The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Hapa napoandika nimecheki statement yangu huko pssf haijawekwa makato kwa mwaka na nusu bila shaka sehemu ya hizo pesa ndio huyo mshenzi amejikopesha.Hawa jamaa wana roho mbaya sana. Hizo hela wanazojikopesha ni za wazee wetu wastaafu, na pia ni za mirathi! Haiwezekani wanufaika wasotee mafao yao kwa miaka mingi, huku fedha zao zikitumika kununulia magari ya watu binafsi! Huu ni uonevu usio vumilika.
Halafu badala ya kwenda benki kukopa, wanajikopesha wenyewe kwa wenyewe.
Nadhani huu utaratibu wa kujikopesha fedha za wastaafu na wafiwa, ungefutwa haraka iwezekanavyo. Mtu akitaka kukopa, aende benki kama wafanyavyo watumishi wengine wa Serikali.
Akikitwa na hatia afukuzwe Kazi haraka Sana na kufilisiwa.
Kuna Wazee 2 hadi sasa wamestaafu toka June hawajalipwa mafao.