Mkuranga, Pwani: Mwalimu afungwa kifungo cha maisha kwa kulawiti mwanafunzi

Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga, imemhukumu kifungo cha maisha jela, aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi St Mathew iliyopo Kongowe, Livingston Kyarwenda (40), baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka tisa.

Kyarwenda, mkazi wa Mbagala Chamanzi anadaiwa kumlawiti mwanafunzi huyo wa kiume aliyekuwa anasoma darasa la nne katika vyoo vilivyopo shuleni hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo, Novemba 29, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Herieth Mwailolo, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

“Kwa kuzingatia uzito wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapa wa mashahidi watano ukiwemo ushahidi wa mtoto mwenyewe, mahakama hii imeridhika pasina kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa ulitenda kosa hilo kinyume cha sheria,” amesema Hakimu na kuongeza;

"Baada ya kukutia hatiani, mahakama hii inakuhukumu kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa iko wazi iwapo hujaridhika na hukumu hii."
Awali, wakili wa Serikali, Leon Kaikuye alidai kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu na upande wa mashtaka upo tayari kwa ajili ya uamuzi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 308 ya mwaka 2023, Mwalimu huyo anadaiwa kumwingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa kinyume cha kifungu cha 154 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code).

Mwananchi
Huyo sio Mwalimu ni Mchawi[emoji24]
 
C tabia ya mtu mmoja isiwe 7bu ya kuona kila mwanaume ni mchafu, mbona wanawek wakatili wapo hao wanaobeba mimba wanakuja kuitoa ina miezi nane wao unaweka kweny kundi gani ,au wanaojifungua watoto vizur alafu wanawatumbukiza chooni hiyo ni tabia tu ya mtu cyo kwamba kila mwanaume yupo hivyo..
Hapana!! Nyie mmezidi 🙌
 
Tungepata mwenendo wa hii kesi kwanza.
Usikute mwalimu kayatimba tu kwa wazazi wenye pesa. Shule ya private kama ile ya St Matthew, mbona inajiharibia jina? Mutembei mmiliki hapa anasemaje?
Anyone to make follow up?
Inasemekana amefariki
 
Imagine ujasili anautoa wapi wa kuchojoa nguo zake atoe dyudyu lake amuingize kijana mdogo wa kiume uume wake?! Huu ukatili umepitiliza!!!
Km ni hamu za kimapenzi kina gigy wapo
Hivi kwa duni ya sasa wanawake ni wakutafuta kweli
 
Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga, imemhukumu kifungo cha maisha jela, aliyekuwa mwalimu wa Shule ya Msingi St Mathew iliyopo Kongowe, Livingston Kyarwenda (40), baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka tisa.

Kyarwenda, mkazi wa Mbagala Chamanzi anadaiwa kumlawiti mwanafunzi huyo wa kiume aliyekuwa anasoma darasa la nne katika vyoo vilivyopo shuleni hapo.

Uamuzi huo umetolewa leo, Novemba 29, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Herieth Mwailolo, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

“Kwa kuzingatia uzito wa ushahidi uliotolewa mahakamani hapa wa mashahidi watano ukiwemo ushahidi wa mtoto mwenyewe, mahakama hii imeridhika pasina kuacha shaka yoyote kuwa mshtakiwa ulitenda kosa hilo kinyume cha sheria,” amesema Hakimu na kuongeza;

"Baada ya kukutia hatiani, mahakama hii inakuhukumu kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hii na haki ya kukata rufaa iko wazi iwapo hujaridhika na hukumu hii."
Awali, wakili wa Serikali, Leon Kaikuye alidai kesi hiyo iliitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu na upande wa mashtaka upo tayari kwa ajili ya uamuzi.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 308 ya mwaka 2023, Mwalimu huyo anadaiwa kumwingilia kinyume cha maumbile mwanafunzi wake wa kiume mwenye umri wa miaka tisa kinyume cha kifungu cha 154 (1) (a) na (2) cha Sheria ya Kanuni za Adhabu (Penal Code).

Mwananchi
Alaf St. Mathew wanatabia ya kuwalazimisha wazazi watoto wa darasa la nne na saba kukaa boarding, jaman bora la saba ila la nne bado wadogo sana wanajifunza tabia kama hizi.

Huyo mwalimu nae kama anataka hayo mambo mbona watu wazima na vijana wapo, kwanini asitafute kwenye mitandao kama romeo na grindr wamejaa kila kona kuliko kumuhatibu mtoto mdogo jaman
 
Back
Top Bottom