Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Hizo resources, muda, nguvu wangezielekeza kwa jamaa waliokufa mto ruvu nadhan tusingekuwa na majibu mapesi kama ya "ni wahamiaji haramu". Tupo pamoja Mkuu hope kila kitu kitakaa vizuri. Nakuombea
 
Huyu jamaa ninamnyanyulia mikono, hua naguswa sana nikiona watu wanapigania kile wanachokiamini.
Bila watu kama hawa hata leo hii tungekua chini ya wakoloni, ni watu kama Nyerere waliamua kujitoa hadi leo hii tunafurahia uhuru, japo sio uhuru 100% maana hawa viongozi weusi nao wana porojo za kujigeuza miungu watu.
 
Hivi jamani ndg zangu wana usalama hamna kazi zingine za kufanya ili kusaidia nchi yetu?
mnakuwa kama VIBARAKA? ni Aibu kabisa ., anyway kila kitu kina Mwanzo na Mwisho.
 
Nilisema Watanzania tumegawanyika na waoga kama Nyumbu

Kundi moja linaonewa, wengine wanakaa kimya jinsi Mamba anavyomla Nyumbu

Mfano: Madokta waligoma, hakuna aliyewaunga mkono

Wafanyakazi wakalia kuhusu FAO La kujitoa, wengine kimya

Sheria ya Vyombo vya habari ikaja, wanahabari nao wakakosa support

Wanafunzi wakakosa mikopo, watu wengine kimya

Sasa ni JF, wengine kimya

Kuna principle inasema, mmoja wetu akionewa, ni wote tumeonewa (hii Tanzania hakuna).......

Watawala watatunyanyasa sana na kura watachukua kwa nguvu.....FFU watapiga mabomu mkikaa mita 200
 
Na yeye ni mmoja wapo wa hao wanaotafutwa. Sababu hiyo habari na yenyewe iliwekwa humu so polisi wakishapata hizo details zao ndio tutajua watakachofanywa
ina maana hajuikani? mbona magazeti yaliandika na mahakama ikakanusha? kwa nini wasimuulize mkurugenzi aliyepokea hiyo amri ya mahakama mpaka wategemee jamii forums?
 
Max naamini atasimama imara,ila wapi freedom of speech jamani?Magu ujue 2020 siyo mbali
 
Taratibu naona utamaduni na desturi za Korea kasikazini zikienea taratibu
 
Sasa unaweza kufanya nini mtu mwenye silaha na mamlaka akikukamata iwe kwa kosa ama kuonewa?
 
G
Kama ni hivvyo unavyoamini basi haujauelewa Ukristo, Yesu alisema siku ya mwisho nitarudi kuwahukumu wazima na wafu, hivyo kwa mujibu wa Yesu na mafundisho ya Kikristo bado tunasubiri hukumu yao/yetu!
Aisee kumbe unasahau neno hili alilosema yesu "wengine kutokana na dhambi zao zimekwisha watangulia hukumuni" hivyo wale waliomsulubisha yesu tayari walisha hukumiwa
 
Mimi nadhani upole wetu wtz ndo kuumia kwetu, hawa jamaa wameshavuka mstari, inabidi kuwatuliza kwanza, kwa mwendo wetu huu wa kulalamika itafika kipindi tutakuwa kama north korea, inabidi tuanze ku deal nao, especially watu wa juu sio hawa polisi wanaotumika, nchi za magharibu huwezi fanya upuuzi huu,Nigeria wanamsemo wao wanasema "u do I do", kama wao wamezamilia kumaliza vijana wote tukumbuke pia na wao wako na familia zao, tuamkeni.
 
Mkuu onesha mfano basi sio unaishia kusema tu humu,maana nawe utakuwa kama hao wanaoishia kulalamika tu.
 
Sasa kila mwana jf achunguze kwanza tread zake zote ambazo alishapost halafu ajipime je yuko salama maana unaweza pata presha bule kumbe uko salama
 
Hizi hali sio ngeni katika nchi za Afrika lakini Tanzania kwa muda mrefu tulijisifu afadhali ukilinganisha na nchi hizo. Watanzania hawakulelewa hivi, hawakuzoea mazila ya namna hii. Kwa hali inavyokwenda na ongezeko la vijana ambao ndio wapiga kura, ima CCM ijiandae kushindwa kwa nguvu ya kura au waipeleke Tanzania kwenye mkumbo wa nchi nyingine za kiafrika-Gambia, Kenya, Liberia nk.

Amani iliyokuwepo ni kutokana na busara chache walizokuwa nazo viongozi wetu toka huko nyuma. Tukiruhusu busara hizi zipotee, tutakuja kujuta. Sisi hatuna tofauti yoyote na waafrika wengine, hivyo mabaya yanayoendelea huko yanaweza pia kutokea nchini kwetu. Mungu aepushe hali hii japo nahisi haiko mbali.
 
Mlijiachia sana wacha wawashtue kidogo,dharau zilizidi mno kwa rais wa nchi hata penye ukweli mnapinga tu. Wakati mwingine nilifananisha hapa km mange kimambi asiejielewa huku mkiwa na fake ID.
 
Kunywa Maji mwanangu.......if your afraid of writting anything on social media then you need a new election"emphasis is mine"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…