta nyumba ndogo, na wengine wanakuwa walevi kupindukia…, na matokeo yake ni kuzaa nje ya ndoa.....’akasema.

‘Kwa, …kwa..hiyo…unasema kusema nini, ku-ku-kuwa mume hapana sio kweli na sitaki kusikia hilo…?’ nikauliza kwa hamaki

‘Hiyo ndio hali halisi kwa wanaume,…sijasema kwa mume wako…na ni kweli wanaume wanakosea kufanya hivyo, swali tujiulize wenyewe wakikosea ni nani anaumia…usipoziba ufa unakuja kujenge nini…na wanawake mnalijua hilo, lakini mnaweza kukutana mkashauriana mambo ya kuumiza ndoa zenu wenyewe..’akasema

‘Eti nini..ni nani kakuambia hilo…zilipendwa, kama akili zetu zitajikita kwenye maswala hayo ya ndoa, ya mahusiano ndani ya familia,…aah,… mambo ya kindoa, mapenzi ya ndani..sijui…, hatutaweza kabisa kupiga hatua za kimaendeleo, maana hilo sio tatizo, na lini iliniona nikikaa na wenzangu kuongea mambo hayo, unanifahamu nilivyo…’nikasema

‘Sawa nakuelewa sana huna tabia hiyo ya kukaa ndio, …ila naelezea hali halisi ilivyo yanatotendeka katika jamii, na sisi na wanajamii, au sio, na sioni kwanini ujishuku , maana mimi sijakushuku wewe bado, nakuulizia tu, kwa nia njema kabisa…’akasema

‘Najua nyie wanaume, kitu muhimu kwenu ni, .. hilo tendo au sio…, jamani…hilo tendo kwenye ndoa ..ni.. ni kitu kidogo tu, kwanini mnakiona ni kitu cha msingi sana,..cha kusingizia,..kwanza mimi sitaki kabisa kulijadili hilo, kama nyie mnaona hilo ni la msingi kwenu, haya shauri lenu,…na, na nikuambie kitu...kama mtu ana tatizo kwa hilo, kwanini haniiambii...’nikasema.

‘Hakumbii nani, una maana mume wako,…sasa sikiliza nikuambie hilo sio jambo dogo…unaliona hivyo kwa hisia zako, labda kwa vile muda mwingi upo kwenye shughuli zako, na shughuli zako umezifanya ni muhimu sana, kuliko hiyo ndoa, ndio maana hulitiliii maanani, na matokea yake mnajisahau, na kulisahau hilo jukumu la msingi wa ndoa..na nakuambie kitu, usilipuuzie hilo kabisa, maana madhara yake yanakwenda kuleta matatizo mengine makubwa,....’akasema.

‘Tuyaache hayo,..., hata kama wewe ni dakitari, hatujafika kwako kukuambia tuna matatizo kama hayo…na mimi silioni kama lina maana kuliongelea hapa, maana kila mwanandoa anafahamu umuhimu wake, na wajibu wa kila mmoja kuwa muwazi kwa mwenzake, hilo eeh ndilo la msingi…, kama mmoja akiwa kimya, akajitwika matatizo yake mwenyewe, utasema nini hapo?’ nikamwambia.

‘Sawa, endelea naona unataka kunielewa…unataka kusema rafiki yangu hayupo muwazi kwako au sio…?’ nikamuuliza.

‘Sijasema hivyo…ila nimekuuliza swali, je rafiki yako kakulalamikia, je alifika kwako akasema kuwa mimi simtimizii hayo mambo…kama kakulalamikia basi, una haki ya kuniuliza lakini kama hajafanya hivyo, na ni wewe unajenga hisia zako tu, unakosea…’nikasema

‘Hajaniambia, ila nahisi hivyo, kwa vile nakufahamu na yeye namfahamu pia,…na unaweza kuona ni tatizo dogo kumbe kwa mwenzako ni tatizo kubwa…’akasema
 
SEHEMU YA 34

‘Hakuna kitu kama hicho, kulikuwa na matatizo madogo na hayo tulishayaongea na mwenzangu, yanahitajia muda, sio lazima niyaseme kwako. Kama ni hayo, japokuwa zizani kama ni hayo, sizani maana ni kitu kidogo cha ndani ya familia…’nikasema hasira.

‘Kwa jinsi ulivyotahayari... shemeji naona kuna tatizo zaidi ya hilo...na hali kama hiyo nijuavyo mimi kwa wanaume wengine wanaweza kuitumia kama mwanya, au kisingizio cha kwenda nje ya ndoa, naomba unielewe hapo...siwezi kusema rafiki yangu yupo hivyo, maana sijawahi kumuona akiwa na tabia hiyo,, ....’akasema huyo dakitari bila kujali jinsi gani nilivyomjibu kwa hasira.

Sikusema kitu hapo ,nikampa nafasi aendelee kuongea, kwakweli alijaribu kuongea kwa upole, kama ujuavyo madakitari wanaofahamu kazi yao vyema.

‘Ila kiukweli naweza kuliweka wazi hili kuwa yule rafiki yangu, yule niliyemfahamu enzi hizo, sio huyu wa sasa, nahisi kuna tatizo, tena inaonekana sio tatizo dogo kama wewe unavyolichukulia hivyo…, na nahisi kuna chanzo, na wewe unakifahamu ila hutaki kuniambia...’akasema na kuniangalia machoni , mimi nikamkwepa na kuangalia pembeni.

‘Hakuna tatizo bwana, usikuze mambo, …’nikasema

‘Una uhakika na hilo, unasahau awali ulisema siku ya leo imakuamkia vibaya, matatizo nyumbani, kwa rafiki yako, umesahau au ? …’akasema

‘Si nimeshakuambia hakuna tatizo, ni ya kawaida tu, sio ya kuambizana kwa kila mtu, na hilo la mwenzangu la kutaka …kuzaa..mmh, kama kakuambia hivyo, kuwa anataka tuzae , tupate mtoto wa kiume, kwani mimi ndio napanga hilo, kuzaa tutazaa, na sio lazima awe wa kiume au,..si ndio hivyo ? alikuambia hivyo au…’nikajikuta nasema hivyo, na kumuuliza…

‘Umeona eeh….hilo ulikuwa unanificha, kwahiyo kumbe, wewe umekuwa mbali na yeye labda kwa vile hujawa tayari kuzaa, na mwenzako , kwa kauli yako, anatamani kupata mtoto wa kiume kwa vile sasa hivi mna mabinti, au sio…?’ akaniuliza

‘Mimi naona tuyaache hayo…unaonaje tukaongelea kuhusu hiyo ripoti ya docta, inasemaje je matatizo hayo ya mume wangu yanaweza kuleta athari gani baadae..?’ nikauliza kukwepesha huo mjadala.

‘Siwezi kuyaacha hayo, maana yanaweza kuwa msingi mnzuri wa wewe na mwenzako hata hiyo ripoti ya dokitari ikija, itakuwa ni ahueni kwako, utajua kipi ufanya na kipi ukikwepe unanielewa hapo..?’ akasema

‘Sijakuelewa, na huenda kama ni hivyo unavyofikiria wewe sitakuelewa au unataka nini hasa labda una lako jambo…?’ nikauliza kwa hamaki

‘Majibu ya vipimo vya mgonjwa ni kitu kingine lakini ninachotaka mimi kwasasa eeh, ni wewe uwe tayari kwa vyovyote itakavyokuwa, kwa ajili ya kumsaidia mwenzako,…tunaweza kuongea haya kama akiba tu, ili kupunguza mawazo yako ,na usisahau kuwa tumekuwa tukiambizana matatizo yetu na kusaidiana kiushauri, sasa iweje hili, unifiche …’akasema

‘Mhh, hapo nahisi wewe waniuliza ukiwa umeguindua jambo, na sasa unachotaka wewe ni kunichimba ili tu isionekane wewe unajenga fitina, na labda kunifanya mimi nisije kuumia baadae, au wewe kuna kitu unataka kukichimba ndani ya ndoa yangu yangu kutokana na tetesi za watu tu…, unataka kuhakiki kitu gani maana sio tabia yako ninayoifahamu mimi…’nikasema

‘Kawaida yangu sitaki kubuni, na mimi sio mtu wa kusikiliza tetesi, unanielewa nilivyo, katika urafiki wetu, siku zote nimekuwa nikikuasa kuhus hilo, mimi nataka uhakika kutokana na vipimo, na ndio maana nimekuuliza maswali muhimu yanayoweza kugusa hoja yangu..na nia ni kusaidia hili tatizo la mumeo..lakini msingi wa yote ni kwanini tatizo hili likatokea,..nahisi sio ajali tu,..nahisi kuna chanzo, nahisi kuna tatizo, kati yenu wawili,....’akasema

‘Kama ni hivyo basii nimeshakujibu au, kuwa hakuna kitu kama hicho, tupo sawa, na maisha yetu ni ya kawaida tu, umeridhika sasa...’nikasema

‘Hdi hapo sijaridikika,..sawa, labda nikuulize hili swali la pili, huko kwa rafiki yako kulikuwa na tatizo gani, maana ulisema wewe mwenyewe kuwa kuna matatizo kwenye familia na huko kwa rafiki yako pi… si ulisema hivyo…?’ akaniuliza

‘Yaaah…lakini sio kwa ukubwa huo…’nikasema

‘Hata kama sio kwa ukubwa huo, nakuuliza tu, je huko nako kulikuwa au kuna matatizo gani..?..., hebu niambie ukweli, maana huenda hayo matatizo yakawa na mahausiano fulani…yawezekana…ikawa hivyo.., wewe ukashindwa kutambua kwa vile yule ni rafiki yako…?’ akaniuliza na hapo nikashituka na kumwangalia machoni, na moyo ukaanza kunienda mbio,....ni kama kuna hisia inataka kujijenga na mimi siikubali.

‘Ni ya kawaida tu…’hatimaye nikasema, baada ya kutulia kidogo

‘Je mume wako wakati anapatwa na ajali alikuwa katokea wapi…?’ akaniuliza

‘Sijui…’ nikasema hivyo, maana kiukweli sijui.

‘Una uhakika hakutokea huko kwa rafiki yako…’akasema

‘Kwa rafiki yangu,..hapana bwana…. hilo nina uhakika nalo, maana mimi mwenyewe nilikuwa huko kwa rafiki yangu..’nikasema sasa nikiwa makini na uhakika.

‘Swali ambalo ninataka tusaidiane, najua nitakuja kumuuliza huyo rafiki yangu na nitafahamu kila kitu, ila kwa upande wako ni mhimu zaidi ukaliweka wazi, nakuuliza nikiwa na maana yangu na wala usinielewe vibaya….’akasema

‘Umeshauliza na umeshapata majibu yake unataka nini tena…’nikasema

‘Yule mtoto wa rafiki yako, …baba yake ni nani…?’ akaniuliza na mimi hapo nikageuka kumuangalia machoni, na yeye akanikazia macho, na ikawa mimi ndiye niliyekwepesha macho yangu, na baada ya muda nikasema;

‘Sijajua bado, hajaniambia…na, kwanini umuulize rafiki yako, au una maana utamuliza rafiki yangu..sijakuelewa hapo,…’nikasema kwa upole.

‘Basi, kama hajakuambia, …basi tuliachie hilo hapo, na kama kuna kitu unanificha ni bora uniambie mapema niweze kukusaidia kimawazo…’akasema

‘Kwanini ukaniuliza mimi hilo swali, kwanini, usingelienda kumuuliza mzazi mwenyewe, maana ni kama vile unahisi mimi nahusika na mimba yake au , eeh,..…unataka kuweka fitina gani ndani ya ndoa yangu…’nikasema

‘Fitina,!!!…hahaha, hapana, mimi au mwingine !!!?’ akauliza kwa mshangao

‘Ndio, umeanza kusema mume wangu alitoka kwa rafiki yangu, kiukweli hajatokea huko, maana mimi nilikuwa huko,…hapo ukashindwa kukamilisha fitina yako,..au dhana yako potofu dhidi ya rafiki yako, na rafiki yangu, halafu ..unafikia kuniuliza mtoto wa rafiki yangu baba yake ni nani….huoni hapo unataka kujenga fitina…’nikasema

‘Na ungelijua, usingelisema hivyo, kwasababu wewe ni rafiki yangu kama alivyo mume wako…na nimekuwa karibu sana na rafiki yangu , mambo yake mengi huwa ananiambia, lakini ikafika muda, ikawa nikimuuliza maswali hataki kunijibu…nikajua kuna tatizo..mimi naweza kuligundua hilo hata kabla hamjaniambia,…lakini nitatoa kauli ya uhakika nikipata uthibitsho, ndio maana nikakuuliza, ili kuondoa hisia mbaya…’akasema

‘Kwahiyo umeshaupata ukweli au sio, sasa ondoa hizi hisia mbaya au kuna jingine…?’ nikamuuliza

‘Bado..sijarizika na majibu yako…, maana hujanijibu kwa uhakika kile nilichokuuliza, unakwepa kujibu swali……’akasema

‘Majibu gani unayo-yataka wewe sasa, mbona siku hizi unaanza udukuzi....sasa sikiliza nikuambie , mimi sitaki,…. na nakuomba tena na tena..huko unapokwenda ni kubaya, sana, mtakuja kukosana na rafiki yako kwa mambo yasiyo kuhusu, kwa ushauri wangu, hilo jambo usiliingilie kabisa, na liishie hapa hapa…’nikasema

‘Hilo jambo lipi sasa…?’ akaniuliza

‘Kuhusu sijui mimi naishije na mume wangu, au, mahusiano yangu na rafiki yangu, au mtoto baba yake ni nani, hayo mambo umeyaanza lini , mbona unabadilika sasa, hayo kiufupi ..hayakuhusu ..kabisa, hayo yaache, na sijawahi kufika kwako kuomba msaada…’nikasema

‘Utakuja tu siku yake..ndio maana nataka kabla haijafikia huko,…nijue wapi pa kuanzia, ila nina uhakika ipo siku utakuja kwangu……si tupo…’akasema

‘Kwanini unasema hivyo, nahisi kuina jambo unalijua hutaki kuniambia…’nikasema

‘Kama mimi ninavyokuhisi wewe, kuwa kuna jambo unalijua, linakusumbua wewe na mume wako, lakini hutaki kuniambia..sasa tukubaliane, uniambie ukweli, ili na mimi niweze kuhitimisha nadharia yangu, kwa nia njema kabisa,…ili tuweze kuweka akili zetu kwenye kumsaidia mwenzetu, hali aliyokuwa nayo inahitajia msaada wetu sote…sawa, utaanza kuniambia au tuache tu..?’akasema kama kuniuliza

Hapo nikawa sina jinsi, …


NB: Choko choko za docta zitasaidia kuuvumbua ukweli, je docta anauliza hivyo akiwa na msingi gani, je huenda anajua ukweli fulani….mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu inakuwaje.....?



WAZO LA LEO: Ndoa nyingi zimekuwa na sintofahamu kwasababu ya kuzarau mambo muhimu kwenye ndoa, na mengine yanaonekana ni madogo au tunayaona hayana maana kwetu… , na mengine ni msingi wa ndoa, lakini wengine wanayaona ni ya kawaida tu ..kama wana ndoa, ni vyema mkayaongelea, maana dogo kwako linaweza likawa kubwa kwa mwenzako, na kama hamtayaongelea wenyewe ni nani atawaongelea, kwanza ongeeni wenyewe, mkishindwa ndio mtafute msaada.
 
SEHEMU YA 35

Hatukuweza kuafikiana siku hiyo, hadi siku nyingine tukakutana tena hospitalini, na docta akafufua yale mazungumzo yetu…

‘Unakumbuka nilikuuliza jambo, tukawa hatukuelewana…nahisi hukunielewa dhamira yangu,..nimeliwaza sana hilo nikaona ni lazima tuliongee na tufikie muafaka, sijui unanielewa….?’ akaniuliza na mimi nikawa nimeinama nikiwaza mengi kichwani. Nimekuwa mtu wa mawazo sana kiukweli. Sipati usingizi kabisa, na nahisi itanieletea matatizo, kwahiyo nikaona ni vyema nisikilizane na docta tu..

‘Lakini, mimi sijaona kosa langu, sijaona kuwa nina matatizo kihivyo…, sioni kabisa, kichwa changu kimetaliwa na kazi zangu za kiofisi mambo mengine ni ya kifamilia zaidi, ni mambo ya kawaida tu na nina imani yataisha tu…,sasa ukiniambia nikuambie kila tatizo la familia yangu unakosea….’nikasema


‘Shemeji, umesema una matatizo ukayataja matatizo kuwa yapo matatozo ndani ya nyumba yako..ambayo uliyaita ni ya kifamilia, ambayo naona umeshindwa kuyasema ni matatizo gani, kwangu nahisi huenda yakawa ndio chanzo cha yote hayo mengine..sijui lakini nahisi hivyo, maana hujanifafanulia...’akasema na mimi nikawa nimetulia tu.

‘Lakini pia ulisema kuwa kuna matatizo ya huko kazini kwako, hayo ukasema ni matatizo ya kawaida tu ya kikazi , au sio, siwezi kuingilia mambo ya utawala wako wa kikazi, sawa nimekubali kwa hilo, huko ni kwako na utaalamu wako…?’

‘Yap…ya kawaida..napambana nayo, …’nikasema

'Hata hivyo nakushauri, hayo mambo ya kikazi, usiyaweke akilini sana, yakawa ndio kipaumbele chako, kiasi kwamba yanameza maswala ya familia yako, kwani unafany akzi ili iweje, ni kwa masilahi ya familia yako, au sio…sasa ukiumiza kichw ahuko, kazi, ukaupa mgongo, ndo ayako utakuwa umefanya nini…unielewe hapo…’akasema

‘Sawa nimekuelewa docta….’nikasema

‘Lakini kuna hili,…ulisema kuwa kuna matatizo huko kwa rafiki yako,…kuna kitu nataka tuje kukijadili, sio kwa utesi,..sipendi tabia hiyo, bali nataka tujenge na kuondoa tatizo kama lipo…kwa kulianza hili je huko kwa rafiki yako kuna tatizo gani hasa la kukusumbua kichwa, maana huyo ni rafiki yako, kama nilivyo mimi, au sio…,?’ akaniuliza

‘Huko kwa rafiki yangu ni matatizo ya kawaida pia, wala yasikuumize kichwa, yule ni rafiki yangu namuona kama mdogo wangu , japokuwa tunalingana ki- umri. Kwahiyo mimi kama mzazi lipo ndani ya uwezo wangu....’nikasema na yeye akaendelea kusema;

‘Hata kama ni ya kawaida...kama unavyodai, kitu ambacho sikiamini, kwa vile umeshataja kuwa ni matatizo, ina maana yapo akilini mwako, na yanakusmbua akilini, na yanaweza kukupa matatizo, ukadondoka kwa shinikizo la damu, huwa inatokea, sasa isje kufika huko,…’akasema na nilikuwa sijamueleza kuwa nilipoteza fahamu.

‘Mhh, hata sikuelewi, …kwanini lakini, au kuna kitu unakijua mimi sikijui, kwanini usiniambie tu, kuliko tuzunguke zunguke…’nikasema

‘Kuna kitu nahisi kuwa kipo kati yako wewe na mume wako hujaniambia…, na kuna tatizo kati yako wewe na rafiki yako, nataka kulijua hilo, kuna kitu ambacho ungeniambia, ningeliweza kuhitimisha hilo ninalolifikiria mimi na tukaangalia njia sahihi ya kulitatua…, lakini kawaida yangu kama unijuavyo,…sipendeleo haya, nimekusihi uniambie wewe kwa vile ni rafiki yangu tu, la sivyo nisingelihangaika kabisa…’akasema

‘Ndio maana nakushangaa naona kama umebadilika siku hizi…, sio kawaida yako, kwanini uyatake haya ya watu, kuyafahamu,… na mwenyewe mara kwa mara umekuwa ukinikanya kuwa nisiwe na tabia ya kufuatilia mambo ya watu wengine.., na nisiwe mtu wa dhana mbaya kwa watu, au sio wewe…’nikasema

‘Hili sio la dhana mbaya…, ila mimi nataka nikusaidie ili baadae usije kunilauamu, najua kabisa baadae unaweza kunilaumu, kuwa huenda, nahusika, huenda nilijua, nataka nijitoe kabisa, lakini ni muhimu kwangu kulitatua hili kadri inavyowezekana…sasa hebu niambie…huyo rafiki yako, ana kukwanza nini, ni kuhusu ndoa yako…?’ akaniuliza tena

‘Ananikwanza,…!!! Sijasema hivyo… Nani kazungumzia kukwazana kwenye ndoa hapo!!!…nikuambie ukweli, huyo rafiki yangu hahusiani kabisa na lolote katika ndoa yangu,...nakuomba usije ukamuhusisha rafiki yangu na haya maswala yangu,..hahusiki na lolote lile..hilo nakuthibitishia...hayo matatizo niliyosema kuhusu mimi na yeye, ni matatizo ya kawaida tu kati yangu mimi na yeye, hata mume wangu hajui...’nikasema.

‘Nikuulize kitu, unakubaliana na mimi kuwa mume wako yupo karibu sana na huyo rafiki yako..?’ nikauliza

‘Ndio hilo halina siri..ila kwa vipi sasa …kwa jinsi unavyofikiria wewe unakosea, sivyo hivyo, acha hilo…’nikasema

‘Nisawa nitaliacha, ila…, nataka kuwa na uhakika tu kuwa hilo umeliridhia, kuwa mume wako yupo karibu na rafiki yako, wanakula pamoja, wanatoka wakati mwingine pamoja…na imekuwa sipo karibu sana na yeye kwa vile wanakuwa na huyo rafiki yako,.utasema labda nawaonea wivu, hapa…sasa ,.je hilo halina wivu kwako wewe, na sio sababu ya matatizo yako na rafiki yako, …wivu labda..?’ akauliza.

‘Karibu sana kwa vipi…ndio, kama umewaona wanaongea, au wanakula chakula pamoja, ni kawaida tu, tumezoea hivyo, wala usiwafikirie vibaya, siwezi kabisa kuona wivu kwa rafiki yangu, kuwa na mume wangu hivyo, na sizani kama inaweza kwenda zaidi ya hivyo, mengine ni dhana zako potofu, na ni wivu wako unakusumbua….’nikasema

‘Kama ni hivyo, sawa, kama umeliridhia hilo, sawa…na sio kwamba nawachimba, au wivu kama unavyodai, hapana, ndio maana nilitaka uhakika kutoka kwako, nilijua hayo matatizo na rafiki yako huenda ni maswala ya wivu, ok sasa…ili tusaidiane, na mimi nirizike, eeh, ..maana kuna kitu kinanitia mashaka…’akasema

‘Kipi hicho kinachokutia mashaka, kuhusu rafiki yangu na mume wangu au…?’ nikauliza

‘Rafiki yako naona kakimbilia kuzaa kwa kuchelea umri, au sio, ni sawa maana aliwahi kuongea na mimi, kuhusu hilo, na mimi kama dakitari nikamshauri kuwa ni bora aolewe mapema, maana umri umekwenda, akasema yupo mbioni kulitatua hilo, nikajua keshapata mume , sasa naona kazaa, simuoni huyo mume…’akasema

‘Ndio hivyo hakuna shida, au ulitakaje wewe,…?’ nikamuuliza

‘Nilimuambia awe lakini awe makini sana na mawazo hayo…maana yanaweza kumpelekea akataka kuzaa tu, kwasababu ya kukimbizana na umri…lakini hakutaka kuongea na mimi zaidi, ni kweli kuna muda alikuwa karibu sana na mimi, mpaka watu wakatushuku vibaya, hata mke wangu, nikaona aah, tukakosana...’akasema

‘Ndio niliwaona mkiwa sambamba, lakini mimi nilijua mumarafiki tu kama alivyo karibu na mume wangu, japokuwa …alikuja kuniambia ulimtaka kweli si kweli…’nikasema

‘Hahaha, hayo yaache, sasa ni hivi, maana wewe ndiye rafiki yake, kwanini akaamua kuzaa bila kufunga ndoa, ulimshauri wewe hivyo, na je baba wa mtoto wake ni nani?’ akaniuliza huku akiniangalia kwa macho ya udadisi, na mimi kwanza nikaguna, halafu nikaangalia pembeni na kusema;

‘Hilo hata mimi sijui..labda baba wa mtoto ni wewe,maana mlikuwa marafiki au sio, sasa sijui ,.. au ndio maana unataka kuchunguza kuhakiki kama mtoto ni wako au ni wa matu mwingine…’nikasema.

‘Aaah, sio wangu bwana.. .kama angelikuwa ni wa kwangu angelifanana na mimi, sura yangu haijifichi..na wewe ungelishaniambia , na nafahamu wewe unafahamu mwenzako katembea na nani , kweli si kweli...?' akaniuliza lakini kabla sijamjibu akasema

'Hivi wewe una uhakika kuwa mume wako hajawahi kutongoza wanawake wengine...hata kiutani tu, hayo yanatokea tu,...lakini baadaye unajirudi,... lakini hayo tuyaache maana ilikuwa zilipendwa, sasa niambie ukweli, unamfahamu aliyezaaa na rafiki yako, maana mimi naulizwa na wazazi wake...’akasema.

‘Mimi simfahamu....’nikasema .

‘Ok. Sio shida, nimewaambi ahivyo hivyo, lakini kuna mambo mengi wameniuliza, hasa kuhus urafiki wako na mwenzako…mmh, unajua mambo mengine unaweza ukayaficha, lakini wazee ni wepesi sana kuyagundua…’akasema.

‘Walisemaje…?’ nikauliza.

‘Hebu nikuulize kwanza, una uhakika kuwa kweli mume wako hakuwa ametokea huko kwa huyo rafiki yako?’ akaniuliza swali hilo na kunifanya nishtuke kidogo. Akilini nikajiwa na kumbukumbu, kuwa kuna muda niliona gari kama la mume wangu, pili, yule kijana wa kuosha magari, alisema ‘shemeji alikuwepo, huyu naye anasisitiza hilo hilo, na sijui anataka kuthibitisha nini…

‘Mimi nilikuwa huko kwa rafiki yangu...kama mume wangu angelikuwa huko si ningelimuona jamani…, labda alipita njia hiyo, sijui akitokea wapi, na sina uhakika na hilo, maana nijuavyo mimi alikuwa kwenye kikao…sasa alitokea wapi akapitia njia hiyo mimi sijui..’nikasema.

‘Kwahiyo mkiwa huko hukumuona mtu, aliyefika kwa rafiki yako, au….?’ Akauliza

‘Labda mdogo wake, nahisi hivyo tu…’nikasema

‘Mdogo wake!!!’ akasema kwa mshangao

‘Nahisi hivyo tu…sina uhakika…’nikasema

‘Kwanini unahisi hivyo…?’ nikaulizwa

‘Nimekuambia sina uhakika, tuliachie hapo tu, maana unanichimba sijui unatafuta nini…’nikasema hivyo maana nilijua hilo linaweza kuendelezwa mpaka nikasema yasiyotakiwa kusemwa.

‘Mbona mdogo wake, nilikuwa naye, alikuja kwangu kuna mambo fulani ya mkewe aliyafuatilia kwangu, ya kiafya..tukawa naye hapa tukiangalia mpira kwenye runinga,na niliachana naye muda mfupi, kabla sijapigiwa hiyo simu ya ajali....sizani kwamba aliweza kuja huko kwa muda huo mfupi,...’akasema

‘Mlikuwa naye nyumbani kwako…?’ nikauliza kwa mshangao

‘Ndio…sasa sizani, kam ni yeye, hata hivyo, yeye aliniomba gari langu kuwa anafuatilia mzigo wake, ndio maana nilishindwa kumchukua mume wako kwa haraka, kwani sikuwa na gari...ndio maana pia tukaamua kuagiza gari la wagonjwa....’akasema.

‘Ina maana gari lako mpaka sasa analo mdogo wa mume wangu?’ nikamuuliza.

‘Ndio maana yake, aliniazima gari langu , kwa vile gari la mumeo alikuwa nalo kikazi, au sio, na anasema alipiga simu kwa mumeo akawa hapatikani, ..haiwezekani akawa ndio yeye, labda yule mdogo wake mwingine, na yule hayupo hapa dar, alisafiri jana kama si kosei kwenda mikoani....’akasema.

‘Basi kama sio yeye, kuna mtu mwingine anafanana na ….huyo….’nikasema

‘Kwanini unasema hivyo…?’ akauliza

‘Hapana, tuyaache tu, sioni kama kuna lolote baya, nitamgudnua tu kuwa ni nani yangu, ninachotaka kusema, ni kuwa mimi nilihisi kuwa yeye alifika huko kwa rafiki yangu wakati mimi nipo huko, kama sio yeye.basi kuna mtu mwingine anayefafana naye....ni hivyo tu basi...’nikasema nikiwa sina uhakika.

‘Mhh..nisamehe tu..akilini mwangu nahisi kuna tatizo hapo,…’akasema

‘Tatizo gani…?’ nikauliza

‘Hebu niambie ukweli....unasema wakati upo huko, alifika mtu anayefanana na mdogo wa mume wako si ndio hivyo, nyie muda huo mlikuwa ndani, au nje…?’ akauliza

‘Tulikuwa ndani…’nikasema
 
SEHEMU YA 37


‘Kakupigia nani,…rafiki yangu…?’ nikamuuliza

Na docta akaikata ile simu, …haikuipokea ikanifanya niwe na mashaka, ni kwanini docta hakutaka kuipokea nikiwemo.

‘Ni kwanini unaikata hiyo simu…ni kwanini hutaki kuongea na yeye,labda anahitajia huduma yako ya kidakitari..?’nikauliza.

‘Hapana , tokea jana anataka kuongea na mimi, ..siwezi kuongea na yeye mpaka nimalizane na wewe…’akasema.

‘Sijakuelewa hapo,…kuna nini kinachoendelea kati yako na rafiki yangu, ..?’ nikamuuliza.

‘Kiukweli,…sijui…alinipigia simu, akasema nikipata muda, anataka tuongee mimi na yeye, nikamuuliza kuhusu nini, akasema ni maswali ambayo hataki kuyaongelea kwenye simu,…nikamuuliza je yanahusu mtoto, au yeye, akasema mtoto….nikamwambia mimi nipo likizo, akasema hahitaji kuongea kiofisi…’akasema

‘Unahisi anakuhitajia nini…?’nikamuuliza.

‘Yeye anafahamu wewe ni rafiki yangu, nahisi ..yale yale ninayotakakujua kutoka kwako, huenda anataka kuyafunika, kinamna.. au…..’akasema

‘Mimi siwezi kukuelewa kabisa, wewe una hisia zako mbaya dhidi ya rafiki yangu au hebu nikuulize kwanini unawazia hivyo…?’ akaniuliza

‘Kuwazia hivyo kuhusu nini…?’ akaniuliza

‘Kuwa huenda huyo mtu aliyekuja wakati nipo kwa rafiki yangu anaweza akawa ni mume wangu, kwanini, rafiki yako unamuhisi vibaya, kwanini lakini..?’ nikamuuliza

‘Kwanza tukubaliane, upo tayari tusaidiane kwa hili, la kumtafuta huyo mtu ni nani, au kumtafuta mwanaume aliyezaa na rafiki yako ni nani, na tuyafanye hayo kwa nia njema kabisa, sio kwa ubaya…?’ akaniuliza

‘Halafu ukishamfahamu,…?’ nikamuuliza

‘Tutakuwa tumemaliza tatizo, sasa itabakia kuona jinsi gani ya maisha yaendelee..nina imani wewe utakuwa huru,..hutahangaika tena, na mume wako atapona haraka….’akasema

*****************

‘Kwahiyo unatakaje hivi…?’ nikamuuliza

‘Ninachotaka mimi, ni wewe kuwa muwazi, uwe mkweli, ….’akasema

‘Kama hayo yatamsaidia mume wangu sawa, nitafurahi sana, lakini kunisaidia mimi, sijui unataka kunisaidia nini hapo, sijakuambia kuwa nina tatizo…?’ nikauliza

‘Nina imani yote yanaendana…kwanza tuanze hivi,..kwanini mume wako akawa mlevi hivyo wakati awali hakuwa hivyo, naomba unijibu kwa uwazi, ili tufike kunakotakiwa…?’ akaniuliza

‘Kiukweli, labda nijenge hisia tu…mume wangu kuna kipindi tulijadili kuwa tuzae, tupate watoto, na wazo lake kubwa ni kupata mtoto wa kiume, sijui kwanini analihitajia hilo sana…’nikasema

‘Ikawaje…mjadala huo uliishia wapi…au wewe ulisemaje..?’ akaniuliza

‘Nilimshauri kuwa hilo lisiwe kipaumbele chetu kwanza, kwasababu tupo kwenye harakati za kujiimarisha kiuchumi, lisubirie, akadai kuwa yeye anahitajia watoto mapema iwezekanavyo, ..hataki kuja kuzaa uzeeni…’nikasema

‘Huoni kuwa ana ukweli fulani hapo, kama wewe ulivyomshauri rafiki yako kuwa azae mapema, mbona wewe hukujiangalia au kuna tofauti kati yako na rafiki yako, unajiamini vipi hapo ..?’ akuliza

‘Tofauti yangu na rafiki yangu ni kuwa mimi nina mume na muda wowote nikihitajia kuzaa, kabla sijafikia ukomo, nitazaa kwa majaliwa ya mungu offcourse , lakini yeye mpaka ahangaike kumpata mwanaume na zaidi anayemtaka yeye, pili awe na uhakika wa ..…na huenda katika kulifanya hilo ikachukua muda, na jinsi gani ya maelewano a huyo mwanaume…’akasema

‘Kwahiyo ukamshauri akazae vipi hapo…?’ akauliza docta

‘Hilo la kuzaa vipi au na nani, nilimuachia yeye mwenyewe, sikutaka kumuingilia hayo…., si unajua alivyo, kwahiyo kama alizaa na nani, sio muhimu sana kwangu, kama hakuna tatizo…’nikasema.

‘Kama hakuna tatizo, nahisi sasa kuna tatizo….ok, ..Je hukuwahi kuongea kuwa azae na kundi gani, walio-oa, au wasio, oa…au azae baada ya kufunga ndoa..najua hilo la kufunga ndoa lilikuwa ni gumu kwake, au sio, kwa jinsi alivyojiwekea misimamo yake,…ya kuchagua chagua sana..sasa ulimshaurije hapo?’ akaniuliza, kiukweli sikutaka kumwambia ukweli wa hicho tulichokubaliana na rafiki yangu.

‘Nimeshakuambia hilo la kuzaa na nani, nilimuachia yeye mwenyewe, …’nikasema na kukaa kimia.

‘Una uhakika?…anyway, sasa hebu nikuulize, baada ya wazo hilo, ni kwanini asitafute wanaume ambao hawajaoa…?’ akaniuliza

‘Aaah, mbona maswali yako ya kujirudia rudia, jibu nimeshakupatia, na sijui alitafuta nani, sijui…’nikasema

‘Nasema hivyo nikiwa na maana. kiukweli mara nyingi huko nyumba alikuwa mbali sana na wanaume za watu, lakini ghafla nikaja kumuona akiwa karibu na wanaume wali-oa….au…mmm mlipanga iwe hivyo…?’akasema

‘Docta, mimi sina tabia ya kufuatilia maisha yake, kama wewe una muda huo, mimi sina muda huo kabisa, ..kwahiyo sikujua ni nani na nani alikuwa karibu naye…kama ni wewe au mwanaume mwingine yoyote…’nikasema

‘Au shemeji yake…’akasema docta na kunifanya nimtupie jicho

‘Shemeji yake..!!? Nani, mume wangu au…na wanini unamtaja yeye, nilishakuambia yeye ni shemeji yake, na hata wakiwa naye, hakuna shida, ..na na…au wewe unamshuku kuwa huenda ana mahusianio ya siri na mume wangu…mbona unantia mashaka ambayo sikuwa nayo kabisa..?’ nikamuuliza, nikimuangalia moja kwa moja usoni, na yeye akatabasamu na kusema;

‘Sijamshuku,… ila nataka kuwa na uhakika, ili tuweze kumsaidia mume wako…, nahisi mume wako ana tatizo kubwa, sasa ni tatizo gani, hilo mimi kama rafiki yake linanisumbua kichwa sana, ....’akasema.

Na hapo tukakaa kimiya kwa muda, mimi akilini nikawa nawazia hiyo kauli ya docta, kwanini ni kama anamshuku mume wangu, na nafahamu kuna muda mwingi baada ya kazi wanakuwa naye..japokuwa sio sana

Nilimuangalia docta, …huku nikiendelea kuwaza,..labda, inawezekana kukawa na lolote kati ya rafiki yangu na mume wangu, ..hapana hilo siwezi kabisa kuliamini, ...yule ni rafiki yangu mpenzi nimemuweka kwenye kundi la ndugu, siwezi hata siku moja kumfikiria vibaya, lakini huyu ni docta, na hana tabia mbaya, ni kwanini aliwazie hili, hapa nikaingiwa na mashaka....

‘Shemeji huenda utaniona, kuwa naingilia ndoa yenu, huenda ukahisi kwa vile nilikukosa wewe ndio maana najaribu kuona kila mlitendalo sio jema,..au kama unavyodai wewe…, kuwa wazazi wako wamenituma, kufanya lolote ili kuiharibu ndoa yenu, ..lakini kwanini tufanye hivyo..

‘Nikuulize wewe…’nikasema

‘Sio kweli, mimi nina nia njema kabisa na ndoa yenu, ndio maana nilikuomba sana mapema tu, nilipoona rafiki yangu anabadilika, anakunwya kupitiliza, nikakuomba sana ukae uongee naye, wewe ukapuuzia, mimi nahisi mume wako ana kitu kinamsumbua...’akasema

‘Mimi bado hapo sijakuelewa, tuongee nini hasa kuhusu starehe yake ya kulewa,..., mimi huko sina muda huo, kama kaona ni starehe yake muache endelee..au wewe unahisi kuna tatizo gani jingine...,mimi ninaanza kuingiwa na wasiwasi, kuna nini kutoka kwa rafiki yako ulichokiona kingine…, niambie, mimi si rafiki yako unaogopa nini sasa…’nikasema

‘Hapana, mimi sijui kitu,..ningekuwa na uhakika ningelikuambia mapema kabisa, ila ninachotaka mimi ni kujua ukweli…, nataka kuwa na uhakika, na uhakika huo nitaupata zaidi kutokwa kwako, na akili yangu inanituma, kuwa kuna kitu ambacho huenda kimesababishwa na mahusiano yenu wawili, wewe na mume wako, na kikaenda hadi kwa rafiki yako, sasa ni kitu gani hicho…’akasema

‘Una maana mimi nimemfanya mume wangu atembee nje ya ndoa, …labda kwa vile..si ndio hivyo…na aliyekwenda kutembea naye, au anayetembea naye ni rafiki yangu, kisa kwa vile umewaona wakiwa naye karibu, au sio, na matokeo yake ni huyo mtoto, au sio..niambie ukweli….’nikasema

‘Unaweza ukawa , haupo mbali na hisia zangu,…unanifahamu nilivyo, mimi ni docta, au sio, siwezi kutibu ugonjwa bila kujua vipimo, ndio maana natadadavua kuupta huo ukweli, na wewe hutaki kutoa ushirikiano…’akasema

‘Kwahiyo…unataka kunipima nini…niambie…’nikasema

‘Ukweli…nataka ukweli kutoka kwako…’akasema

‘Hebu niambie kuna nini kinachoendelea kati yako wewe na rafiki yako, naanza kuhisi vibaya, kuwa huenda kuna jambo kalifanya, au kuna jambo unalifahamu dhidi ya rafiki yako, labda mlishirikiana wewe na yeye, sasa wewe unatafuta namna ya kujikosha kwangu, ili usionekane kuwa na wewe unahusika, sasa ...niambie rafiki yako kafanya nini?’ nikamuuliza kwa ukali.

‘Shemeji siwezi kujua zaidi , ...yule ni rafiki yangu, lakini tuna mipaka yetu, sio rafiki wa kujua kila kitu, kuna yake anayafanya mimi siwezi kuyafahamu,..lakini naomba unielewe , mimi nilichokiona ni hiyo tabia yake ya kunywa kupita kiasi, ilianza tu…nikamuuliza akasema kaamua tu, na unielewe sio kila siku ni kitoka jioni ninakuwa naye, hapana. Hebu nikuulize je hajawahi kulala nje...?’
 
SEHEMU YA 38

‘Kulala nje!!!..., hapana, hawezi kulala nje, kwanini alale nje, wakati ana nyumbani yake, labda kuwe na sherehe ya kukesha huko kazini kwao, hilo linatokea…, na hilo kwa siku hizi halijawahi kutokea, ...kuchelewa hilo nalikubaliana au kurudi akiwa kalewa sana huwa inatokea, na yah, …kuna siku alichelewa sana mpaka nikawa na mashaka, kama mara mbili tatu hivi…karudi alifajiri....lakini yeye ni mtu mzima, ulitaka hapo nifanye nini mimi, nijiumize kichwa na starehe za mtu, kaamua, tumuache, dunia itamfunza...’nikasema.

‘Na akiwa kalewa sana ni nani anamleta nyumbani kama mimi sipo naye…, maana akilewa sana nikiwa naye, huwa mimi namleta mwenyewe, je kama sipo, ni nani mwingine anapenda kumleta nyumbani, maana hapo huwezi kunificha kuwa halewi kiasi cha kutokujitambua?’ akaniuliza.

‘Wewe unafahamu bwana, kuwa mara nyingi ni mdogo wake anayemleta, huwa akiona kalewa kupitiliza kiasi cha kutokujitambua, sijui kwanini mtu mzina kama huyo anafanya hivyo…mimi nijuavyo kama haupo, anamuita mdogo wake, na mdogo wake, anafika hapo alipo anamchukua...’nikasema.

‘Kwahiyo …eeh, mdogo wake atakuwa anafahamu mengi kuhusu kaka yake ambayo mimi siyafahamu, …sawa hapo eeh,.. umenipa wazo, jinsi ya kulifuatilia hili jambo, huyo ni mtu mwingine anaweza kutusaidia, umeliona hilo hata wewe.....?’ akawa kama ananiuliza

‘Mmhh,…kuliona …!!Lakini nikuulize kwanza, ni kwanini unamshuku rafiki yako, kaua, kafanya jambo gani baya sana, maana unavyouliza ni kama vile kuna kesi ya mauaji,..., au hahaha, kufamaniwa, …hapana huyo sio mume wangu, …ka-kafanya nini kikubwa hivyo, mbona hutaki kuniweka wazi?’ nikamuuliza.

‘Sijasema kuwa kafanya lolote baya, hilo uliweke akilini, ninachotaka kukifanya hapa ni kutafuta kama kuna tatizo, ta-ti-zo ...je huko kuendesha gari kwake kwa kasi huoni kuwa kuna kitu kilitokea akawa anakimbia, au kuna jambo alikuwa akilifuatilia nyumbani kwa haraka, huenda alikuwa anakuja kuku....’akakatisha

‘Unataka kusema alikuwa anakuja kutaka kunifumania au....acha hayo mawazo hayo docta, wewe ni msomi bwana…na familia yangu ni ya watu wastaarabu, hakuna mwenye tabia chafu kama hiyo...kama unayo wewe usifikirie kila mtu ana tabia kama hiyo.’nikasema kwa hasira.

‘Hahaha…lakini, unanifahamu sana, nilivyo, lakini vyovyote iwavyo, sote sisi ni wanadamu inaweza kutokea mtu akateleza, jua ibilisi mkubwa wa mwanadamu ni mwanadamu .., huwezi jua,...hata wewe unaweza kughilibiwa ukajikuta umefanya jambo ambalo baadaye linakuja kukuleta matatizo, ukawa unatafuta njia ya kujisafisha, lakini wenzako wameshaliona na huenda wamekuweka kati, dunia hii ina watu wabaya.....’akasema

‘Mpaka sasa sijakuelewa msingi wa maswali yako...unachokitafuta hasa ni nini, kuwa mimi nina matatizo au mwenzangu ana matatizo?’ nikamuuliza.

‘Sijawa na uhakika na hilo ndio maana nakuuliza ...maana kama wewe ungeliweka wazi, kuwa kuna tatizo, kwako au kwa mwenzako, ningejua jinsi gani ya kufanya, na nini nifanye ili niweze kusaidia, lakini naona nyote mnanificha, ndio maana najaribu kuwa mpelelezi, kwa nia njema kabisa ....’akasema.

‘Yatakushinda....siku hizi umeacha kazi yako ya udakitari unaanza kufuatilia ndoa za watu, haya na ili upate faida gani...’nikasema na yeye akaangalia saa yake, halafu akasema;

‘Kuna watu wawili wanaweza kutusaidia kwa hil tatizo , ...ili kugundua kuwa huenda mwenzetu ana tatizo gani, hadi sasa kwa uoni wangu nimeona kuwa kuna tatizo, sasa ni tatizo gani, ni muhimu sana tusaidiane kulitafuta haraka iwezekanavyo kabla hali haijawa mbaya zaidi, ...’akasema.

‘Umeona kuwa kuna tatizo, umeona kuna tatizo gani,..kuwa huenda ajali hiyo ilikuwa na msukumo fulani, si ndio maana yake hiyo, au..?’nikasema kwa upole, kwani hapo niliona kuna hoja ya msingi.

‘Ndio ...hebu angalai hili bila kujali kuwa mimi ndiye nalifuatilia, angalia kwa nia ya kumsaidia mwenzako, na hatimaye kuisaidia ndoa yako, na urafiki wenu na huyo rafiki yako, huenda tatizo limeanzia kwako bila kufahamu ...’akasema.

‘Nani na nani wanaweza kutusaidia sasa, maana hili naona umelivalia njuga, na ukianzisha jambo lako mpaka upate majibu, haya ili tuyamalize haya, ni nani anaweza kutusaidia, nataka uwe huru, kuwa unavyohisi sio kweli, ni nani atatusaidia....?’ nikauliza na yeye akasogea karibu yangu, na kusema kwa upole.

‘Wa kwanza ni mdogo wa mume wako, ....japokuwa kwenye ajali hiyo hakuwepo , lakini nahisi anafahamu mengi kuhusu mienendo ya kaka yake....huyo naweza kuongea naye mimi, naona uniachie mimi huyo mtu,..nitambana mpaka atanieleza...’akasema

‘Sawa nakuachia wewe hilo…na mwingine au huyo anatosha…?’ nikamuuliza, hapo nilianza kuingiwa na mawazo , nikijiulia kweli ni kwanini mume wangu aliendesha gari kwa mwendo huo, na ni kinyume na tabia yake, ...basi kulikuwa na jambo, lakini mbona hata mimi niliendesha kwa mwendo kasi,nilipopewa ujumbe huo kuja nyumbani haraka,kumbe inawezekana ikatokea hivyo ..

‘Kama ni kujua kwanini alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi, mimi naona hakuna cha muhimu hapo, mbona hata mimi , leo nilijikuta nikiendesha kwa mwendo kasi uliponipigia simu kuwa nije nyumbani kwa haraka, kwasababu kuna tatizo huku nyumbani...na sikujua kabisa kuwa nilikuwa naendesha kwa mwendo kasi.....’nikasema.

‘Unaonaeeh,wewe ulifanya hivyo kuja nyumbani kwasababu hiyo ya msingi, je mume alifanya hivyo kwasababu gani ya msingi.., nikuulize swali ili uone kuwa kuna tatizo, je mume wako ana tabia ya kuendesha gari kwa fujo, hapana au sio namafahamu sana?’ akaniuliza.

‘Hana kabisa tabia hiyo, ndio maana nashindwa kuelewa,.....’nikasema.

‘Unaonaeeh, sasa tunaanza kuwa pamoja..?’ akawa kama ananiuliza.

‘Ninaona nini hapo, kuwa pamoja kwa vipi, mimi nataka nifane unavyotaka wewe, sawa, hisia zipo, na kiukweli sio kwamba sina hisia kama zako, lakini nazipotezea, maana hao ni watu nawaamini, sasa kama kuna walakini, haya ngoja tuutafute, sawa?’ nikamuuliza.

‘Ndio maana yake mimi nina imani kuwa mume wako alikuwa akikimbia tatizo,....maana kama wewe huna tabia anayoihisi mume wako,...na alifahamu kuwa haupo nyumbani, basi huenda alikuwa akikimbia jambo, sasa alikuwa akikimbia jambo gani, au alikuwa akifuatilia jambo gani, ataulizwa hilo na watu wengi wakiwemo watu wa usalama, bima nk......’akasema, na mimi hapo nikatulia kidogo nikiwaza.

‘Yawezekana ndio,…ndio maana hata hakutaka kwenda hospitalini...’nikasema.

‘Kwahiyo huyo mmoja, anatosha kutusaidia….?’ nikauliza

‘Mtu wa pili ambaye anaweza kutusaidia ni rafiki yako, ....’akasema.

‘Kwani vipi shemeji ....rafiki yangu anahusikanaje na mambo yangu ya kifamilia..au ajali ya mume wangu, hapo ….ok, ok, ….lakini kama na yeye ni muhusika, atanisaidiaje,, hebu niambie hapo,?’ nikamuuliza .

‘Akusaidie kujua kama anafahamu lolote, kuhusiana na mume wako, kama kuna tatizo linalomsumbua, maana inawezekana mume wako yupo kwenye mtego wa watu wanaomtishia amani, labda kama asipofanya hivi au vile anaweza akaingizwa kwenye matatizo, ....nasema tu, kama mfano, ....'akasema

'Mhh, huko umekwenda mbali, rafiki yangu amrubuni mume wangu, na amwambie kuwa asipofanya hivyo, atafanya vile..kwanini..hapana, kwa maana hilo alilofanya rafiki yangu, tulishauriana mimi na yeye, sasa kwanini ...'nikasema

'Mlishauriana, ndio, lakini umesema, hkumshauri amtafute mume gani, au sio..je kama alimtafuta mume wako,...?' akaniuliza na kunifanya nishtuke

'Acha hayo maneno kabisa, usinichafue...hivi nikuulize kuna mtu anaweza kutembea na shemeji yake mwenye akili timamu, unazungumzia hapo rafiki yangu, unamfahamu kabisa alivyo, hapendii kabisa kutembea na wanaume za watu, ...usimzushie rafiki yangu uwongo....'nikasema

'Kuna kitu nataka tukihakiki...je wewe unaweza kufanya hivyo, kuongea na rafiki yako, au, nina wazo, hebu fanya hivi, unaweza ukamuita rafiki yako , akaja hapa hospitalini, na ikiwezekana aje na mtoto wake, anaweza kuja, au sio..?’ akaniuliza.

‘Aje na mtoto, ...mhh, kwanini lakini, yupe bado ni mzazi, kwanini tumsumbue, atoke ahuko na mtoto kwanini lakini...na huyo mtoto wake unamuhitajia nini...hahaha nimeshakuelewa, unataka kufanya nini...hapana siwezo...’ akasema.

'Sikiliza...ni muhimu sana...fanya hivyo, kuna kitu nimekiona , fanya hivyo, muite rafiki yako aje hapa hospitalini,..na mtoto, ....unaweza kufanya hivyo...?' akasema

'Mhh.....' nikaishia kuguna, na sikuelewa kabisa docta anataka nini, lakini, ....

NB: Docta anataka nini hapa, …mtoto…mtoto wa nini…?

WAZO LA LEO: Urafiki wa kweli ni wa kujaliana, mwenzako akipatwa na tatizo, iwe ni kama wewe umepetwa na tatizo hilo. Ni faraja sana ukiwa na tatizo rafiki yako akawa anatafuta njia ya kukusaidia.
 
SEHEMU YA 39


‘Ningefurahi nimuone, tukiwa pamoja sote.....kuna mambo nashindwa kukuambia, maana nikikuambia kwa hivi sasa utaona kama nakudanganya, najaribu kuwaza kuhusu baba wa huyo mtoto, kabla ukweli haujabainika...’akasema.
‘Mimi sijakuelewa hapo, lengo lako hapo ni nini, ni kutaka kujua baba wa huyo mtoto au unahisi labda huyo mtoto ni wa kwako kwa vile uliwahi kutembea naye nini..nikuambie ukweli, sio wa kwako, kwasababu hafanani na wewe kabisa, umenielewa…?’ nikamwambia
‘Anafanana na nani…?’ akauliza akiniangalia kwa uso wa udadisi
‘Anafanana na mama yake....’nikamdanganya, na yeye akacheka kicheko cha dharau
‘Kweli..umemuangalia vyema..una uhakika kuwa anafanana na mama yake..?’ akaniuliza akitikisa kichwa kwa mashaka
‘Nina uhakika kwa vile mimi nimemuona, …kwahiyo kama nia yako ni hiyo basi zoezi lako liishie hapa, na kwanini unatia shaka na jibu langu?’ nikamuuliza.
‘Ok….mimi huko sipo kabisa, hayo unabuni wewe, siwazii lolote kuwa huyo mtoto ni wangu maana sio kweli kuwa niliwahi kutembea naye,.na kufanana na mtu fulani wakati huu, sio tija, maana watoto wachanga wengi hufanana, subiria akue kue, utajua anafanana na nani...’akasema na mimi nikatabasamu
‘Kwanini umetabasamu,.....?’ akaniuliza.
‘Kwa vile jibu lako limenipa faraja, na kuniondoa wasiwasi niliokuwa nao...nahisi itakuwa hivyo...’nikasema bila kusema zaidi
‘Sasa fanya hivyo basi usipoteze muda, mpigia rafiki yako uone utakavyofanya ili aje hapa..nina imani akifika hapa, tutagundua meng nyuma ya pazia, niamini mimi
‘Ok, hilo hakuna shida maana rafiki yangu ninamuamini sana, kama nilivyokuambia kuwa ni zaidi ya rafiki, ni ndugu yangu..., kama ni kulifanyia kazi hilo, kwa kupitia kwake, basi hakuna shaka, nitamuita aje na mtotoni sitaki kashifa kwenye familia yangu,...’nikasema.
‘Sijasema hilo...na sioni kwamba kuna kashifa hapo, usijali, na wala usiwe na wasiwasi....’akasema.
Nilitulia kidogo nikiwazia hilo wazo la huyo docta, kwa namna moja nilikuwa nimeliunga mkono, huenda kweli mume wangu yupo kwenye matatizo, makubwa, lakini hataki kunihusisha, ila siungu mkono ya kuwa mume wangu huenda ana mahusiano na wanawake wa nje, hususani kutembea na rafiki yangu
‘Kweli atakayeweza kunisaidia kwa hili na kuondoa hii taswira iliyoanza kujengwa nafsini mwangu ni rafiki yangu, na docta atabakia mdomo wazi, ngoja nimuite.
Nikampigia simu rafiki yangu huyo, kwa muda huo alikuwa kakaa nyumbani kwake anaangalia runinga, na aliposikua kuwa ni mimi akawa na hamasa sana ya kuongea na mimi…
‘Nakuomba uje hapa hospitalini, alipolazwa shemeji yako, mara moja…’nikasema
‘Kuna nini..!!! Ina maana..she-she-, shemeji anaendeleaje kwani..?’ akuliza akionekana kuchanganyikiwa kwenye simu
‘Tafadhali nakuomba uje tu,…’nikasema
‘Sasa na…oh, na mtoto itakuwaje…?’ akauliza
‘Njoo naye, usimuache, tafadhali…’nikasema na kukata simu.
Nilijua atafika tu, maana mimi nimekuwa nikimtumia sana kwenye shughuli zangu nje ya kazi yake, ili kumsaidia kuongeza kipato, na anafahamu nikimpigia simu ya namna hiyo, basi ni jambo la haraka, na anaitikia alifanyie kazi mara moja.
‘Una uhakika atakuja…?’ akaniuliza docta
‘Atakuja…ila naona kama nimempa hali ngumu,…asije akapatwa na mengine…’nikasema
‘Hamna shida, rafiki yako huyo ni shupavu, namuaminia sana, mtu anaweza kupigana ngumi na wanaume, sio mchezo…’akasema na kucheka kwa mdhaha…
‘Lakini sio kwa mambo kama haya, yanashtua sana, sio vitu vya kuchezea, au kumjaribu mtu..hapana, utani mwingine uufanye lakini sio kwa afya, kifo, na…hapana, hayo, hayana uvumilivu…’nikasema
‘Ni kweli, hata sisi madocta tunalifahamu hilo, ndio maana hata mimi najaribu kuliweka hili jambo, liwe rahisi kwenu..najua tutalimaliza salama, na rafiki yangu atapona kwa haraka, tushirikiane tu…’akasema na mimi nikamtupia jicho la kujiuliza
‘Unajua kiukweli, umenifanya nafsi yangu ianze kufikiria mambo ambayo sikutaka kabisa kuyafikiria,..nimekuwa nikiyapiga vita sana…lakini kila hatua unanifanya nianze kuwaza mengine..mungu anisamehe tu…’nikasema
‘Usijali, kama yametokea yametokea, kama hayapo basi, tutayamaliza kwa amani, ila mimi ninachotaka ni kuhakikisha, kuwa hakuna cha kulaumiana..hakuna cha kumuongezea mgonjwa mawazo, na yote ni sisi watu wake wa karibu..tufanye jambo, nakuomba ten asana ulifahamu hilo…’akasema
‘Mbona wanachelewa hivyo…?’ nikauliza, nikikwepa maongezi yake, maana muda huo akili yangu ilikuwa kwingine kabisa, namuwazia mume wangu, nahisi kama kuna kitu hakipo sawa, miguu inaanza kuniisha nguvu..
‘Ngoja nikaangalie nahisi watakuwa tayari, labda kuna kitu wanakisubiria…’akasema docta na kuondoka kuelekea huko. Na mimi pale nilitaka nimfuate nyuma,lakini sheria ikanikwaza.
*************
Baadae docta akarudi…hakuonyesha furaha usoni, japokuwa alikuwa akijaribu kujificha kinamna kwa tabasamu la uwongo na kweli, na hali hiyo ikanizidisha mashaka, nikamuuliza kwa haraka haraka…
‘Vipi huko ulipokwenda wanasemaje, mume wangu anaendeleaje, maana ungechelewa kidogo tu na mimi ningelikuja huko huko..?’ nikamuuliza
‘Hali yake inendelea vyema usiwe na shaka, …wamemchunguza na kuona kila kitu kipo sawa…’akasema
‘Sikuamini docta, kwanini…na mimi niende nikamuona tu jamani…’nikasema huku nikishika kichwa.
‘Shemuuuh, …huaniamini…anaendelea vizuri, hali ya jana sio ya leo, leo anatizamika, ika kwa vile alikuwa kwenye uchunguzi, lazima hali kama hiyo itakuwepo, kuinuliwa, hivi na vile…wamechunguza wamesema hakuna sehemu iliyovunjika…’akatulia kidogo.
‘Na mashaka yao walioyokuwa nayo awali yameondoka, kwani walihisi huenda kuna athari za ndani kwa ndani..kiukweli hakuna athari yoyote iliyojificha ya ndani kwa ndani, ila bado wanaendelea kumfanyia uchunguzi zaidi , kwani bado alikuwa analalamika maumivu, lakini ni kwasababu ya kashikashi hizo, yatakwisha, ndio maana nataka wewe na rafiki yako, tuje tuongee vyema, kwa hili mtaniona mbaya….’akasema
‘Kwahiyo uliweza kuongea naye…?’ nikamuuliza bila kujali kauli yake hiyo.
‘Bado hawajaruhusu kuongea na mtu, niliongea na docta wake tu, wakati wanamrejesha wodini, na kweli nilimsikia akilalamika maumivu, hasa ya mgongo na kiuno,...inawezekana ni kutokana na hali halisi, kama nilivyosema… na kule kulala muda..unajua mwili ulivyo…, lakini yupo vizuri, yupo… yupo vizuri...’akasema
‘Unasema kutokana na hali halisi kwa vipi….?’ Nikamuuliza nikimkazia macho.
‘Kwa vile ajali hiyo imegusa uti wa mgongo, kwahiyo kuna maumivi sehemu kubwa ya mwili, kwa hivi sasa bado wanaendelea naye , tuwape muda wafanye kazi yao, ili kuhakikisha kila kitu kipo sawa, usijali mambo yatakuwa sawa...’akasema huyo rafiki wa mume wangu.
‘Lakini, niambie ukweli, wewe kama docta unahisi vipi, huko kulalamika mgongo na kiuono, inawezekana ni jambo la muda, litakiwisha ni kweli hakutakuwa na athari zingine zinaweza kujitokeza huko baadae?’ nikamuuliza.
‘Mhh, hakuna,..maana vipimo vinasema, ila ngoja tusubirie wamalize kazi yao, nitaongea nao, nitakagua ripoti zao, lakini yale muhimu yanayotuhitajia sisi, tuyafanye, tuhakikishe tunakwepa yale yote yanayoweza kumkwaza, maana kama kuna athari zitakuja kujitokeza zitakuwa ni za kibinadamuu, mimi sina wasiwasi na hilo....’akasema.
‘Kwahiyo sasa hivi yupo macho , nikienda naweza kuongea naye…?’ nikauliza
‘Ndio yupo macho, kazindukana, lakini bado madocta wanamfanyia uchunguzi wa hapa na pale, naona wamekutana wote, kuhakikisha kuwa hawafanyi makosa, na hilo la kulalamika, nina uhakika na kutokana na hiyo mitikisiko ya kumuinua, inua, itakwisha tu, ....’akasema.
‘Mhh, hapo mimi bado nina mashaka, mpaka nionane naye…na kama wameshindwa wasema tumpeleke juu zaidi, au...?’nikasema.
‘Hawajashindwa bwana, …nakuhakikishia hilo, huniamini mimi shemeji,…ila mimi nilikuwa nakushauri kitu,naona wewe una shughuli nyingi umeziacha bila ya maagizo,kwa vile mimi nipo likizo, ninaweza kubakia hapa, ili niendelee kuona hali ya mgonjwa kwa ukaribu zaidi na kama kuna lolote la kusaidia, nisaidie, unaonaje,…’akasema
‘Kuondoka…haaah weeeh!!! Hapana, kwanza umesahau ulichoniagiza au…?’ nikauliza
‘Oooh…hilo achana nalo,muhimu ni wewe na shughuli zako, najua hilo tutalifanyia kazi, maana lina umuhimu wake, hasa kwa mgonjwa, …. Mgonjwa pamoja na matibabu, lakini kuna mazingira akiyaona, akisikia kauli zenu, anaweza akatatizika, hili muwe makini sana …’akasema
‘Sasa ndio unanishauri niende nyumbani, akiona sipo, huoni atajisikia vibaya…?’nikauliza
‘Hapana, kwa vile mimi nipo najua jinsi gani ya kuongea naye…hilo lisikutie shaka, maana tunaweza kuacha mgonjwa, kwa ajili ya mgonjwa mwingine…’akasema
Mimi sikukualiana na wazo lake hilo, la mimi kwenda nyumbani bila kumuona mume wangu, nikawa nimekaa kimia, akilini nikimuwazia mume wangu, ina maana kitu kidogo tu kinaweza kumfikisha mwanadamu hapo, ooh, sijui ni kosa langu au kuna tatizo, jingine kama ni kosa langu sijui nitajijutiaje, ......hapo nikahisi machozi yakinilenga lenga.
Nikainua kichwa kumuangalia docta, nikamuona akinichunguza kwa macho, na muda huo machozi yanakuja kwa kasi,… kabla sijaathirika na hiyo hali, nikageuka upande mwingine, docta akaitambua hiyo hali na kusema;
‘Usiwe na shaka, ...nakuhakikishia kuwa mume wako hana matatizo, ...ni swala la muda tu, utakuwa naye, ajali ni ajali, na hiyo ajali yake ilikuwa ni kubwa sana, hutegemei mtu aliyetoka pale awe hai, uhai wake bado mkubwa sana, hata yeye sizani kama ataamini kuwa aliweza kutoka hapo salama....’akasema na mimi sikusema.
Na ni wakati nainua kichwa kuangalia sehemu ya nje, kwenye mlango mkubwa ndio nikamuona rafiki yangu akija kwa mbali, na wakati huo huo docta akawa anaongea na simu yake. Na alipomaliza kuongea na simu, akanigeukia na kusema;
‘Ni vyema kwa leo, hata kama tutaruhusiwa kumuona mgonjwa, wewe hakikisha huruhusu watu wengi kuonana na mume wako, hata kama ni rafiki yako, mimi mwenyewe nitalisimamia hilo ...’akasema
‘Kwanini,…si umesema yupo sawa, ..ok, tutawasikiliza madocta watakavyosema au sio,. Kuonana na watu kwa wengine ni faraja au…’nikasema
‘Hata mimi ni docta, au huniamini, kwa vile kuna mambo nimeshayaona, nisingelipenda akaja mtu akamzidishia mawazo, hasa nyie wawili,…’akasema
‘Ndio maana maana ya kumuita rafiki yangu au..sasa na mtoto ni wa nini,…?’ nikamuuliza, na je rafiki yangu akija hapa, hatamuona mgonjwa,…?’ nikamuuliza
‘Yeye kumuita hapa, awali nilitaka iwe hivyo, tumuone mgonjwa pamoja, nyie ni marafiki au sio, lakini kuna kitu nilitaka kiwe wazi,…lakini baada ya kumuona tena mgonjwa alivyo, naona hata akija rafiki yako, tutaongea naye tu,.’akasema
‘Haitakuwa vyema, tutamuambia asifanye lolote …amuone tu…’nikasema
‘Mhh….kiukweli hivi sasa mume wako hahitaji mshutuko wowote, hahitaji, kitu cha kumpa mawazo, ni bora akutane na wewe tu na mdocta mpaka hapo hali itakapo kuwa sawa…’akasema
‘Sawa , hilo halina shida, kama umesema hivyo, hakuna shida,..nitafanya hivyo hivyo, ila tutakuwa tumemsumbua rafiki yangu aje tu, bila kumuona mgonjwa, sio vizuri, lakini sawa, nimekuelewa…’nikasema
‘Ok, sasa unaonaje wazo langu, la wewe kurudi nyumbani kidogo, umalizane na mambo ya kazi, halafu utarudi, ikibidi,..nahisi huyo rafiki yako hatafika....na kwa vile ni mzazi, tumuache tu, tutakuja kuongea naye hata nyumbani.....’akasema , alikuwa hajamuona huyo rafiki yangu maana sasa alikuwa anakuja muelekeo wetu lakini docta alikuwa kampa mgongo.
‘Anakuja..nashukuru kaja,…hata hivyo, mimi ninachotaka nikaonane na mume wangu kwanza,…au…hapa sina amani kabisa, …’nikasema.
‘Mumeo anaendelea vyema, usiwe na wasiwasi, tutakwenda kumuona lakini tukishamalizana huku, najua mengine, au mpigie rafiki yako asije tutaongea naye huko huko…’akasema hivyo.
‘Kaja…ili tuweze kuyamaliza haya mambo, ili na wewe uweze kuondoa hofu yako dhidi yake ..’ nikasema na huyo rafiki yangu akawa sasa keshafika, kasimama nyuma ya docta.
‘Sawa kama una uhakika …kuwa atafika, sawa, nina mambo yatakuwa sawa, mimi nilikuwa nimekitaka ni kumbana rafiki yako, aseme ukweli, …lakini kwa vile kuna hii hali ya sasa, …haina haja ya kulazimishana…ila nyie kama binadamu ningeliwaomba muwe wawazi, ili na mimi niweze kutoa ushauri unaofaa, kama mtakwua mnanificha ficha mambo, inaniwia vigumu, haya ngoja aje tuone atatusaidiaje, nina uhakika….’kabla hajamaliza rafiki yangu akakohoa na kusema;
‘Sam-samahanini kuwakatili kwenye mazungumzo yenu, maana mtoto nimemuacha nje, Haya nipeni habari za mgonjwa, .maana umenifanya nitoke wangu wangu hata bila ya kubadili nguo, niambie kuna usalama huku...’akasema kweli akionyesha mashaka.
‘Oh….’docta akashtuka, akisikia rafiki yangu akiongea nyuma yake, akaguna hivyo, halafu kwa haraka akasema;
‘Wewe umemuacha mtoto nje ndani ya gari, na nani?’ akauliza docta kwa mshangao.
‘Kuna mtu yupo naye, usitie shaka, hahaha, naona ulivyoniangalia, ulifikiri nimemuacha ndani ya gari peke yake, hapana,…weeh, hapa kwenye natamani nirudi, siamini mtu kabisa...’akasema huku akiniangalia mimi machoni.
‘Karibu…’nikasema
‘Haya niambieni hali ya shemeji ipoje..nakuona kama unalia...kuna usalama kweli…?’akasema rafiki yangu huyo akiniangalia usoni kwa mashaka, na mimi nikapitisha leso machoni.
 
SEHEMU YA 40
****************
‘Kuhusu mume wangu,...mhh, bado,...sijaonana naye tangu wamchue , wanasema wanataka kumchunguza zaidi leo, uchunguzi wa kawaida, …. lakini kwa taarifa za kupitia huyu rafiki yake,…docta…. wanasema hajavunjika mahali,....ila analalamika maumivu kwenye kiuno...na mgongo, na hilo kwangu mimi naona ni hatari au...’nikamwambia huyo rafiki yangu.
‘Kwenye kiuno..na mgongo mhh, au huko kulala lala namna moja bila kujigeuza kwa muda, lakini vipimo vitasema au sio docta,.. mimi sioni kwanini uwe na wasiwasi....kwani majeraha ya hiyo ajali yamegusa mgongo, kichwa, au…?’ akasema huyo rafiki yangu
Docta aliposkia hivyo alimuangalia huyo rafiki yangu kwa makini…na baadae akasema;
‘Hajapata athari kubwa sehemu hizo, kiukweli hali yako haipo mbaya kihivyo, uchunguzi wa leo ni wa kujirizisha tu,.... tumpe muda, tuwape muda madocta wafanye kazi zao au sio.....’akasema huyo docta akimwangali huyo rafiki yangu, na huyo rafiki yangu akawa kama hataki kuongaliana na docta, akawa ananiangalia mimi na kusema;
‘Kwahiyo eeh,…. Ulivyoniita kwa haraka hivyo…nahisi kuna jambo la dharura,…unajua mimi nilipanga kuja kumuona lakini ulivyoniita nikajua kuna tatizo jingine kubwa, ooh, umenishtua kweli, ..sasa eeh, hiyo ajali ilitokeaje?’ akaniuliza
‘Hata mimi sijajua vyema , mambo yamekuwa ya harakaharaka sana, ila watu nilio-onana nao wanadai kuwa eti mume wangu alikuwa kwenye mwendo kasi, ...ndio ikatokea hiyo ajali, gari likawaka moto...’ nikasema.
‘My, my ….mbona mkosi huu…mhh, unajua najiuliza mbona shemeji hana tabia hiyo ya kuendeshe gari kwa mwendo kasi, ilikuwaje lakini, nahisi …oh,…au.., alikuwa anakimbia nini, kuwahi kitu gani, ....aliogopa nini…mmh hapo kuna tatizo....’akasita kidogo na kugeuka kumwangalia huyo docta, na haraka akaniangalia mimi na kusema;
‘Na hiyo ajali ilitokea wakati anatokea aah....wapi?.’akasita kidogo na kumalizia hiyo `wapi’ kwa kusita, na kugeuka kumwangalia docta inaonekana hakuwa na amani kuwepo huyo docta. Na huyo docta akawa anajifanya hatuangalii sisi
‘Sina uhakika sana....maana kama ninavyokuambia mambo yametokea kwa haraka sana,..sijapata muda wa kulifuatilia hilo,...sina uhakika sana alikuwa katokea wapi...’nikasema na doca akasema.
‘Atakuwa alitokea maeneo ya huko kwenu, na sio kazini, kama angelitokea kazini angekuwa upande mwingine wa barabara...ukiangalia lile gari lilivyokuwa ...’akasema docta, na huyo rafiki yangu akasema.
‘Yaah, itakuwa hivyo.........’akasema na huyo docta akamkatiza.
‘Kwani uliwahi kuonana naye kabla ya hiyo ajali...?’ akauliza na mimi nikainua kichwa kumwangalai rafiki yangu ambaye alikuwa katulia na nilipoona hajibu kitu, mimi nikasema;
‘Kama alitokea huko kwako, mimi …si tungeliliona hilo gari likipita maana pale ndani tukiwa tumekaa tunaona bara barani, eti, wewe uliliona gari la mume wangu likipita , yawezekana labda, alitaka kuja kumuona mzazi, sasa kwanini akapita..na kuna muda nilimpigia simu akasema yupo kazini, sasa hapo mimi naona ..lakini tuyaache tu, nitakuja kuyafahamu yote hayo..’nikasema.
‘Alikuambia anakuja kumuona mzazi sio ...?’ akauliza docta
‘Ndio anakwenda, kumuona mzazi ….’nikasema
‘Mzazi gani huyo…?’ akauliza
‘Nakumbuka …unajua hata wakati mzazi huyo yupo hospitali alikwenda kumuona na nahisi ndio huyo alikuwa anakwenda kumuona nyumbani kwake…’nikasema
‘Ni nani huyo…sizani kama kuna mzazi mwingine zaidi ya huyu rafiki yako, ,…na nakumbuka mimi niliwahi kuongea naye, akaniambia rafiki wa mke wake kajifungua, sasa sizani kama kuna mzazi mwingine, hajaniambia …au …?’ akauliza akimuangalia rafiki yangu.
‘Yupo mwingine bwana….nahisi anaweza akawa mke wa mfanyakazi mwenzao, au ..mfanyakazi mwenzao, …sina uhakika, maana sikupata muda wa kumuulizia zaidi….’nikasema
‘Mhh…labda….’rafiki yangu akaguna na kusema hivyo..
‘Sio labda, ni kweli…’nikasema
‘Sizani…ehe, hebu rafiki yako atusaidie hapo…’akasema docta na kabla hajamaliza rafiki yangu akadakia kwa kusema;
‘Unajua nimekumbuka, kuna watu walikuwa wakiongea, kuhusu ajali iliyotokea kwenye kona ya barabara ya kuingia barabara inayotokea bara bara kuu, wanasema ni ajali mbaya, na hakuna mtu aliyepona, ina maana ndio hiyo…?’akasema rafiki yangu na kuuliza.
‘Itakuwa ndio hiyo…’akasema docta
‘Kwakweli hapa nilipo nashindwa hata cha kuongea, maana sielewi, ni kitu gani kilimfanya aendeshe gari kwa mwendo kasi, ...sijui alikuwa kalewa, au alikutwa na janga gani, maana siku hizi kama unavyojua, mume wangu kabadilika, amekuwa mlevi...’nikasema.
‘Nahisi ana tatizo, nilikuulizia hilo ..lakini sasa,…tuseme ajali haina kinga…sasa eeh.. hebu niambieni kinachoendelea maana kama nilivyowaambia mtoto yupo kwenye gari, sitaki kukaa sana, ninaweza kwenda kumuona mgonjwa mara moja, ....?’ akauliza rafiki yangu.
‘Mhh,…hapana… kwa hivi sasa haitawezekana, tulitaka iwe hivyo, kabla hujapigiwa simu, lakini nilivyokwenda kumuona kwa hivi sasa hitawezekana, rafiki yako alitaka uwe karibu naye karibu …kwa muda huo.., unajua tena mlivyoshibana namuona , ..ana wasiwasi sana, nimemuambia hakuna cha kuhofi…’akasema
‘Mhh…ni kweli hata ingelikuwa ni mimi….’akasema rafiki yangu.
‘Ila hata hivyo nina mazungumzo mimi na wewe na…shemeji hapa, muhimu sana tukaongea, sasa sijui, na kama huna haraka, basi tusubirie ndani ya gari, maana mgonjwa hatakiwi kwasasa kuongea na watu wengi, mkewe sawa, anaweza kwenda kumuona mara moja, haijuzu…’akasema
‘Maongezi kuhusu nini hasa …?’ akauliza kwa mashaka, nakuniangalia mimi
‘Kuhusu mgonjwa, …na mengineo yake, wewe utanisaidia sana kwa hili, kama utakuwa mkweli, na halikadhalika rafiki yako, ni muhimu sana hili jambo, mkawa wawazi ili tuone jinsi gani ya kuliweka sawa,..ok, sasa sikilizeni,..eeh,…umesema mtoto yupo kwenye gari, nilikuwa nataka nimuone, unamficha sana, kwanini, unaogopa nini…, hahaha,, ...’akasema huyo docta akimwangalia huyo rafiki yangu, na huyo rafiki yangu akawa anamkwepa wasiangaliane, na kugeuka kuniangalia mimi, na mimi nikadakia na kuuliza
‘Mtoto wa nini bwana, wewe kwa sasa hutakiwi kuondoka hapa, mimi naona ..eeh ...’nikasema kabla sijamalizia simu ya docta ikaita
Docta akasema samahani aipokee hiyo simu, ni mteja wake muhimu…na kuchepuka pembeni, na mimi nikabakia na rafiki yangu, na hapo nikaona ni nafasi nzuri ya kuongea nilichotaka kukiongea, na sikutaka maongezi yangu hayo yasikiwe na huyo docta, nikamgeukia rafiki yangu na kusema;.
‘Nilikuwa nataka unifanyia kazi maalumu, ni kazi ambayo sikuwa nataka ifanywe na mtu mwingine...,lakini kwa sasa sina jinsi, na kutokana na maongezi yangu na huyu docta, nimeingiwa na mashaka …kuna kitu mume wangu ananificha…, nataka wewe unisaidie kwa hili, uchunguze ni kwanini mume wangu alikuwa na haraka hivyo, nina imani hiyo ajali sio ya bure bure, kuna jambo,…’akasema
‘Hata mimi naona hivyo, sio kawaida yake, kuna jambo..sizani kama …’akasita.
‘Sasa tuache dhana,..nataka uutafute ukweli, fuatilia nyendo zake, alikuwa anatokea wapi…maana alikuwa kwenye kikao, kwanini akatoka kwenye kikao kwa haraka, kuna nini alikuwa akifuatilia, na ni kwanini akaendesha kwa mwendo wa kasi hivyo, kuna kitu hapo…umenielewa hapo...’nikasema
‘Mhh…kwani docta kasemaje..?’ akaniuliza.
‘Docta ana mambo yake, ana shuku shuku zake..mimi sijamuelewa, …muhimu kwangu, ifanye hiyo kazi, wewe ondoka ukaifanye mengine niache mimi na docta tutayamaliza…’nikasema
‘Hujamuambia docta kuhusu mambo yetu, ..?’ akauliza
‘Yapi…?’ nikamuuliza
‘Si haya ya mtoto, tulivyokuwa tumepanga, mpaka ikatokea hivi, unakumbuka tulipanga nini, tukasema iwe siri yetu hata iweje tusije kuitia au sio, kumbuka,….ahadi ni deni….’akasema
‘Ni siri ...hilo siwezi kusahau, jamaa kanidadisi wee kafika sehemu kasalimu amri sasa anataka kupata taarifa kupitia kwako, mimi nakuahidi kuwa itaendelea kuwa siri, niamini hilo, unasikia, na wewe usije kunisaliti, ufunge huo mdomo wako, maana huyu docta ni mjanja sana, umenielewa…’nikasema
‘Sawa nimekuelewa,...kama ni hivyo nimekuelewa sana aheri umenishtua maana sikujua umeniitia nini..., lakini sasa kuhusu hiyo kazi mbona ni inakuja kuturudia, eeh, hebu elewa hapo…’akasema kwa kusita
‘Sikiliza mimi, kuturudia kwa vipi, na wewe bwana, haya yetu hayaguswi, unaonaeeh,..ninachotaka ni hivi, nijue kila kitu, kuhusu mume wangu... , sio kawaida yangu kufanya hayo lakini sina jinsi...'nikasema
'Nahisi kuna kitu, naanza kuingiwa na mashaka, sasa nataka kujiaminisha mwenyewe, je ni kweli wanayosema watu kuwa mume wangu ana tabia chafu, kuacha hizo za ulevi,...je kuna jambo la kunitia aibu, unajua kazi zetu zilivyo, kashfa zinaua soko, na wazazi wangu wakijua, nitaumbuka...'nikasema
'Mhh..lakini....'akataka kujitetea
'Mapema nikijua ni bora zaidi, tutajua jinsi gani ya kuyafukia mashimo, unanielewa hapo, hakuna jinsi, kama kafanya kafanya, lakini...kafanya nini...kama ni kazi za hivi hivi kupata soko, sawa, lakini kama ni mambo ya kibinadamu, labda...nasema mfano...tuone jinsi gani tutamsaidia...'nikasema
'Kama inatuhusu sisi wenyewe je...?' akauliza
'Kwa vipi...?' nikauliza
'mfano hii soo yetu...naona kama inakuzwa, na sijui docta kazungumzia nini, ndio nilitaka niongee na yeye nijue anajua nini, labda kasikia kitu...'akasema
'Hajasikia lolote, ndio ananichota chota mimi, nimuelezee, na mimi siwezi kuyaongea mambo yetu, kwa vile ni sirii yetu, sasa wewe tafuta bwana mtafute huyo mume muongee naye mliweke sawa, unanielewa...nilitaka nionane naye, lakini naona ..hata sijui kwanini umeninfanyia hivyo...'nikasema
'Kwahiyo....?' akauliza
'Mii ninachotaka ni kufahamu nyendo za mume wangu, ilikuwaje mpaka ikatokea hivyo, nikijua nitajua jinsi gani ya kumsaidia..nataka hilo ulifanye haraka iwezekanavyo, namuombea apone tu….nampenda sana mume wangu,
sitaki aje kukutana na kashfa mbaya, sijui kwanini,...ila nahisi kuna kimwanamke kinamsumbua, kama kipo nataka nikifahamu haraka iwezekanavyo, na nitajua jinsi gani ya kumfanya, atahama jiji...atajiua kabla hayajamkuta mauti…’nikasema
‘Mungu wangu, ina maana utamfanya kitu kibaya...?' akauliza
'Hutaamini kama nini, mimi na wewe ni rafiki, lakini hujawahi kuifahamu sehemu ya pili ya nilivyo..hutaamini...'nikasema nikionyesha uso ambao hajawahi kuuona kabla, nilimuona akitikisika.
'Kama ni hivyo, hapana......siwezi...'akasema
'Eti nini huwezi...acha tabia hiyo,…umeshanifanyia kazi zangu nyingi zaidi ya hii, hii ni muhimu kwangu kuliko, nataka nifahamu hili kabla mume wangu hajakaa sawa…unanielewa, na mengine uniachie mimi mwenyewe, nitajua ni nini la kufanya, 'nikasema
'Mungu wangu kwanini ....mbona imekuwa hivyo tena...'akasema
'Ogopa kuchezewa ndoa yako...unakuja kulifahamu hilo ukiolewa...'nikasema
'Kwahiyo, hata kama aliyefanya hivyo ni mtu wako wa karibu...?' akauliza
'Mtu wangu wa karibu hawezi kunifanyia hivyo, hilo halipo, ...sizani, ni nani huyo, hapana, sizani, eti docta anakushuku wewe...'nikasema
'Docta, kasemaje....?' akauliza kwa mashaka.
'Achana naye, ...sasa sikiliza fanya hivi, sehmu ya kuanzia, hebu jaribu kugundua huyo mzazi ni nani, huyo mzazi aliyekwenda kumuona hospitalini, na baadaye akaenda, au akataka kwenda kumuona nyumbani, ni nani,…nahisi ukianzia hapo unaweza kufika mahali, nahisi kuna kitu hapo, sitaki kumshuku mume wangu vibaya, lakini huyo mzazi ana lake jambo, nahis ndiye kidudud mtu….’akasema
‘Mzazi…!! Mzazi gani huyo…na kama ni kweli..?’ akauliza
‘Sipendi…unasikia, sipendi... nimekutuma kazi, fanya kazi…au…mbona una mashaka mashaka…sio kawaida yako, …utaifanya hi kazi au hutaifanya…?’ nikamuuliza na mara docta huyo akaja..

WAZO LA LEO: Ni vyema tukajenga tabia ya kuhakiki mambo, tusikimbilie shuku, au dhana mbaya. Ukiangalia kwa makini, dhana mbaya zinachukuliwa kwa uharaka zaidi kuliko dhana nzuri, watu wanafikia kuchukiana kisa , kasikia, kisa, kaambiwa....!Waliokuwa marafiki wanakuja kuwa maadui, na hata vita vingi duniani vimeanzia huko..watu wanafikia kuuana, kisa ni dhana, kisa alisema fulani, na maadui wanatumia mwanya huo, kuongeza fitina na propoganda potofu. Tujaribuni kuwa na uhakika na mambo ya kusikia, tusikimbilie hatua, kabla ya kujirizisha,.
 
ZINATOSHA?? AU TUENDELEE??
.......MKIJIBU NDANI YA DAKIKA 20 TUTAENDELEA....MKICHELEWA TUKUTANE SAA 5 USIKU
MUDA WA SASA: 19:10
 
SEHEMU YA 41


‘Docta ana mambo yake, ana shuku shuku zake..mimi sijamuelewa, najua ni kwanini,…muhimu kwangu, wewe uifanye hiyo kazi niliyokupa…sasa.., wewe ondoka ukaianze hiyo kazi mara moja, mengine niache mimi na docta tutayamaliza…’

Tuendelee na kisa chetu….

***************


Docta alikuwa anakuja, akiwa kashikilia simu yake mkononi, kama anaandika kitu kwenye simu yake, nahisi alikuwa akiongea na mtu fulani muhimu kwake…kuna muda alikuwa akiongea huku anageuka kidogo kutuangalia, ikanipa mashaka kuwa huyo anayeongea naye, anaweza akawa na jambo na sisi..lakini sikuwa na shaka na hilo.

Niliona kamaliza kuongea na sasa alikuwa akija pale tulipokaa mimi na rafiki yangu, lakini alikuwa hatuangalii, anaangalia simu yake,.. na alipotukaribia tu ,simu yake ikaita tena, ikabidi ageuka na kurudi pale alipokuwa awali, akaendelea kuongea na simu yake, na kwa muda huo rafiki yangu alikuwa kasimama hajui afanye nini,…

‘Sasa wewe unasubiria nini, nenda kaifanye hiyo kazi, ukimsubiria docta…akija hapa, ataanza kukudodosa, kwa maswali mengi ya ujanja ujanja…na lengo lake jingine anataka kumuona mtoto, nahisi kuna jambo analifahamu, anataka kulithibitisha,..au kuna jambo analifuatilia….’ nikasema hivyo.

‘Mhh,…ni kweli naondoka…ila mimi sijakuelewa hapo.., maana unachotaka ni kama mtu kuchunguza kivuli chako, ni mambo ambayo hata wewe mwenyewe unayafahamu,..’akasema

‘Nayafahamu kwa vipi, sijakuambia uchunguze mambo yetu, mimi ninachotaka ni wewe kuchunguza hili tukio la mume wangu, chanzo chake, na ni nini kipo nyuma ya haya yote, unajua…mimi sitaki mambo ya kusikia,..nataka ukweli, nataka uhakika,..sawa hisia hizo zipo, watu wanasema hili na lile, lakini mimi sio mtu wa kihivyo….nataka tuupate ukweli…’nikasema

‘Kwahiyo eeh, hili….’akasema na kabla hajamaliza, nikamkatiza kwa kusema;

‘Sitaki nikufundishe kazi…. siku zote nikikuelekeza kazi unasema nisikufundishe nimeshakupa kazi basi nikuachie wewe mwenyewe utajua jinsi gani ya kuifanya,…iweje leo, kulikoni, unajua naanza kukutilia mashaka,…’nikasema na yeye hapo akabakia kimia.

‘Katika jambo silitaki, ni kuwatilia mashaka watu wangu ninaowaamini…wewe nakuamini sana, nilikupeleka shule usomee ujasiri, ujua jinsi gani ya kujilinda, na uje kunisaidia na mimi, …unilinde kwa kila hali, unakumbuka, uliapa mbele yangu, ndio, urafiki upo pale pale, lakini mengine ni dhima, unanielewa hapo….’nikasema

‘Aaah,..ndio..naelewa…lakini kabla sijaifanya hii kazi, ni lazima tukubaliane…eeh, kuna utata hapa…’akasema

‘Kukubaliana husu malipo au, kama ni malipo hakuna shida, toka lini nikakupa kazi bila kukulipa, wewe angalia gharama zako nipatie ankara ya deni,…au unataka kusema nini…?’

‘Kwahiyo, mmh, unataka nimchunguze shemeji….mmmh….’akasema

‘Ndio…umchunguze, …kwa masilahi yake, na masilahi ya familia,….fanya ufanyalo, ila cha muhimu, nakuomba, na nasisitiza, mimi sitaki kashifa kwenye familia yangu, ..na hili tumeshaonywa na wazazi wangu mara nyingi, hata wewe uliwahi kusikia wakati baba akiongea, ..sasa kama kuna tatizo nataka tuliwahi mapema kabla halijafika kwa wazazi wangu,...’nikasema

‘Nikuulize tu, samahani bosi… kabla sijaondoka, sasa kama ni kweli mume wako kahusika na hicho unachokiita kashfa,..itakuwaje…?’ akauliza na mimi nikamuangalia kwa macho makali, nikasema

‘Ninacho-kiita mimi kashfa..una maana gani, lugha gani hiyo…..ok, sikiliza…mimi sitalivumilia kashfa yoyote kwenye familia yangu, hasa zile zenye kuharibu biashara, zenye kuharibu ndoa, zenye kuleta jina baya kwenye familia yangu, zote unazielewa..sitake nianza kuzitaja…’nikasema

‘Mhh…’akaguna hivyo.

‘Wazazi wangu unawafahamu walivyo, walinikataza nisioane na huyo mume wangu kisa ni kuhusu familia yao, kuwa eti imegubikwa na mambo hayo…mimi sikuamini hayo, najau tabia mtu anaijenga mwenyewe..mimi niliwahakikishia wazazi wangu kuwa kashfa mbaya hataiweza kutokea kwenye familia yangu…’nikasema

‘Lakini kashfa yaweza kutafsiriwa vingine,..kama jambo limefanyika kwa makubaliano linawezaje kuwa ni kashfa…muhimu tuliweke sawa,..kuna mambo labda yalifanyika hivyo, sasa labda imekuwa kinyume kutokana na kutokuelewana…sasa sizani ni kama ni kashfa, labda iwe ni kashafa kwa mtizamo wa watu wengine……’akasema

‘Kwa makubaliani!!! Weeeeh, makubaliano na nani..kuwa mimi nitendewe ubaya, kwa vipi sasa, kuwa mume wangu, mbona haiji akilini… kuwa yeye akazini nje ya ndoa au, tuchukulie kashfa hiyo ni ya ndoa, mimi sijui..yaani mimi, nikae na mume wangu kuwa akafanye hivyo,…au nimwambie mume wangu akaibe au..najua mume wangu hawezi kufanya hivyo, hata siku moja,..na mimi sio kichaa wa kukubaliana na ujinga kama huo, hata dunia itanicheka au unataka kusema nini…’nikasema.

‘Sawa…lakini nikuulize kitu kingine kutokana na hali ya shemeji, ukagundua kuwa kafanya hivyo, na hali kama hiyo, .. utachukua hatua gani, huoni unaweza kumuua mume wako bure....?’ akaniuliza na mimi nikageuka kumuangalia docta, alikuwa bado anaongea na simu, nikasema.

‘Kwanza tujue ukweli, unanielewa,, ....cha kufanya baada ya ukweli.. , nitajua mimi mwenyewe, hiyo sio kazi yako… ila kiukweli, kama ni kweli wanavyosema watu mimi bado siamini,…huyo aliyemghilibu mume wangu, huyo shetani mtu…kama kweli kaghilibiwa, maana mume wangu hakuwa na tabia hiyo,..huyo mtu, huyo shetani,,… nitahakikisha kuwa hanisahau maishani , na atajuta kuingilia ndoa za watu kupoje…’nikasema kwa ukali, na uso wangu ukiwa sasa umebadilika kabisa,….

Mdada aliniangalia usoni, akionyesha wasiwasi mkubwa, mpaka, akawa anarudi kinyume nyume..halafu akasimama ..rafiki yangu ni jasiri..alipitia mafunzo ya ujasiri, kwahiyo anajua aweje kwa wakati gani…, lakini kwa hali aliyoniona nayo usoni nahisi hakutarajia,…kabisa….

‘Ina maana utamuua au,…ha-ha- hata kama…?’ akaniuliza akionyesha wasiwasi, akasita kumalizia.

‘Wewe subiria tu…utaona nitakachokifanya, unajua nimevumilia sana, nimekuwa mtu wa watu, nawapenda sana watu wangu wa karibu, nawabeba kwa mbereko....sasa ina maana kwa hali hiyo watu wanipande hadi kichwani, hapana,..hata awe ni nani …’nikasema


‘Mhh, rafiki yangu siamini hili kabisa, lakini mume wako ni mtu mwema sana, na kama kafikia kulifanya lolote baya, atakuwa na sababu…sizani kama anaweza kufanya jambo ambalo analifahamu ni kinyume ..msamehe tu…’akasema

‘Nimsamehe nini sasa…kwanza, eeh, nisikilize, sio tukurupuke, kwanza, tujue kosa lake ni lipi,…ili tujue jinsii ya kumsaidia,…unajua yapo makosa ya kusamehe, mimi ni binadamu, nitayapima, …lakini sio kosa la kuingilia ndoa za watu…watu hao wanatakiwa kuuwawa…unasikia, ku-uwawa, sasa mimi niwachekee, ndoa sio kitu cha mchezo bibie…, ..’nikasema

‘Sikiliza…mimi naomba urejee yale mazungumzo yetu, mbona….’akasema

‘Mbona mbona nini…ile ni kitu kingine…najua unachotaka kukisema…ndio maana nilikusihi iwe siri…sasa kama na wewe umelikoroga huko, acha mwenye mali afanye kazi, yake utajua mwenyewe, na mimi natetea ndoa yangu…sasa nikuulize uUtaifanya hiyo kazi au huwezi nimpatie mtu mwingine..’nikasema kikazi zaidi.


‘Mimi naona sitaiweza hiyo kazi, ..na ukizingatia nina mtoto, si unajua tena….’akasema

‘Sikiliza, sitaki kusikia kauli hiyo…na nataka uifanye wewe….na nataka iwe siri kubwa, unanielewa, siri kubwa, sitaki watu wengine waje kuligundua hilo kabla yako, kuna watu wameshaanza kutaka kulifuatilia hilo tatizo la mume wangu, wanataka kujua kwanini mume wangu akawa hivyo,…hiyo ajali sio ya kawaida,…wameshaanza kutunga hadithi…najua wakitaka jambo watalipata tu…’nikasema

‘Akina nani hao…?’ akaniuliza akionyesha mashaka

‘Docta anataka na yeye kulichunguza kwa nia ya kumsaidia rafiki yake, najua sio hivyo tu,…najua kabisa… wazazi wangu watakuwa wamemtuma kufanya hivyo,…sasa sitaki aje kugundua kitu kabla ya yako, nataka wewe ukishagundua tunahakikisha hakijulikani kitu tena…unanisikia, umeona jinsi gani jambo hilo lilivyo nyeti,…umenielewa hapo…’nikasema

‘Mhh, mbona imekuwa ni tatizo, sikujua kuwa haya yote yanaweza kutokea,…sasa huyu docta anataka kutafuta nini,…ina maana ndio maana umeniita hapa, ili…na wazazi wako wanalifuatilia hili, mungu wangu …mimi sasa naanza kuogopa, naona nijiondokee tu kwenda kusoma haraka iwezekanavyo, ….’akasema sasa akirudi kinyume nyume

‘Sikiliza wewe ni rafiki yangu ninayekuamini, ndio maana kila kitu tunaambizana, na huwa tunashauriana kwa kila jambo, sawa si sawa....wewe ndio mimi, na wewe huwezi kufanya jambo la siri kinyume na makubaliano yetu, sizani kama wewe unaweza kunigeuka mimi…nimekuwa nikikulinda kwa kila hali, mpaka sasa.…’nikatulia

‘Ni kweli….’akasema sasa akiwa kainama chini kama mtoto mbele ya wazazi wake akiwa kakosa au kuona aibu. Ni lazima awe hivyo kwangu mimi licha ya urafiki lakini mimi nimekuwa kama mlezi, nilitumia gharama nyingi kumjenga huyu binti kutoka kwenye hali ya kukata tamaa hadi akafikia sehemu ya kujiamini..

***********

Rafiki yangu huyu, niliamua kumsaidia kutoka kwa wazazi wake, hii ni kutokana na ule ukaribu wetu, sikutaka nimsaidie kipesa tu, lakini pia kumjenga katika hali ambayo anaweza kufanya jambo lake kwa kujiamini.

Sisi kwenye familia yetu japokuwa tuna uwezo, lakini wazazi wetu walifanya juhudi kubwa ya kutujenga kihali ambayo mtu anaweza kufanya jambo bila kutegemea wazazi, walitujenga kujiajiri zaidi, pamoja na elimu yetu, na mimi nikaona nimsaidie rafiki yangu awe hivyo hivyo...

Wazazi wake kuna kipindi walitaka binti yao aolewe na mtu waliyeona kuwa atamfaa, na binti yao hakuwa tayari naye, kama alivyokuwa hayupo tayari kwa wanaume wengi waliomtaka kumuoa kabla ya huyo ambaye wazazi wake, waliamua kumshurutisha aolewe naye...ndio maana tatizo lake nikalichukulia sawa na la kwangu..kuwa hata mimi nilikataa kuolewa na chagua la wazazi wangu

‘Hawa wazazi wangu siwaelewi, kama wamenichoka, na huenda wanaona mimi ni mzigo kwao, waniambie, lakini sio kunitafutia mwanaume,....hivi wananionaje mimi, eti niolewe na yule mzee, ..eti kwa vile ni tajiri, ....hapana, siwezi kuishi na yule mzee, hata siku moja....’akaniambia.
 
Back
Top Bottom