Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Were hujitambui kwasasa unakurupuka
Nimekuambia
Sheria ya mitandaoni ilipitishwa kipindi Magufuli hategemewi kuwa Rais
Tena Huyo Lowassa ni mmoja wa walio pitisha sheria hiyo

Point. Tena wengi wetu hapa tumekuwa tukimsifia Kikwete kwamba aliruhusu uhuru wa watu kujieleza hata mitandaoni tukiwa ama tumesahau au hatujui kwamba ni Kikwete ndiye aliyetega bomu la sheria ya matumizi ya mitandao kabla hajasepa.
 
Siwezi kupanda zaidi ya hapa sana sana ni kushuka tu (kwa hiari) au kubakia hapa hapa kwa maana nimeshafikia mwisho wa nilichonuia kukifanya maishani mwangu!
Kama umemaliza wengine ndo tunaanza. Tafadhali we na wenzio mliomaliza mtuache tutengeneze kesho yetu.
 
Jamii forum wabadilike ili kila mwanachama aje humu kwa jina lake halisi kwani kuna ubaya gani?

Hivi kama wewe unamheshimu na kumwogopa Mungu na umeahidi moyoni mwako kuyatenda yaliyo ya kweli na kuukwepa uongo.

Harafu ukajiunga jf kwa jina la uongo huoni kwamba unatenda dhambi?

Jf inawaongoza wana chama wake kutenda dhambi ya uongo na kwenda jehanum ya moto.

Nashauri kila mwanachama aje kwa jina lake halisi.
Kwa majina haya ya uongo kitu gani kinafichwa?
Sasa kama kutenda dhambi na unalijua hilo kwanini bado una ID fake?
Watanzania unafiki tutaacha lini sijui!!!
 
JF kuwe na Plan B. Hizi ni zama ngumu kabisa katika uhuru wa kujieleza. Ikitokea baya limeikumba JF basi kuwe walau na namna hizi habari zote zirudi ili mijadala iendelee, baada ya hao wadhalimu kushindwa

Hakuna mahali duniani utawala dhalimu umedumu muda mrefu. Aliuliwa Ghadafi mtaroni na Sadam kwenye kishimo kama fuko nani atashindikana?

So chondechonde admins wa JF kuweni na backup ya mijadala yote humu maana kuna kila dalili za watawala wa sasa kutamani kuifungia kwa sheria au kwa ubabe.
 
Jamii forum siyo forum ya kwanza duniani, na hakuna mahali ambapo members wanalazimishwa kuja na identity zao kamili.
Huu ni ushauri kwa wale wenye hofu ya Mungu kutambua kuwa kujisajiri kwa majina ya uongo ni kutenda dhambi ya uongo.

Na hii ndiyo sababu wengi wanajificha kwenye majina ya uongo kudaganya au kutukana.
Wakiamini hawawezi kupatikana.
 
Hilo tukio unalolisema mimi binafsi nililijua humu JF baada ya mtoa mada kupost. Hivyo kila mtu anaamini na anahisi nani aliyefoji ile documents. Thays y polisi wanamtaka huyo aliyepost aseme kalitoa wapi na ili waweze kumpata muhusika na speculation kama hizo zako za kudhania ziwe confirmed.

Kwa hili serikali ina nia njema sana. JF inabidi irudi kipindi kile cha Na sio sasa imekuwa Political Forums. Kwa CCM na Chadema kuleta habari zao za kichochezi huku hawatoi hata 30,000 za kuwa Gold members
JF ina majukwaa mengi ukiona Jukwaa la siasa ni moto unaenda kujipoza mmu.
 
Tafadhali msitunyang'anye Jf, ndio social network pekee iliyo bora hapa tz na East Africa. Hakuna jambo litatokea halafu usilione Jf
 
Sasa dhana ya "rule of law" ina maana gani?
Na uzushi anaweza kujaji kwamba huu ni uzushi ni nani?
Hii serikali silijinasibu kwamba niya wanyonge, kwann wa kubwa wanaachwa , wadogo wanasakwa?

Tofautisha uzushi na uchochezi. Uzushi ni kama huu mnaoeneza kuwa Ben Saanane katekwa na CCM uchochezi ni kugushi nyaraka muhimu za serikali ili kucreate panic au chaos kwa wananchi.

Kwa mfano Aliyefoji na kupost ile barua ya mahakama kuzuia uchaguzi wa meya mpaka chombo na mhimili mkubwa kama mahakama kuja kukanusha ule uchochezi. Na judging by political situation ya kipindi kile ingeweza hata kuleta machafuko kati ya wafuasi wa chadema na ccm.
 
Jamii forum wabadilike ili kila mwanachama aje humu kwa jina lake halisi kwani kuna ubaya gani?

Hivi kama wewe unamheshimu na kumwogopa Mungu na umeahidi moyoni mwako kuyatenda yaliyo ya kweli na kuukwepa uongo.

Harafu ukajiunga jf kwa jina la uongo huoni kwamba unatenda dhambi?

Jf inawaongoza wana chama wake kutenda dhambi ya uongo na kwenda jehanum ya moto.

Nashauri kila mwanachama aje kwa jina lake halisi.
Kwa majina haya ya uongo kitu gani kinafichwa?
Unafiki unafiki tu kwa nn usianze na ww kuwa verified user
 
JF ina majukwaa mengi ukiona Jukwaa la siasa ni moto unaenda kujipoza mmu.

Hii comment yako inahusiana nini na Mada husika au hicho nilichokipost. Watu kama nyinyi ndio mnaosababisha kutia madoa JF na kuwaweka matatizoni viongozi wake
 
Nafikiri wafunge tu social media zote kama ndio raha yao. Mbona simple tu? Kwamba kuanzia leo hakuna Facebook,Insta.tweeter na n.k
twitter!! halafu on behalf of my self mkulu ataandika wapi!!

just joking
 
JF ina rensponsibility kubwa sana, kama vivlivyo vyombo vingine vya Habari, kuna mambo mengi ya uongo na uzushi huletwa humu na kuachwa, ikumbukwe kwamba nchi nyingi kama Kenya, Rwanda, Burundi n.k Vita ililetwa na Vyombo vya Habari kama redio na TV, hivyo JF ina jukumu la kulinda amani ya nchi, kama ni kweli amekamatwa, na kama siyo kweli basi wajifunze na wabadilike, watambue jukumu lao kwenye Jamii!

CEO wa JF asipumbazwe na watu wanaosapoti kwenda kinyume na Serikali hapa, wengi wao wana maisha yao na wala hawaishi TZ, na JF ikifa kesho, au ofisi ya JF kunyimwa kibali cha kufanya kazi TZ hawana cha kupoteza, zaidi ya kuhamia kwenye mtandao mwingine na kuendeleza wanayoyafanya, hivyo angalia maisha yako na familia yako, fanya lililo sahihi na jinsi Serikali inavyokutaka kwani mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye nchi, watakushauri wanachama wa JF wanavyotaka lkn Serikali ndiyo wasimamizi wa hii nchi!
Julius Nyerere, Kwame Nkrumah, Nelson Mandela, Samorah Machel, n.k hawa wangekuwa na akili za kipuuzi kama hizi mkoloni leo angekuwa bado yuko
 
Mimi sishangai aisee, haya niliyatarajia kabisa tangu mwanzo.
 
Wewe punguani kweli unadhani JF ni mali ya Chadema.

JF ni jukwaa huru.

Nyienyie ccm ndio vinara wa matusi humu.Hili si la chama we kijana.Hata wewe ni muhanga.Sasa matusi na dharau za nini?
 
sio swala la hata sisi tupo mashakani!!!!!
sababu kisa cha yeye kuwa huko ni sisi member ..... kwahiyo sisi ndo tupo mashakani yeye ni kwavile tu amegoma kuwapatia majina
hehehee ngoja nihame id hii kwanza niende ile ingine kiboo
Exactly amekubali yote kwa sababu ya kuwalinda members

Inatisha sana
 
Back
Top Bottom