Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Hapa kilicho baki Ni kuzima JF Haraka iwezekanavyo.......
 
Pamoja na kuwa rushwa ilikuwa ni kubwa katika serikali iliyopita lakini mitandao ya kijamii na uhuru wa kujieleza ulisaidia sana. Hebu imagine kama tungekuwa tumefungwa midomo, yaani jamaa wangepiga hela kanini. sasa tuendako serikali ya kuendeshea gizani, sijui itakuwaje.
 
Bora mmempa ban mpeni ya mwezi mzima maana saa hizi tuna hasira NA wao wanaleta maneno ya ajabu ajabu humu bora apumzike NA Sisi tuheme kheeee
 
Sasa unataka tuwe tunasfia tu? Hapa ilibidi polisi iseme inamtafuta nani na kwa makosa gani lkn wao wanachota ni kuwajua wachangiaji wote ktk jamii forum na kumonitor mijadara yote na kuamua mada gani iwekwe na kujadiliwa. Tupinge kwa nguvu zote
 
Kama ni kwel kwamba wamemkamata kwa sababu za kushindwa kutoa siri za jf... Basi interijensia yote inapaswa kuacha kazi...
.
Maana kwa dunia ya sasa ni rahisi muno, hata ukimchukua mtt Wa kichina mwaka Wa kwanza anafanya..

Kuwen wabunifu, ila kama ni tatzo jingine mmmhh....
 
Nimewaza tu. Hivi juzi si ndo wameenda ofisini kuchukua baadhi ya nakala alizo lipia kodi?. Hawa jamaa sio wazuri na wanaweza kuja na option ya kwamba jamii forum ilikuwa hailipi kodi hivo inavujwa au wakaja na zengwe lolote lile. Nawaza tu jinsi itakavo kuwa jamii forum isipo kuwepo. Tumejifunza mengi sana pengine na wengi wetu hapa ilikuwa ni kama kibuludisho na pengine sehemu ya kutolea stress

Serikali ituache na uhuru wetu kwanini wanataka kutuziba midomo. Lazima kuna uozo unakuja wanahofua aibu watakayo ipata sio bure
 
Jamani huku sasa tunakokwenda kumezidi[emoji22][emoji22]..Max wewe ni shujaa,wanasema dhahabu ukiichoma moto ndiyo inazidi kung'aa...usigive Up..kaza mpaka mwisho Max
 
Si mamlaka zote zinatoka kwa Mungu... Mfano idi Amin dadaa unataka kusema mamlaka yake yalitoka kwa Mungu??
 
Nchi inatakiwa kuwa chini ya katiba na sio serikali. Ni udikteta nchi kuwa chniya serikali. Uhuru wa maoni ni maoni aina zote. Mazurj na mabaya
Acha kutaka kuliweka taifa gizanj. Maoni mazuri kwa polisi ni mabaya kwa mwizi ndiyo ukweli. Hakuna mwenye kipimo cha kupimia maoni mazuri au mabaya kwa kuwa uzuri au ubaya wa maoni ni subjective Mkuu
 
Wewe ni rahisi kusema hivyo kwa sababu upo upande huo wa uovu
 
Huyu bwana hatoki. Kuna gepu ya katiba inakuja soon.
 
Shairi kwa Max

[HASHTAG]#FreeMaxenceMelo[/HASHTAG]

Nimekuja mara moja kuonesha mshikamano kwa heshima ya Max.

Max Melo yupo selo, wengi twaona kero
Kashikwa na makachero, sheria za lelolelo
Pasi dhamana jero, ya katiba kapelo
Kwa wengi shujaa hero, hasi mfalme Nero

Max si mhalifu, kijana muadilifu
Ukumbi yakinifu, kuweka ubadilifu
Watu watoe kifu, pia hata kusifu
Kwa wengi shujaa hero, hasi mfalme Nero

Max alikataa, habari za hadaa
Majina kuwafaa, kwake kubwa fadhaa
Kanuni za nakaa, muhuri ushakaa
Kwa wengi shujaa hero, hasi mfalme Nero

Kiranga ka nabii, haya aliyaona
Akafanya utii, kaenguka kuonya
Ukumbi namna hii, tutakosa kunyonya
Kwa wengi shujaa hero, hasi mfalme Nero

Basi nduguzanguni, tuzidi shikamana
Walio uzunguni, hadi kwetu kwa mama
Tulio uvunguni, kazi bila lawama
Kwa wengi shujaa hero, hasi mfalme Nero
 

Good to have you back!
Please stay
 
Badili msimamo wako kiranga mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…