Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Max mkuu pole kwa yaliyo kupata naamini unaipigania JF ili kulinda mawazo yetu huru,tuko pamoja mkuu,tukisubiri yatakayo endelea kesho.
 
Vipo vigezo humu na masharti pia. Ulitaka yapi tena? Au ndio woga kwahiyo unaanza kujitakatisha na comments safi
 
 
Sizonje mtu wa ajabu kabisa kama anataka kufanya kazi afanye itaonekana tuu kwenye kumpongeza tutafanya hivyo na kwenye kumponda tutafanya hivyo daima ndo maisha yetu tuliyochagua great thinkers, we will always be one step ahead of you sizonje!
 
Kumekuwa na Kasumba ya serikali yetu kila tatizo likitutokea huwa wanasema hata mataifa mengine makubwa nayo wana matatizo kama yetu,sasa Mbona USA wana uhuru mkubwa wa kujieleza mbona na sie hatuigi? Obama,Bush wanatukanwa kweupe na hakuna kumbuguzi mtoa maoni ila TZ usitoe maoni yanayokosoa SIRIKALI.

Kitendo cha Polisi kumakamata Maxence Melo wakati kuna kesi ya msingi ipo mahakani ni kinyume cha katiba ya nchi,Nawaomba Jeshi la Polisi wazingatie taratibu tulizoziweka,Mahakama ndio chombo cha kutoa tafsiri ya sheria...Unaomba Data za Mteja wa JF wewe kama nani? kama Polisi unataka kwa sababu zipi na wamevunja vifungu vipi?

Maxence na Uongozi wa JF Endeleeni Kukaza uzi,Kumkamata mtu kwa kutumia laptop ni ngumu sana maana IP ni Dynamic na pia kuna Apps za kufake IP,Kuna Proxy sites kibao.
 
Vipi wamiliki wa Facebook na Instagram wameshatiwa nguvuni na Polisi?
 
Kwa mwendo huu wa ngosha lazima tutazima data kwa mwaka mmoja pasipo malaika kushuka
 
Nipo likizo ...nitaenda mahakamani kumpa kampani kamanda Maxence Melo...
 
Tatizo la hawa walinda amani wetu, wao hutumia nguvu kuliko kufuata sheria.
Mbona wale wa marekani wa Apple, walikataa kushirikiana na FBI lkn hakuna hata waliowekwa ndani
Nchi za kiafrika za kijinga sana. Wao kila kitu wanakuruzinzalize.
 

Hiyo namba tatu umeisisitiza japo sijaielewa naomba ufafanuzi
 
ushauri mzuri
 
Sizonje mtu wa ajabu kabisa kama anataka kufanya kazi afanye itaonekana tuu kwenye kumpongeza tutafanya hivyo na kwenye kumponda tutafanya hivyo daima ndo maisha yetu tuliyochagua great thinkers, we will always be one step ahead of you sizonje!
Utawala huu ni wa ajabu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…