Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkurugenzi amsimamisha kazi Mwalimu aliyewatuma wanafunzi kupakia kuni zake wakapata ajali ya gari
Njombe
Mwalimu Furaha Msule anayefundisha shule ya Sekondari Kidegembye iliyopo Lupembe halmashauri ya wilaya ya Njombe amesimamishwa kazi kwa kosa la kuwachukua wanafunzi na kuwapeleka kupakia kuni zake kinyume na sheria na kupelekea kupata ajali ya gari wakati wakirudi majira ya saa moja usiku.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Christopher Sanga ameeleza kumsimamisha kazi mwalimu Msule na kutoa wito kwa watumishi kufanya kazi kwa kufuata sheria kanuni na taratibu.
"Ofisi ya mkurugenzi kwa kushirikiana na tume ya walimu TSC imechukua hatua ya kumsimamisha kazi mwalimu aliyehusika huku utaratibu,sheria na kanuni zingine zikiendelea"amesema Sanga
Sanga amesema mnamo October,1,2023 ofisi yake ilipokea taarifa ya kutokea ajali ambapo mwalimu Furaha aliwachukua wanafunzi na kwenda kupakia kuni zake lakini kwa sasa wanafunzi wote 11 wakiwemo 6 waliokuwa wakitibiwa katika hospitali ya Kibena wameruhusiwa na kurejea shuleni.