Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Hayo yakwako
Mada hapa ni Sheria ya mitandao ilipitishwa kabla ya Magufuli kuwa Rais

Kosa lake ni lipi?
Mkuu wewe ndiyo umeonesha kua anaheshimu uwepo wa hilo bunge.

Akiwa kama rais na anajua kua katiba yetu inaheshimu faragha ya mtu si angeanzisha muswada wa dharura kupinga hiyo sheria iliyopitishwa mwanzo?
Tufanye hana muda, ameshindwa hata kusapoti raia ambao walisimama mahakamani kutetea faragha ya wananchi.

Baada ya hapo tukasikia milioni kumi zimegewa kwa wabunge ili muswada wa kuendelea kubana uhuru wa vyombo vya habari upitishwe, hajaongelea hilo la wabunge wa chama husika kupewa pesa na muswada akasema atausaini.

Ushaona kosa lake?
 
Niliwahi kusema jf hii
Kuna watu wanavuka mipaka
Sasa mzigo anabebeshwa Kipenzi chetu jf !!!.
Wewe ukoje? Badala ya kumlaumu anayemkatamata watu bila hatia wewe unawalaumu watoa maoni. Mimi nachukia sana watu kuitwa v.i.l.a.z.a lakini wanaoita hivo wenzao wanachukuliwa hatua gani?
 
Tanzania hii hakuna uhuru wa vyombo vya habari. Naona Serikali inataka kuua huu mtandao.
 
Tumesoma Terms & Conditions za JF? Privacy Policy je? Kama Polisi walifuata taratibu kwa kupata kibali cha mahakama kuomba taarifa binafsi kutoka kwa mmiliki wa JF, basi alitakiwa atoe, otherwise ni ubabe wa polisi na mmiliki wa JF yuko sahihi kukataa kutoa taarifa hizo

Lameck Madelu naye ameumizwa sana na thread humu, hapa kesi zitakuwa ni uchochezi tu.

Hivi awamu hii ndiyo kuna uchochezi sana?
 
Nawaza!..... atakuwa amegoma kutoa taarifa za yule mama kichaa alie mpakazia mkulu kuhusu sababu za mama mkuu kulazwa na kifo cha bintie.. hataka kama ni mimi ningehakikisha yule mama namtia adabu kwa uzushi ule!

Mawazo yangu sio msimamo wako.
 
Kila la kheri katika utafitaji wao ,watu wapo busy kusaka pesa wengine wapo busy kawasaka watu JF.
Ila Tanzania itaendelea kulaaniwa hadi mwisho kama haitabadilika katika uongozi.

Uzuri wa Dunia hii ni kwamba hakuna kiumbe atakae ishi milele leo wewe ni polisi kesho ukiondoka mwanao hujui atakuwa nani na hujui familia yako itakuwa wapi.

Haki huwa ni kama sumaku inavuta watu wenye haki hata kama wako mbali na siku wadai haki wakijua maana ya haki hakuna atakae wazuia kwa maana mioyo yao itakuwa imejaa maumivu. IPO SIKU YAJA.

RAPHAEL WA URENO......nikija Tanzania kama nitamaliza mapema shughuli zangu nitaripoti kituo cha polisi kuwapa jina langu.
 
Kuna uzi humu ulisema wazi na ushahidi kuwa Makamu wa rais amejiuzulu.

Kuna uzi humu ulipost barua ya ikulu ikionyesha nembo ya ikulu na sahihi ya msemaji wa ikulu ikielezea kutenguliwa kwa mrisho gambo. Huo sio uchochezi ? Au uchochezi kwako ni mpaka watu washike bunduki
Makamu akijiuzulu watu wanaingia mitaani kufanya fujo?
Soma hii uone kama kusema amejuizulu kunaleta shida:
Whoever, by words, either spoken or written, or by signs, or by visible representation, or otherwise, brings or attempts to bring into hatred or contempt, or excites or attempts to excite disaffection towards,
 
Huu Ni uchochezi totally......unataka kupeperusha ndege wa watu mkuu!
 
Back
Top Bottom