Mkurugenzi PSSSF kikaangoni kwa kujikopesha fedha ya kujinunulia gari

Mkurugenzi PSSSF kikaangoni kwa kujikopesha fedha ya kujinunulia gari

Kwa nn wasikope bank? Ni ajabu sana hili kufanyika. Hata NHIF Hali ipo hivi, watu wanajikopesha pesa bila riba na unafanyika ujanja mkopo haulipwi.

Waweke kanuni mfuko hautoi mikopo kwa wafanyakazi, anayetaka kukopa aende bank Kama wanavyofanya watumishi wengine
Kwani hawarudishi?
Hio ndio ingekua shida

Revolving Fund zipo hata huku Sekta binafsi
 
Dodoma. Baraza la Maadili la Taifa lilimweka kikaangoni Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugani wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Ernest Khisombi kwa kutumia vibaya Sh193.9 milioni.

Kiasi hicho kinajumuisha Sh117.88 milioni alizokopeshwa kinyume na utaratibu wa sera ya mikopo ya PSSSF ili anunue gari binafsi na Sh76 milioni alizolipiwa kodi ya kuliingiza nchini gari hilo.

Sera ya mikopo na fedha ya PSSSF inaruhusu baadhi ya watumishi kukopa fedha za kununulia magari na mfuko kuwalipia kodi, hata hivyo, sera hiyo inataja kuwa kodi hiyo italipwa ikiwa gari ni jipya lisilowahi kutembea.

Khisombi amepelekwa hapo akidaiwa kutumia vibaya madaraka yake na kukiuka maadili ya utumishi huku akijua ni kosa.

Shahidi katika kesi hiyo, Gidioni Mafwili akiongozwa na Wakili wa Serikali Hassan Mayunga mbele ya mwenyekiti wa baraza hilo, Jaji Ibrahim Mipawa alisema mshtakiwa alilipwa fedha hizo kwa ridhaa ya kamati ya mikopo ambayo yeye ni mjumbe.

Mafwili alisema baada ya fedha hizo kutolewa, hundi iliandikwa na kupelekwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kulilipia gari hilo.

“Utaratibu uliotumika kwa yeye kujikopesha haukuzingatia sera yao na maadili ya utumishi, lakini kitendo cha kulipiwa kodi kwa gari ambalo limetembea kilomita nyingi haikuwa sahihi, alipaswa kulipiwa kwenye gari ambalo halijatembelea hata kilomita moja,” alisema Mafwili akinukuu sera ya mikopo ya PSSSF ya mwaka 2018.

Kingine kilichowatia hofu ni mfanano wa chesesi za magari yake kati ya lililolipiwa kodi lenye namba T884 DWP likiwa na chesesi TRJ1500096060 na jingine la zamani analolimiki.

Wakili Mayunga alihoji iweje mkopo huo uidhinishwe na kupitishwa haraka bila kufuata utaratibu na mhusika kushiriki vikao vya kuupitisha mkopo huo.

Baada ya maelezo ya ushahidi, Khisombi alikana tuhuma alizosomewa. Akiongozwa na wakili wake Daniel Weluwelu, alisema utaratibu wa yeye kukopa na kununua gari ulifuatwa na hakuna mahali alipovunja sheria.

Alisema ni haki yake kwa ngazi aliyofikia kulipiwa kodi ya gari analonunua na si jambo geni.

Kuhusu kulipiwa kodi kwa gari lililotumika, alisema sera ya PSSSF ilibadilishwa Mei 2021 na kuruhusu hata kwa magari yaliyotumika ingawa tayari yeye alishachukua mkopo huo kipindi hicho.
Urefu wa kamba yake unamruhusu, sioni kama Kuna jipya
 
Kingine kilichowatia hofu ni mfanano wa chesesi za magari yake kati ya lililolipiwa kodi lenye namba T884 DWP likiwa na chesesi TRJ1500096060 na jingine la zamani analolimiki.[emoji3064]

Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
ver
Hawa jamaa wana roho mbaya sana. Hizo hela wanazojikopesha ni za wazee wetu wastaafu, na pia ni za mirathi! Haiwezekani wanufaika wasotee mafao yao kwa miaka mingi, huku fedha zao zikitumika kununulia magari ya watu binafsi! Huu ni uonevu usio vumilika...
Inasikitish sana, kuna watu wanastaafu wanakaa zaid ya miaka miwili bila mafao ambayo hayazidi hata 100m wakati kuna walamba asali wanakopeshana mpaka 100m na ushehe na kodi za mamilioni wanalipiwa. shame
 
Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Ernest Khisombi Septemba 12, 2022amefikishwa mbele ya Baraza la Maadili kwa tuhuma za kujipatia mkopo wa gari binafsi wenye thamani ya Shilingi 196,570,931.00 kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

Akisoma mashtaka mbele ya Baraza la Maadili, Wakili wa Serikali Bw. Hassan Mayunga ameliambia Baraza kuwa, mtuhumiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kukopa fedha za mfuko kiasi cha shilingi 117,808,470.00 bila kufuata utaratibu.

Katika lalamiko hilo Na. 5 la mwaka 2022, kosa la pili ni kulipiwa kodi kiasi cha shilingi 78,762,461.00 bila kufuata utaratibu wa Sera ya Mikopo ya PSSSF.

Kwa mujibu wa Bw. Mayunga, kitendo hicho kinamfanya Bw. Khisombi ambaye ni Kiongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kushidwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) na (b) na hivyo kukiuka maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu cha 6(2) cha Sharia ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hata hivyo, Bw. Khisombi amezikana tuhuma hizo na kulieleza Baraza la Maadili kuwa, “fedha hizi ni ihaki yangu kama Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi kwa mujibu wa Sera ya Mikopo ya Mfuko.”

Shahidi wa mlalamikaji Bw. Gideon Mafwiri ameliambia Baraza kuwa kiongozi huyo alijipatia mkopo kinyume na utaratibu uliowekwa na mfuko wa mikopo wa PSSF.

Mfuko wa mikopo umeweka utaratibu wa ni viongozi wapi wanastahili kulipiwa kodi na mfuko nan i gali la namna gani litalipiwa kodi na mfuko kwa mujibu wa taratibu,” alisema.

Kwa mujibu wa maelezo ya shahidi, utaratibu wa Mfuko ni kuwa maombi ya mkopo yaidhinishwe na Kamati ya Mkopo ya Mfuko, mkopaji kulipia asilimia 5 ya mkopo kabla hajapatiwa mkopo pamoja na kulipiwa kodi gari jipya la kiongozi kwa asilimia 100.

“Sera ya mikopo ukurasa wa 10 inasema mkopo huo outalipiwa asilimia 5 kabla mkopaji hajapatiwa. Utaratibu huu haukufuatwa,” amesema.

Bw. Mafwiri ameeleza kuwa wakati mfuko unalipia kodi ya gari la Bw. Khisombi, gari hilo halikuwa jipya kama Sera ya Mfuko huo inavyoelekeza. Ushahidi wa shauri hilo Na. 5 la mwaka 2022 umekamilika na kufungwa kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Baraza la Maadili lililoanza vikao vyake vya uchunguzi Septemba 6, 2022, limekwisha sikiliza malalamiko mengine kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongizi wa Umma dhidi ya Bw. Godfrey Chibulunje aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu katika Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Hoseah Kashimba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) na Bi. Beatrice Lupi, Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

Baraza hili linaloongozwa na jaji (Msf) Ibrahimu Mipawa na wajumbe Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi linafanya uchunguzi wa wazi kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sura 398).

Chanzo: Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
 
ver

Inasikitish sana, kuna watu wanastaafu wanakaa zaid ya miaka miwili bila mafao ambayo hayazidi hata 100m wakati kuna walamba asali wanakopeshana mpaka 100m na ushehe na kodi za mamilioni wanalipiwa. shame
Hawa watu ni wasumbufu sana wakati wa kufuatilia mafao, na pia mirathi. Unajaza fomu zote kwa ukamilifu!

Ila ukienda kwenye ofisi zao, utasumbuliwa na kuzungushwa mpaka ukome! Mara fomu hii haionekani! Mara njoo kesho! Mara njoo wiki ijayo!! Kumbe hela wanakopeshana!!

Nchi ngumu sana hii.
 
Kule Ntwara tunasema,"Cha Ntu uliwa na Ntu,Chuma pekee uliwa na kutu Somo"
Twafwaaa!
 
Mbona sisi Wakina-Njomba Nchumali tunaochangia pesa zetu kwenye mfuko hatukopeshwi!!!
 
aliyegundua GIRISI/ grease oil aliwaza sana. Vyuma vikikaza kila mmoja anatafta namna ya kuvilainishaaa
 
Back
Top Bottom