Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

"Thinking is strictly prohibited" ...nalikumbuka sana hili shairi la Prof. Baregu.
 
Kujifikilia wewe na familia yako ni mawazo ya kijinga na dunia hii isingekus hivi. Hivi kama nyerere angeifikilia kwanza familia yake Leo tungekuwa hapa?

Huo ndio ukweli inasikitisha lkn ndiyo hivyo wote ninyi akiwahitaji kesho hamtakuwepo!
 
Ndugu Watanzania tuendelee kupost tu kile tunachoamini tunataka watu wajue. Kumkamata Melo hawawezi kushindwa hata kama anadhibiti posts za watu. Si wanaweza hata kujitungia habari na kisha kutuma then wanakuja wanamtafuta mmiliki wa Forum?

Historia inatufundisha kuwa ukiona mwenzako anakandamizwa sema, manake hujui akiwamaliza wapinzani nani atafuata. Walianza kwenye vyama pinzani tukakaa kimya then wanakuja kwetu.

Ngoja tuisome numerali
 
Hizo taarifa baada kugundulika ni feki si zilifutwa? Tatizo liko wapi?

Kwa style hiyo basi gerezani watu wangeisha. Kwakuwa mtu kakuibia na mali zako ukazipata basi hakuna haja ya kesi.

Hapo haitafutwi JF na ndio maana hawakumkamata mello kwa kosa la uchochezi. Kwa nilivyoelewa Wao wanataka details za mtu aliyepost hizo taarifa. Aseme sahihi ya msemaji wa ikulu kaitoa wapi?
 
Mwigulu Nchemba ni member wa JF, pia Mwigulu Nchemba ndio boss wa Jeshi la Polisi na pia tuhuma za kughushi boss huyu ziliandikwa humu JF kisha boss huyu akaja na kanusho/utetezi usioingia akilini pa wengi, je kuna nini hapa?

Naomba jopo la mawakili wasomi liundwe mara moja tuwekewe account number tutatowa pesa kuliko zile tunazochangia harusi na hakika wale wanaounderestimate power of JF watapata clear message.

Itakuwa ni aibu kwetu na nitajitowa rasmi JF kama Max atafikishwa mahakamani akiwa anatetewa na mawakili wasomi chini ya 10.

Na nyinyi mawakili mliopo humu muache kuendekeza njaa hizi ndio kesi za kuvolunteer kujenga credibility na legacy yenu kwa jamii.

Mods sasa anzeni kukusanya thread zote za wanaomtukana Lowasa humu, na wanaomtukana Nyerere wakiongozwa na Faiza Foxy ili tuelewane vizuri mbeleni.
 
Magu hausiki hapa
Sheria ya mitandao imepitishwa ns bunge Magu si Rais
Hilo mlifahamu,
Watu wanapost habari za uzushi bila kuangalia athali zake kwa jamii.

Hii inaleta maana kuwa
Unapo leta uzushi ujue sheria IPO
Uwe tayali kukabiriana na sheria husika.
Kama ni uzushi si zinapuuzwa tu. Mbona hawa mawaziri wake wanatoa taarifa za uzushi tunawapuuza?
 
Hivi yule aliyefoji amri ya mahakama umeya kinondoni. Alifanywa nini
Na yeye ni mmoja wapo wa hao wanaotafutwa. Sababu hiyo habari na yenyewe iliwekwa humu so polisi wakishapata hizo details zao ndio tutajua watakachofanywa
 
Pole sana kaka Max. Naamini kuwa jambo hili litaenda salama
 
ndugu yangu sio utani tunapoelekea kubaya sana maana maisha magumu na kuongea tunachaguliwa maneno ya kuongea,yaani ni sawa na mtu aliyekuzidi nguvu anakufinya na kukupiga halafu anakuzuia kulia wala hata kusema "yalaaaaaaaaa".Yani we uwe kimya tu na uendelee kuumia
nini kifanyike sasa maana watanzania hawana hata dalili za kujiongeza, inaumiza
 
Wakuu naomba nijuzwe namna ya kupata hifadhi ubalozini ili usishtakiwe na nchi yako kama alivyofanya Julian Asange wa wikileaks?

Asange alikuwa akipata taarifa alizochapisha toka kwenye nchi alikokimbilia kujificha.Walikuwa wabia wake wa miaka mingi kwenye mtandao wa weakleaks.Hakukimbilia walimchukua wenyewe.Ile kusema alikimbilia ubalozini ni geresha tu.
 
View attachment 445691

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Kosa ni kuwanyima Polisi taarifa binafsi za wateja wa mtandao wa JamiiForums zilipohitajika. Maxence ameendelea kushikilia msimamo kuwa ni uvunjwaji wa sheria na haki za wananchi kufanya hivyo.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.

Pole Mkuu yamewakuta wengi si wewe peke yako. Watu wanauona mtandao huu unawaharibia ulwa wanataka ufungwe au watu waukimbie .
 
Mwigulu Nchemba ni member wa JF, pia Mwigulu Nchemba ndio boss wa Jeshi la Polisi na pia tuhuma za kughushi boss huyu ziliandikwa humu JF kisha boss huyu akaja na kanusho/utetezi usioingia akilini pa wengi, je kuna nini hapa?

Naomba jopo la mawakili wasomi liundwe mara moja tuwekewe account number tutatowa pesa kuliko zile tunazochangia harusi na hakika wale wanaounderestimate power of JF watapata clear message.

Itakuwa ni aibu kwetu na nitajitowa rasmi JF kama Max atafikishwa mahakamani akiwa anatetewa na mawakili wasomi chini ya 10.

Na nyinyi mawakili mliopo humu muache kuendekeza njaa hizi ndio kesi za kuvolunteer kujenga credibility na legacy yenu kwa jamii.

Mods sasa anzeni kukusanya thread zote za wanaomtukana Lowasa humu, na wanaomtukana Nyerere wakiongozwa na Faiza Foxy ili tuelewane vizuri mbeleni.
well said mkuu!
 
Bila shaka serikali inabidi itoe muongozo kwa wananchi mambo yafuatayo
1.Maneno ya kuongea
2.Maneno ya kuandika
3.Maneno ya kufikiria n.a. kipi cha kufikiria
4.Maneno ya kuipongeza serikali
 
Back
Top Bottom