Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dr Ayoub Ryoba aendeleza matusi kwa wakosoaji wake. Aivaa JamiiForums...

Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dr Ayoub Ryoba aendeleza matusi kwa wakosoaji wake. Aivaa JamiiForums...

JINOME

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Posts
958
Reaction score
1,427
Amani kwenu wadau,

Wiki moja iliyopita niliwaeleza jinsi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la habari Tanzania (TBC), AYOUB RYOBA alivyotaka kupigana na mtangazaji wa EFM Radio, Gerald Hando
Dr. Rioba wa TBC ataka kupigana na Gerald Hando wa E-FM kwa kuambiwa TBC imemshinda

Jana TANAPA walikutana na wahariri jijini Tanga ili kuzungumzia uanzishwaji wa CHANELI ya Wanyama TBC. Katika kikao hicho ambacho AYOUB RYOBA alihudhuria, ulipofika wakati maswali, bosi huyo wa TBC aliulizwa juu ya tuhuma za kutaka kupigana na Gerald Hando wa EFM ndipo Dkt. Ryoba alipoanza tambo, kebehi ,matusi na dhihaka badala ya kujibu swali aliloulizwa.

Hii hapa ni nukuu ya maneno yake:
"Kuna Dada kanifuata kuniuliza upumbavu. Mimi sijibu upumbavu. Mimi si mnafiki, hata huyo aliyeniuliza sijui kama hata amemaliza darasa la saba hata digirii hana.

Jamii Forum nilipokuwa Ulaya nilikuwa naitumia sana kama chanzo cha kupata taarifa na kushiriki mijadala. Najua kuna maprofesa, majenerali wengi walikuwa member humu

Lkn sasa uongo na uzushi umezidi. Mimi siku nasoma taarifa ya kuteuliwa nilikuwa na kazi ya kulipwa milioni 60, ndiye mwandishi wa kwanza kumiliki Range Rover, sasa hivi hali yangu mbaya, natukanwa zaidi, afya yangu mbaya ....

Hata kama nitatumbuliwa nitaendelea kumuunga mkono (rais)."

Baada ya maneno hayo ya Ryoba, ABISALUM KIBANDA alimtaka Mkurugenzi huyo Mkuu wa TBC kuacha lugha za matusi na dharau kwani ni mtu msomi, kiongozi na mtu anastahili kuheshimu watu ii naye aweze kuheshimiwa
 
Mimi nahitaji kujua kwamba ukiwa mhadhiri kweli waweza lipwa hio 60 milioni? sasa jamaa amesoma na anajua kua haiwezekani kulipwa mil 60 tbc kwanini alicha huko na kwenda tbc ukiwa mnafiki na muongo lazina uwe na kumbukumbu vizuri
 
Mimi nahitaji kujua kwamba ukiwa mhadhiri kweli waweza lipwa hio 60 milioni? sasa jamaa amesoma na anajua kua haiwezekani kulipwa mil 60 tbc kwanini alicha huko na kwenda tbc ukiwa mnafiki na muongo lazina uwe na kumbukumbu vizuri
Alikuwa anafundisha vyuo zaidi ya kimoja akikusanya income inafika!
 
Naona mnamkoroga sana huyo baba wa watu, kana kwamba hamjui kuongoza lile dude ni headache ya kiwango cha mwisho kabisa cha maumivu..
 
Back
Top Bottom