Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mlijiachia sana wacha wawashtue kidogo,dharau zilizidi mno kwa rais wa nchi hata penye ukweli mnapinga tu. Wakati mwingine nilifananisha hapa km mange kimambi asiejielewa huku mkiwa na fake ID.
Kwahyo raisi hapingwi !??
 
watu wanaongea ukweli uliopitiliza na jamaa hawako tayari kuvumilia. Wanaotafutwa ni wale wanaokosoa tu.Kama.unasifia usishangae kupata cheo
kina lizaboni@rutashobolwa@MOTOCHINI wangoje kupanda vyeo
 
sheria ya Mitandao ya mwaka 2015 imo wazi sana ktk hili
 
Ndio maana naanza kuisifia serikali siku Hizi...
 
Hii huwa ni battle kubwa sana na sio Bongo tu.. Watu wa usalama wanaamini ni interest za security ya nchi wamiliki wa platforms wanaamini ni muhimu kulinda usiri.. Mmoja huwa anashinda..
 
Maxence Melo, mkurugenzi mtendaji wa jamii forums amekamatwa na jeshi la polisi, kituo cha kati Dar.

Polisi wanaeleza kuwa kesho atafikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kutoa ushirikiano kwa mamlaka.


Kesho atapanda kizimbani.
Lakini mbona hili ni kosa la kipuuzi sana kiasi kwamba halingii akilini badala yake linazua maswali yawezekana kuna cha ziada ambacho sisi hatukijui kilichofanya wao wamshikilie!!!?

sasa vipi kama ikiwa ni kweli hafahamu taarifa za hao watu si mwishoe atawapa taarifa za uongo hili tu apone!?

Alafu kwani hao whalifu wengine wanaowakamataga huko facebook huwa wanasaidiwa na wamiliki wa mtandao? au wameamua tu kuuonea huu kwa sababu ni mtandao wa hapa hapa Tz.

Hili linchi limekuwa la ajabu sana
 
dah! nimeangalia movie ya JASON BOURNE ya 2016
sikuamini kwamba haya mambo yanaweza kutokea katika nchi yangu
mpaka leo!
 
Asa nitakuwa secret star kweli kama polisi wanataka siri zangu za chumbani! Ngoja nijiite open star sasa..
 
JK aliiwezaje hii nchi? Tulikuwa na shida lakini maisha yalikuwa yanaenda just fairly!
 
Uhuru wa kuongea upo ila baada ya kuongea unatoweka haraka sana
 
Nenda Brunei wamefungua ubalozi mikocheni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…