Mkuranga, Pwani: Mwalimu afungwa kifungo cha maisha kwa kulawiti mwanafunzi

Unakuta mtu ana mke na familia sasa ndio mambo gani ya kijinga .!!

Mambo ya ngono ni kuendekeza na kulemaza akili tu ,mtu mzima badala a'focus kwenye kutafuta mali kazi kuwaza ngono yaani mpaka analawiti.

Madhara👉 Anaenda jela na ndoa ishakufa kama watoto ni wadogo wanakuwa nusu yatima ..Kama alikuwa tegemezi maisha yanakuwa magumu kwa familia yake.

Baadhi ya mambo yanapokemewa sio athari kwa mtendaji tu ,bali kuna mlolongo wa watu wataumia kupitia ujinga wako hata taifa kwa ujumla.
 
Wanaume ni viumbe katili kuwahi kutokea ktk uso wa dunia[emoji17]
C tabia ya mtu mmoja isiwe 7bu ya kuona kila mwanaume ni mchafu, mbona wanawek wakatili wapo hao wanaobeba mimba wanakuja kuitoa ina miezi nane wao unaweka kweny kundi gani ,au wanaojifungua watoto vizur alafu wanawatumbukiza chooni hiyo ni tabia tu ya mtu cyo kwamba kila mwanaume yupo hivyo..
 
Kuna makosa yanatakiwa kuondolewa haki ya rufaa ikiwa mtuhumiwa atatiwa hatiani na mahakama kujiridhisha, hili likiwemo.

Nayafikiria maumivu ya hao wazazi na mtoto nashindwa!
Hapana.
Sababu mtu anaweza jengewa mazingira ya kubambikiwa kosa hili kwa kisasi au kukomoana kumbe hajatenda kosa hilo. Au lengo la mabazazi kujipatia watakacho kirahisi.

Yaani mfano namtaka Nifah huku yeye moyo wake upo kwa Mwamba mwingine namuandalia zengwe mshindani anafungwa life sentence kisha najifanya mwema kumfariji Nifah huku nikijua kibinadamu Nifah atajikuta analipa fadhila kwangu wakati huo nami nikitimiza lengo langu.
 
Samahani Nifah kwa kutumia ID yako kutolea mfano huu.
 
Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga, imemhukumu kifungo cha maisha jela, aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi St Mathew iliyopo Kongowe, Livingston Kyarwenda (40), baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka tisa.

Kyarwenda, mkazi wa Mbagala Chamanzi anadaiwa kumlawiti mwanafunzi huyo wa kiume aliyekuwa anasoma darasa la nne katika vyoo vilivyopo shuleni hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo, Novemba 29, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Herieth Mwailolo, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

“Kwa kuzingatia uzito wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapa wa mashahidi watano ukiwemo ushahidi wa mtoto mwenyewe, mahakama hii imeridhika pasina kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa ulitenda kosa hilo kinyume cha sheria,” amesema Hakimu na kuongeza;

"Baada ya kukutia hatiani, mahakama hii inakuhukumu kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa iko wazi iwapo hujaridhika na hukumu hii."
Awali, wakili wa Serikali, Leon Kaikuye alidai kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu na upande wa mashtaka upo tayari kwa ajili ya uamuzi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 308 ya mwaka 2023, Mwalimu huyo anadaiwa kumwingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa kinyume cha kifungu cha 154 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code).

Mwananchi
Walezi wa watoto wetu wanapogeuka simba tumuamini nani!
 
Kama kweli ametenda kosa hilo, basi atakuwa amevuna alichopanda. Lakini kama amesingiziwa kwa kufanyiwa figisu na watesi wake, basi Mungu amsimamie na kuwapa malipizi hao watesi wake.
 
Akili yangu inanituma kama kama mwalimu kafanyiwa zengwe tu. Sema nini,hii dunia bana tunahitaji kuishi kwa tahadhari sana kama uwapo kwenye mbuga za wanyama
Usikae mda mrefu chobingo na mtoto wa mtu unajitafutia matatizo kaa nae open space kila mtu akuone sio unaenda kujifungia nae hata km hujamfanya kitu wanazengo lazima wakuungie pira la moto
 
Unakuta mtu ana mke na familia sasa ndio mambo gani ya kijinga .!!

Mambo ya ngono ni kuendekeza na kulemaza akili tu ,mtu mzima badala a'focus kwenye kutafuta mali kazi kuwaza ngono yaani mpaka analawiti.

Madhara👉 Anaenda jela na ndoa ishakufa kama watoto ni wadogo wanakuwa nusu yatima ..Kama alikuwa tegemezi maisha yanakuwa magumu kwa familia yake.

Baadhi ya mambo yanapokemewa sio athari kwa mtendaji tu ,bali kuna mlolongo wa watu wataumia kupitia ujinga wako hata taifa kwa ujumla.
Hii adhabu inaumiza wasio na hatia. Wangefyeka nyeti halafu aende kuhudumia familia, angejuta maisha yote. Jela atazoea ataanza kulawiti wenzake.
 
Unadhani mtoto wako yupo sehemu salama shuleni kumbe kuna baadhi ya walimu wenye roho za kishetani wanamtendea vibaya huyo mtoto!

Kama kweli ametenda hilo tukio basi hiyo ni stahiki yake.
 
Back
Top Bottom