Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Hiyo namba tatu umeisisitiza japo sijaielewa naomba ufafanuzi
Vpn=virtual private network

Mfano saizi umejiunga kifurushi cha tigo sasa isp=internet service provider wako ambaye ni tigo anakupa IP address na anaku monitor kila step unayofanya

Sasa VPN unatumia private network mfano network ipo uholanzi,Romania au popote pale sasa Ww utadownload VPN kwenye site yake kisha utalipa kiasi cha pesa aidha kwa mwezi au mwaka huyu anakupa IP address yake yy,ya server yake mtu yeyote akikutafuta anakutana na IP ya server ya VPN yako kama yupo Romania basi itaonyesha Ww upo Romania huyu mwenye server IP yko anaificha ..

VPN -virtual private network

Raha ya kusoma BCS ndio hii
 
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi anaitwa Mwigulu Nchemba , huyu ndiye kiongozi wa jeshi la polisi katika nchi hii , chochote kinachofanywa na polisi ama amekiagiza yeye mwenyewe kifanyike , ama anakijua na amekikubali kifanyike .

Huyu pia ni member wa JAMIIFORUMS , bahati iliyoje kwa JF kuwa na mwanachama ambaye ni kiongozi mkubwa wa serikali ! Lakini katika uongozi wake huo ndipo kiongozi wa JF anakamatwa na kunyimwa dhamana , kwamba katika kipindi ambacho Mwigulu , ambaye pia ni mwandishi wa jf , mchambuzi , mfafanuzi , mtetezi wa ccm na mwanzisha nyuzi ( juzi juzi kaweka uzi wa wachina na vitambulisho feki , aliowagumia Airport ) ni Waziri , Maxence anateswa !

Hakika kikulacho umekivaa .


Ndiyo tatizo la Sheria hilo, halina Urafiki wala undugu, sheria ikishapitishwa kinachofwatia ni utekelezaji tu!
 
Haya ndiyo tuliyoyachagua wenyewe mwaka jana.
Tuipe serikali nafasi ifanye yale inayoona yatafaa kwa watanzania waliopiga kura mwaka jana na kuichagua CCM .
Wazungu sio wajinga wanapobadilisha vyama vya siasa na sera zake kila baada ya muda. Sisi tunafanya vyama kuwa ni kama dini.
Kosa kubwa watanzania walilofanya ni kuipa serikali ya CCM wabunge wengi kupita kiasi. Kuna majimbo waliacha kuchagua wabunge wa vyama vingine na kuendelea kuwang' ang'ania wabu ge wa CCM waliotawala mika nenda rudi kwa kutegemea mambo mapya kwa watu wale wale.

Sasa CCM imeendelea kuwepo madarakani na imeamua kuminya uhuru wa habari na uhuru wa kisiasa inabidi tuiunge mkono pia mana haya yote waliyaleta wao na wanaona kuwa yatawaondoa na mwaka jana walinusurika kuondoka; sitegemei ccm iendelee kufanya kosa la kuruhusu uhuru uliotaka kuwaondoa.
Cha msingi ni watanzania kujitambua kuwa wao ni binadamu wanahitaji nini.
Uhuru wa habari hauwezi kuondoa amani. Ingekua hivyo nchi za magharibi zingekuwa na vita na zile za Afrika na asia wangekua na amani ya kupindukia.
Watanzania tusiilaumu serikali ya CCM mana inatekeleza sera zake na majukumu yake. Ni wakati wa kuisoma namba.
Vyombo vya habari huwa ni vizuri sana kwa mtu anayesimamia haki na kuwa muwazi lakini kwa wezi na wapiga dili ni hatari sana. Sasa sielewi nani anayekwazwa na uhuru wa vyombo vya habari. Inaonekana bado kuna masalia ya wapiga dili waliojivika ngozi ya kondoo.
 
Melo yuko salama..wala hakuna jambo jipya kaitwa kuhojiwa tuu.
Lakini walio sababisha kuitwa kuhojiwa ni wale waleta habari za uzushi ambazo serikali inalazimika kuhangaika kuzikanusha kila leo...
sheria ile ya mitandao ina ipa mamlaka polisi kupata taarifa za mtu kutoka kwa mtu na inawezekana hata kuchukua vifaa husika...
Melo yuko salama salimini.
Ahsante Kiongozi.

Kama ni hivyo, basi ni Habari njema.

Tunashukuru kwa kutujuza
 
Safari imewiva
huashan6.jpg
 
Ni mwendo wa kinyonga sasa ni kama gari iliyopata shida kwenye mfumo wake wa mwendo linachechemea....! Wengi wetu wamevuta handbrake, wanaingia huku siasani kwa kuchungulia...Ni kama vile forum ya siasa imepata kitu kama semi paralysis...!
Tusiogope lakini tusidhihaki...yanayotokea sasa inabidi yatokee ni mfumo wa kiasili kabisa kwenye hatua za maisha ni lazima kuwe na changamoto...! Changamoto hukufanya uwe imara zaidi! Changamoto hukuongezea imani hekima na busara pia, changamoto hukuumba kuwa kiumbe mpya mwenye mitazamo mikuu zaidi
Tafakuri! utulivu wa akili! kunena na kuamua kwa weledi, huku ukipanga kwa utulivu na kuvumilia maumivu yenye kuumiza sana daima huleta ukombozi na ushindi
Tushikamane katika kipindi hiki tuwe wamoja tusiachane lakini muhimu kuliko yote tusidhihaki wala kubeza...we are great thinkers
Wakati si milele....! Tuombeane
 
Unguvu ni moja Udhaifu ni utengano...
Ukiona mlango mmoja unataka kufungwa kuna mengine iliyo wazi tupite safari iendeleee...
 
Subiri kwanza serikali imalizane na wazushi,sio kila siku serikali iwe na kazi ya kukanusha uzushi
 
[HASHTAG]#Great[/HASHTAG] JF, [HASHTAG]Free[/HASHTAG] [HASHTAG]Max[/HASHTAG]
Ni wakati wa kuonesha Nguvu yetu, JF haijawahi kushindwaa.

[HASHTAG]#Hatushindwiiiii[/HASHTAG]!!!.
 
Back
Top Bottom