Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mwendokasi analipwa zaidi ya milioni kumi kwa mwezi; hajawahi hata kutembelea abiria aone kero zao

Nadhani haupo SAHIHI kiongozi,kwa huyu CEO mpya,Ndugu Kihamia ameshaanza kutembelea vituo mbalimbali vya huu MRADI wa Mwendokasi,..wiki iliyopita vyombo vingi vya habari vilionyesha picha zake akiwa na abiria,akipokea maoni toka kwao..tumpe nafasi

Sema namuonea huruma MGOSI kwa kubebeshwa huu MSALABA,sijui ataweza masikini?

Ukifuatilia michango ya waliokuwa Wabunge wa Upinzani wa Dar Es Salaam, wakiongozwa na Mh Mdee na Kubenea hata Mh Ex Mayor Mwita,miaka ya 2015-2020 ni kana kwamba MRADI huu ULIANZISHWA na KUTEKELEZWA KWA UBATILI MTUPU..Kuna ulaghai mwingi kuanzia Mikataba wenyewe,ununuzi wa Magari(Mdee alisema magari mengi ni Kuu kuu,tena akiwa ndani ya Bunge + over priced)

Kingine menejimenti iliyopewa kuendendesha Mradi huu,chini ya Bwana Kisena ,ilijaa UTAPELI ,UONGO,WIZI ndio maana Kisena et al wamehukumiwa nadhani miaka 10 Gerezani

Wito wangu,
i.Mh Mdee et al tokeni na endeleeni KUPAZA sauti hadi Majizi yote yapate stahilii zao,Kisena na hao wachache hawatoshi

ii.Serikali ipitie kikamilifu MIKATABA wote wa UENDESHAJI wa huu MRADI ili kujua UOZO wote na kufanya MABORESHO+ kuwafikisha mahakamani WEZI wote

III.Serikali kununua mabasi mengi aliyo kwenye hali nzuri kwa kuangalia taratibu na kanuni zote za manunuzi.

IV;Watafutwe WEENDESHAjI NGULI ndani or nje ya Tz kwa ajili ya kusimamia Mradi huu

OR

V.Tuwape sekta BINAFSI kwa ajili ya kuuendesha kwa 100% ,serikali ibaki kuboresha MIUNDO MBINU + kukusanya KODI
 
Madhara ya kuteuliwa kwa fadhila badala ya kupata kazi kwa vigezo. Kwani kuna anayejua ni sifa gani zimepelekea akateuliwa kwenye hiyo nafasi??
Huyu Mkurugenzi ni nani? Usikute ni yule aliyetoka LATRA!
kama ni huyu basi hakuna cha kwenda mbele zaidi ya majungu yake, fitna na kutishia walio chini yake!
 
Jibu swali. Kugombea basi unataka Mkurugenzi ajr kuwapangisha foleni ya kupanda basi?
 
Mkurugenzi katoka tume ya uchaguzi....!! Labda tujue kwani lazima wakurugenzi wa taasisi watoke TISS hata kama hawana hizo taaluma ? Kwani lazima mwendokasi iwe ya serikali 100% ?
 
Kwa imani yangu.
Huu mradi wakipewa wapiga debe wa stendi..madereva na makondakta watafanya vizuri sana sana.
 
Tatizo magari hakuna ndo maana Mbagala gari haziendi
 
Yule Asumani Kihamia kateuliwa juzi tu, ndo mkurugenzi wa mwendokas?
 
Huyo mkurugenzi ni mafiii kabisa hata mabasi ya mwendikasi hayafanyiwi usafi hata siku moja kapokea maagizo kutoka kwa raia feki kuwa afanye hayo anayo yafanya nilisema hapa Rostam azizi na familia yake wasipo uliwa nchi itakwama watu mnanipuuza
 
Kugombea basi na hapo mnamlaumu Mkurugenzi?
Kushangaa kwako ndiyo kunamfanya Mkurugenzi asitambue jukumu lake la msingi. Ufanisi wa uongozi wa Kiongozi Mkuu ni kuondoa adha huyo ambaye mazingira ya utendaji wa.Dart yanamlazimu agombee kuingia kwenye gari ili asisubiri dakika 47 nyingine.
 
Tukupe wewe mradi
 
Huyu Mkurugenzi ni nani? Usikute ni yule aliyetoka LATRA!
kama ni huyu basi hakuna cha kwenda mbele zaidi ya majungu yake, fitna na kutishia walio chini yake!
Huyu ni Athumani Kihamia, CV yake ni kuwa katibu tawara mkoa, mkurugenzi wa uchaguzi a.k.a fundi wa kuiba uchaguzi N.K
 
Mchengerwa na Chalamila walisomea wapi usafirishaji wa abiria katika majiji? Hizi kazi zinasomewa na zinahitaji hesabu, utafiti wa njia, na utaratibu wa uendeshaji unaotoa viwango vya utendaji; kwa mfano, kwa mabasi 20, pale Fire, gari liendalo Kivukoni linatakiwa lipite kila baada ya dakika ngapi na ratiba hiyo ifuatwe! Hili linawezekana kwa sababu mabasi haya yana barabara zake! Kazi hizo zinatakiwa zitangazwe, si kazi ya uteuzi wa sura! Waziri akitaka, atembelee nchi nyingine ajifunze utawala/uendeshaji wa usafiri katika majiji ili ajue uongozi wake unahitaji nini. Mwalimu Chalamila anajua kukemea watoto darasani. Sosholojia na saikolojia ya kuendesha watu wazima ni jambo la kujifunza.
 
Hapo ni kuyasusia kupanda pengine watawaelewa
 
Siku hizi mwendokasi ukipita lazima ukute gari sio chini ya 3 zimeharibika njiani yani ni USUMBUFUU PLUS KWA WANANCHI.. unakata ticket unalipa nauli gari zinaharibikia njiani kiufupi hawana magariii hayo yanayotembea ni roho ngumu tu na wanamalizia kuyaua jumla.
 
Mkurugenzi gani tena huyo hajafika site jamani?
Ata tajiri kisena na mke wake enzi hizo daily walifika jangwani pale kwa wizi tu. Huyo ambaye hafiki ofisini mkurugenzi gani?
Hata asumani mbona yeye daily yupo kwenye road. Ni yupi mnamuongelea.
Nyie semeniwendokasi kichwa cha mwendawazimu sio maboss
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…