Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana


Dah acha tu nikuonee huruma.
 
Pole sana kaka Max najua uko sahihi pigania unachokiamini kuacha heshima yako duniani
[HASHTAG]#justiceformelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#FreedomofSpeech4All[/HASHTAG]
 
Mimi toka nilipoitwa kuchunguzwa kipindi kile natumia ID fake na kilichonikuta huko, sikuona haja tena ya kuogopa MTU, kwani kile nilichofanyiwa hakijapishana sana na adhabu ya kaburi.

Kwa sasa kama ni mbwai wacha iwe mbwai, uwoga mwiko.
Natumia jina langu halisi na hata Namba ya simu ukitaka nakupa na ukibip nakupigia.

Narudia tena UWOGA MWIKO
 
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema yupo magereza kwa kosa la kupinga udikteta uchwara kwenye nchi yetu mtu mmoja kujiona yeye ana mamlaka yote.
Tuungane bila kujali itikadi za vyama kupinga udikteta uchwara kwenye nchi yetu. @Maxence amekamatwa na kunyimwa dhamana kwa sababu maalumu hatuwezi kukubali tena upuuzi kuendelea
 
Mbona Tim Cook CEO wa Apple Inc. hakukamatwa na kuwekwa ndani kwa kukataa kuwapa FBI taarifa za kwenye simu ya yule gaidi. Huku Tz Polisi wetu sijui wana shida gani hasa!! Wangefungua kesi dhidi ya Jamii Media na sio kumkamata mkurugenzi wake
 
[...Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. .

Sijui zile taarifa za waliogawana hela pale bank na kuzibeba ndani ya sandarusi walishaiomba? hii hatari sasa..
 
Kuhusu ishu ya iOS

FBI walisaidiwa na kampuni moja ya security, ile simu walichezea hardware ikafunguka..

Hawaku hack server wala nn
 
Kumenya uhuru wa habari kwa mabavu ni sawa na kukamata sabuni ya mche iliuyoloa maji mkononi kwa nguvu...itateleza na kudondokea mbali...tusubiri tuone mwisho wa hii sinema.
 

Hilo nisawasawa
 
Tusizunguke mbuyu, leta jambo lolote au tukio lililochochewa na hayo mabandiko.
Let's deal with facts and not fiction.
 
Huo ndio ukweli inasikitisha lkn ndiyo hivyo wote ninyi akiwahitaji kesho hamtakuwepo!
Hatutakuwepo kimwili lkn kiroho tutakuwepo. Achague kuitumikia serikali akose member's ambayo itampelekea kufunga au awe huru apate members
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…