Mkurugenzi Manispaa ya Songea akabidhi eneo la Mradi wa Ujenzi wa Soko la Sh Bilioni 22.9 - Manzese A na B

Mkurugenzi Manispaa ya Songea akabidhi eneo la Mradi wa Ujenzi wa Soko la Sh Bilioni 22.9 - Manzese A na B

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Machi 28, 2025, Mwanachama wa JamiiForums.com aliwasilisha andiko lake akilalamikia changamoto ya Miundombinu ya soko la Bombambili kwa kueleza Songea: Hali ya Soko la Bombambili si salama, wakati wa mvua hali ni mbaya

Alisema Soko la Bombambili ambapo ndipo Wafanyabiashara walipohamishiwa baada ya lile la Manzese kubomolewa, lina changamoto ya Miundombinu na hali huwa mbaya zaidi hasa wakati wa Mvua, akidai Wafanyabiashara na Wateja wanapata wakati mgumu kutokana na matope, uchafu na mvurugano, baada ya andiko hilo Serikali imetangaza hatua zinazofuata:

UAMUZI WA SERIKALI...
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Wakili Bashir Muhoja, tarehe 15 Julai 2025 amekabidhi rasmi eneo la mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa katika maeneo ya Manzese A & B pamoja na kiwanda cha kuchakata mazao ya nafaka kilichopo Kata ya Lilambo kwa Mhandisi kutoka Kampuni ya China National Aero Technology International Engineering Cooperation.

Mradi huo mkubwa unaogharimu jumla ya Shilingi Bilioni 22.9, unatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo na biashara katika Manispaa ya Songea kwa kuongeza thamani ya mazao, kukuza uchumi wa ndani, na kutoa ajira kwa wananchi wa maeneo husika.
MANZESE B.jpg

Picha ya Eneo la Soko la Manzese B kabla ya kuanza ujenzi.

manzese-a-b.jpg

Picha ya eneo la Soko la Manzese A kabla ya kuanza ujenzi.​

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi Muhoja alimtaka Mhandisi anayesimamia mradi huo kuhakikisha anafanya kazi kwa uweledi wa hali ya juu, uwajibikaji, na kuzingatia muda uliopangwa. Pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na mipango madhubuti ya kazi hususan katika kuzingatia msimu wa mvua unaokuja, ili mradi usikwame wala kucheleweshwa.

“Ninamtaka Mhandisi ahakikishe kazi hii inafanyika kwa viwango vya juu, kwa uadilifu, na kwa kuzingatia muda. Tunahitaji kuona tija kwa wananchi wetu, na hatutakuwa tayari kuona ucheleweshaji wowote unaotokana na kutozingatia hali ya hewa au maandalizi duni,” alisema Muhoja.

Kwa upande wake, mhandisi wa kampuni hiyo aliahidi kutekeleza mradi huo kwa kuzingatia viwango vya kimataifa na kuhakikisha unakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa.
Snapshot_391.png
Makabidhiano hayo yamepokelewa kwa matumaini makubwa na wananchi, ambapo wengi wameeleza kuwa mradi huo utasaidia kuboresha miundombinu ya masoko na kuimarisha mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo kwa wakulima wa maeneo hayo.

Ujenzi unatarajiwa kuanza rasmi katika kipindi kifupi kijacho mara baada ya maandalizi ya awali kukamilika.
WhatsApp Image 2025-03-28 at 12.21.43.jpeg

Hali ya Soko la Bombambili inavyokuwa wakati wa mvua
​
Pia soma ~ Songea: Baada ya malalamiko ya Wananchi, RC wa Ruvuma afanya ziara kukagua Soko la Bombambili na masoko ya Manzese A
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-03-28 at 12.21.43.jpeg
    WhatsApp Image 2025-03-28 at 12.21.43.jpeg
    255.4 KB · Views: 36
Back
Top Bottom