Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Makamu akijiuzulu watu wanaingia mitaani kufanya fujo?
Soma hii uone kama kusema amejuizulu kunaleta shida:
Whoever, by words, either spoken or written, or by signs, or by visible representation, or otherwise, brings or attempts to bring into hatred or contempt, or excites or attempts to excite disaffection towards,

Dah acha tu nikuonee huruma.
 
Pole sana kaka Max najua uko sahihi pigania unachokiamini kuacha heshima yako duniani
[HASHTAG]#justiceformelo[/HASHTAG]
[HASHTAG]#FreedomofSpeech4All[/HASHTAG]
 
Mimi toka nilipoitwa kuchunguzwa kipindi kile natumia ID fake na kilichonikuta huko, sikuona haja tena ya kuogopa MTU, kwani kile nilichofanyiwa hakijapishana sana na adhabu ya kaburi.

Kwa sasa kama ni mbwai wacha iwe mbwai, uwoga mwiko.
Natumia jina langu halisi na hata Namba ya simu ukitaka nakupa na ukibip nakupigia.

Narudia tena UWOGA MWIKO
 
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema yupo magereza kwa kosa la kupinga udikteta uchwara kwenye nchi yetu mtu mmoja kujiona yeye ana mamlaka yote.
Tuungane bila kujali itikadi za vyama kupinga udikteta uchwara kwenye nchi yetu. @Maxence amekamatwa na kunyimwa dhamana kwa sababu maalumu hatuwezi kukubali tena upuuzi kuendelea
 
Mbona Tim Cook CEO wa Apple Inc. hakukamatwa na kuwekwa ndani kwa kukataa kuwapa FBI taarifa za kwenye simu ya yule gaidi. Huku Tz Polisi wetu sijui wana shida gani hasa!! Wangefungua kesi dhidi ya Jamii Media na sio kumkamata mkurugenzi wake
 
[...Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. .

Sijui zile taarifa za waliogawana hela pale bank na kuzibeba ndani ya sandarusi walishaiomba? hii hatari sasa..
 
I thought wangefanya jitihada kuhack hii jf na kutafuta wanachokitaka instead ya kumuwajibisha mmiliki.

Inanikumbusha kesi ya Apple na FBI kuhusu kuwapa backdoor ya IOS, mahakamani walishindwa FBI then they bypass it kupitia third person.

Kuna haja ya kuongeza wataalam wa ethical hacking katika kitengo chao. I can't believe imewashinda kuhack server.
Kuhusu ishu ya iOS

FBI walisaidiwa na kampuni moja ya security, ile simu walichezea hardware ikafunguka..

Hawaku hack server wala nn
 
Kumenya uhuru wa habari kwa mabavu ni sawa na kukamata sabuni ya mche iliuyoloa maji mkononi kwa nguvu...itateleza na kudondokea mbali...tusubiri tuone mwisho wa hii sinema.
 
Unaweza kuwa na wazo huru lakini la kizushi na hali itakapochafuka watu watakupatia wapi wakati unasajili humu JF detail zako zote zipo kwa Maxence Melo ambae leo hii yeye ndio anasota rumande wewe unakatisha tu mitaa.
kama detail ulizoweka ni za uongo hapo ni inshu nyingine yeye anatakiwa kuweka vigezo na masharti ya kujiunga humu JF vinavyoendana na sheria za nchi.

Hilo nisawasawa
 
Tusizunguke mbuyu, leta jambo lolote au tukio lililochochewa na hayo mabandiko.
Let's deal with facts and not fiction.
Kuna uzi humu ulisema wazi na ushahidi kuwa Makamu wa rais amejiuzulu.

Kuna uzi humu ulipost barua ya ikulu ikionyesha nembo ya ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu ikielezea kutenguliwa kwa mrisho gambo. Huo sio uchochezi ? Au uchochezi kwako ni mpaka watu washike bunduki
 
Huo ndio ukweli inasikitisha lkn ndiyo hivyo wote ninyi akiwahitaji kesho hamtakuwepo!
Hatutakuwepo kimwili lkn kiroho tutakuwepo. Achague kuitumikia serikali akose member's ambayo itampelekea kufunga au awe huru apate members
 
Back
Top Bottom