Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana

Humu ndani hata watu wakitoa lugha chafu mnasema freedom of speech.

Tutofautishe kuropoka na Freedom of speech.
Hata kama wameropoka ni kifungu gani cha Sheria Kilichosema Waropokaji wakamatwe?

Rais yyt anaweza kutukanwa, akakshfiwa na akasemwa kwa kebehi vile vile.
Hayo ni mambo ya kawaida ktk NCHI ZOTE ZENYE DEMOKRASIA YA KWELI.
Tazama Obama na Marais wote w Ulaya. Wanachorwa mpk Wamevaa vichupi tu.
Wanatukanwa na Kukebehiwa kila siku. Nani umeskia Kakamatwa?

Ingia Face book, Twitter and so on uone matusi wanayotukanwa Viongozi wa Nchi za wenzetu. Umeshawahi kusikia Wamekamatwa.?

Magufuli anatawala Nchi KIBEBERU.
Wakati wa Mzee wetu Kikwete Watu walikuwa wanasema wapendavyo.

Na Mzee wa Watu wala habari hana.
Leo KIKWETE anakumbukwa.
Na Huyu Magufuli Pia atapita tu.

Hizi ni Jazba za kisukuma.
Zina mwisho wake.

Walitokea kina King Arthur and Ferrous walitawala EMPIRE wacha nchi ndogo km Tz. Leo hii WAKO WAPI?
Kwisha maneno yao.
Hata mifupa yao Hakuna.
 
Nashauri tu wana jamii forum nasi tuwe makini na maon yetu kwenye hoja mbali mbali, mambo mengine Mungu atatupa wepesi tu jamani si kila siku kulumbana na serikali matokeo yake ndio tunawaweka sehemu mbaya wenzetu, pole mr melo huwa hayeendelei daima
 
1481691170620.png
 
View attachment 445795
Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo, ameitwa na baadaye kuwekwa ndani, Central Police.

Polisi wanaeleza muda huu kwamba leo atalala ndani hadi kesho atakapofikishwa mahakamani.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi namba 9 ya mwaka 2016 dhidi ya Jamii Media dhidi ya polisi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.

=====================

MKURUGENZI Mtendaji wa Jamii Media na mwanzilishi wa mtandao maarufu wa JamiiForums, anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo kuu cha polisi, Dar es Salaam, kwa madai ya kugomea agizo la muda mrefu la jeshi hilo.

Polisi wamekuwa wakiagiza na kuamuru kupewa taarifa za watumiaji wa JamiiForums bila mafanikio.

Maxence alipigiwa simu leo akiwa ofisini kwake asubuhi akitakiwa kufika kituoni hapo na alitekeleza mwito huo.

Baada ya kufika polisi kati, akiwa ameongozana na mhariri na mwanaharakati wa uhuru wa mawasiliano, Simon Mkina na mwanasheria, Nakazael Tenga, Maxence alinyimwa dhamana ya polisi.

Jeshi la Polisi limeeleza kuwa Maxence atafikishwa makahamani kesho asubuhi kujibu mashitaka ya kuzuia upelelezi wa polisi dhidi ya makosa ya mtandao.

JamiiForums imekuwa na msimamo wa kutotoa habari za wachangiaji wake kwa yeyote, kwani kufanya hivyo ni kuingialia uhuru na faragha ya wateja wake.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006, msingi mkuu wa mtandao wa JamiiForums umekuwa kulinda faragha ya watumiaji wake.

Watumiaji wa mtandao wa JamiiForums wako huru kuweka mijadala, kuanzisha mijadala, kuchangia chochote pasipo kuvunja sheria za nchi au kuhatarisha usalama wa taifa.

Kampuni ya Jamii Media, inayoendesha mitandao ya JamiiForums.com na FikraPevu.com imejijengea heshima na umaarufu kwa muda mrefu kutokana na namna inavyoendesha na kusimamia shughuli zake ambazo kwa kiwango kikubwa ni za kimtandao.

Mtandao wa JamiiForums ni mtandao mkubwa wa Kiswahili kwa Afrika Mashariki na duniani ukiwa na wasomaji wasiopungua Milioni 2.5 kwa mwezi ambapo kwa mwaka 2016, mtandao huu unatimiza rasmi miaka 10 tangu uanzishwe.

Mtandao huu unasifika kwa kutoa fursa ya kipekee kwa watumiaji wake kutoa yaliyo mioyoni mwao huku wengine wakijifunza mbinu kadha wa kadha za kijasiriamali, afya, elimu na hata kuibuka wanasiasa wapya waliofundwa na wanajumuia ya JamiiForums.

Pamoja na kuendelea kutoa huduma hata katika nyakati ngumu, mtandao wa JamiiForums unakumbana mara kwa mara na changamoto nyingi zinazosababisha waanzilishi na waendeshaji wake kuwa katika misukosuko mara kwa mara, hasa na polisi.

Kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, Jeshi la Polisi limekuwa likiushinikiza mtandao wa JamiiForums (kwa njia ya barua rasmi) kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake.

JamiiForums katika kuhakikisha inasimamia usiri wa wateja wake, imekuwa ikihoji shinikizo kutoka Polisi yanazingatia sheria gani na kutaka kujua ni vifungu gani vya sheria ambavyo wadau wa mtandao huo wamevivunja bila kupewa maelezo yanayoridhisha zaidi ya kuelezwa kuwa hatua zaidi zitachukuliwa kama ushirikiano hautatolewa kwa Jeshi la Polisi.

Tayari Jamii Media imefungua kesi Mahakama Kuu ya Tanzania (Kesi namba 9 ya mwaka 2016); kutaka Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 32 na 38 viangaliwe upya kwa kuwa vinapelekea kuvunjwa kwa haki za msingi za watanzania watumiao mitandao ili kulinda maslahi ya umma kwa kuzingatia vifungu 26(2) na 30(3) vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.




Baada ya kufungua kesi hiyo Serikali, kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliweka mapingamizi sita ikitaka kesi nzima ifutwe na Jamii Media walipe gharama zilizoingiwa.

Lakini mnamo tarehe 4, Agosti 2016 Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kuzipitia hoja zilizowasilishwa na Serikali na Wanasheria wa Jamii Media iliamua kuwa mapingamizi yote sita ya Serikali hayana mashiko na hivyo kesi ya msingi itaendelea kusikilizwa.

Maxence Melo anakamatwa huku kukiwa na Kesi hiyo ya Kikatiba dhidi ya taarifa ambazo Jeshi la Polisi wanazitaka, kesi ambayo mahakama kuu itatolea hukumu, tarehe 20 Februari.

Chanzo: FikraPevu

ha asante melo endelea kutulinda
 
JF ina rensponsibility kubwa sana, kama vivlivyo vyombo vingine vya Habari, kuna mambo mengi ya uongo na uzushi huletwa humu na kuachwa, ikumbukwe kwamba nchi nyingi kama Kenya, Rwanda, Burundi n.k Vita ililetwa na Vyombo vya Habari kama redio na TV, hivyo JF ina jukumu la kulinda amani ya nchi, kama ni kweli amekamatwa, na kama siyo kweli basi wajifunze na wabadilike, watambue jukumu lao kwenye Jamii!

CEO wa JF asipumbazwe na watu wanaosapoti kwenda kinyume na Serikali hapa, wengi wao wana maisha yao na wala hawaishi TZ, na JF ikifa kesho, au ofisi ya JF kunyimwa kibali cha kufanya kazi TZ hawana cha kupoteza, zaidi ya kuhamia kwenye mtandao mwingine na kuendeleza wanayoyafanya, hivyo angalia maisha yako na familia yako, fanya lililo sahihi na jinsi Serikali inavyokutaka kwani mwisho wa siku Serikali ndiyo yenye nchi, watakushauri wanachama wa JF wanavyotaka lkn Serikali ndiyo wasimamizi wa hii nchi!
Acha ubinafsi wewe na usitake kudanganya kwamba vita inaletwa na kuruhusu watu kutoa maoni yao kwenye media. nyakati hizo zimekwisha na kuongoza kizazi cha sasa kunahitaji kutumia akili zaidi kuliko nguvu za misuli
 
  • Thanks
Reactions: J C
while there is already a pending case at the high court, a criminal case has been instituted.

forum shopping at its pinnacle
 
Alafu kila siku eti 'mniombee'.
Ili aendelee kutufanyia mambo ya ajabu ajabu, sawa tutakuombea, ila hilo ombi........
ha ha limekufika hapa! kumbe nawewe huwa unabwabwaja!
 
Kwenye hili la Uhuru wa kujieleza namkumbuka sana Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete
 
Mmmmh, hii ngoma nzuri, kichaka kimevamiwa. Kwa sasa bora kuwa msomaji tu kilichoandikwa
 
Unataka kutuambia nini Mkuu ? Unawaweka watu kwenye mtego eeh ?

Ngoja niende kule kwenye mapenzi japo sie wengine tuna nyota za punda mpaka tubebeshwe mzigo ndio tule
MMU naomba mnipokee
Karibu MMU... Huku tunaingiaga kwa machale tukihitaji stress ndo tunakuja wengine
 
Vpn=virtual private network

Mfano saizi umejiunga kifurushi cha tigo sasa isp=internet service provider wako ambaye ni tigo anakupa IP address na anaku monitor kila step unayofanya

Sasa VPN unatumia private network mfano network ipo uholanzi,Romania au popote pale sasa Ww utadownload VPN kwenye site yake kisha utalipa kiasi cha pesa aidha kwa mwezi au mwaka huyu anakupa IP address yake yy,ya server yake mtu yeyote akikutafuta anakutana na IP ya server ya VPN yako kama yupo Romania basi itaonyesha Ww upo Romania huyu mwenye server IP yko anaificha ..

VPN -virtual private network

Raha ya kusoma BCS ndio hii
Sasa gharama ya hiyo VPN ikoje kwamfano?
 
Kuna sheria gani inaruhusu kuingilia faragha ya mtu
 
jamani niliimisi sana Jf,imenisaidia vitu vingi sanaaaa ambavyo nlikua busy navyo hadi nikapotea humu jukwaani.
habari hii imenishitua sanaaaa........
ni mwendo wa kuzidisha maombi tu,haya yote yatakwisha.....
 
Back
Top Bottom