Mkurugenzi PSSSF kikaangoni kwa kujikopesha fedha ya kujinunulia gari

Mkurugenzi PSSSF kikaangoni kwa kujikopesha fedha ya kujinunulia gari

Kwa nini wasiende kukopa bank kama wafanyakazi wengine? Nchi hii Kuna watu wanaishi ilhali wahusika wa kuchangia wanapigika.
Wafute hizo kanuni za kukopeshana waende bank.
 
Kwani hawarudishi?
Hio ndio ingekua shida

Revolving Fund zipo hata huku Sekta binafsi
Shida ni Kwamba lazima watatemoper na pesa za watu kama hivi.
Na pia utakuta pia riba ni ndogo sana.
Sasa ili kuondoa migobgano kama hii waende wakakope bank wasiheze na pesa za watu.
Kwani wao Wana usoecial gani mpk wapate mikopo tofauti na watumishi wengine?
 
Hizi hela kweli wastaafu na waliokufa huwa wanapata kweli au ndio zinapigwa tu na mabaki ni namba?
 
Huu ndo ujinga ulioko katika nchi hii, fedha ni za watumishi na ni nani aliyeweka kipengele cha kukopesha watumishi wa PSSF fedha za watumishi?

Wastaafu hawalipwi maslahi yao kwa wakati kumbe fedha zao wanakopeshana wao wenyewe.na hayo yote ni madudu yanayopitishwa bungeni na wabunge wa CCM.

Watanzania ni muhimu kufuata nyayo za kenya ule ujinga wa kusema ukichagua upinzani kutakuwa na vita ni upuuzi na ulichochewa na hilo lichama.mbona kenya wamefanya mabadiliko na hakuna vurugu iliyotokea?

Changes is now from the constitution to election. 2025 wananchi tuamke mabadiliko ni muhimu.
Upinzani wa akina Zitto na Mbowe ?hawana tofauti na hawa hawa waliopo.kama ilivyo kwa Ruto labda mpinzani wa kweli atoke CCM na kuunda chama chake
 
Shida ni Kwamba lazima watatemoper na pesa za watu kama hivi.
Na pia utakuta pia riba ni ndogo sana.
Sasa ili kuondoa migobgano kama hii waende wakakope bank wasiheze na pesa za watu.
Kwani wao Wana usoecial gani mpk wapate mikopo tofauti na watumishi wengine?
nahisi huwa ni scheme za Staff retention katika Taasisi zenye mahela mengi sana ili walau waridhike wasifanye ufisadi ambao hamtaujua

Mtu anapitisha mamilioni afu apewe gari IST kweli?

Imagine kama mawaziri mtu kama Awesso anasimamia miradi ya Billions of money afu aendeshwe na gari haieleweki?
Yanawasaidia kuwapoza nahisi
 
Hebu ngoja kwanza, hawa watu kumbe kuna sheria inawapa haki ya kulipiwa kodi ya gari hadi milioni mia[emoji24] KULIPIWA, siyo kukopeshwa. Halaf mwalimu wanamnyima exemption ya ki IST cha milioni 10 maskini wa Mungu. Africa bara la kiza lililolaaniwa.
 
Mtu amekopa, sasa kosa lipo wapi ?hizi hela zitarudishwa na riba. Tuache wivu.
 
20220915_134932.jpg
 
Yaani hela za mafao watu wamedunduliza miaka hadi 40 wewe unajikopesha kununua ndinga ya mamilioni huku wastaafu wakiminywa kwa kikokotoo na kusotea mafao yao hadi wengine miaka mitatu, halafu wachangiaji kwenye hiyo mifuko wakiomba kukopeshwa sehemu ya michango yao hawapewi haki hiyo, wanaishia kupigwa riba kubwa kwenye mabenki, hii si haki hata kidogo..
 
Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Bw. Ernest Khisombi Septemba 12, 2022amefikishwa mbele ya Baraza la Maadili kwa tuhuma za kujipatia mkopo wa gari binafsi wenye thamani ya Shilingi 196,570,931.00 kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995.

Akisoma mashtaka mbele ya Baraza la Maadili, Wakili wa Serikali Bw. Hassan Mayunga ameliambia Baraza kuwa, mtuhumiwa anashtakiwa kwa makosa mawili ambayo ni kukopa fedha za mfuko kiasi cha shilingi 117,808,470.00 bila kufuata utaratibu.

Katika lalamiko hilo Na. 5 la mwaka 2022, kosa la pili ni kulipiwa kodi kiasi cha shilingi 78,762,461.00 bila kufuata utaratibu wa Sera ya Mikopo ya PSSSF.

Kwa mujibu wa Bw. Mayunga, kitendo hicho kinamfanya Bw. Khisombi ambaye ni Kiongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kushidwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) na (b) na hivyo kukiuka maadili ya viongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu cha 6(2) cha Sharia ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hata hivyo, Bw. Khisombi amezikana tuhuma hizo na kulieleza Baraza la Maadili kuwa, “fedha hizi ni ihaki yangu kama Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi kwa mujibu wa Sera ya Mikopo ya Mfuko.”

Shahidi wa mlalamikaji Bw. Gideon Mafwiri ameliambia Baraza kuwa kiongozi huyo alijipatia mkopo kinyume na utaratibu uliowekwa na mfuko wa mikopo wa PSSF.

Mfuko wa mikopo umeweka utaratibu wa ni viongozi wapi wanastahili kulipiwa kodi na mfuko nan i gali la namna gani litalipiwa kodi na mfuko kwa mujibu wa taratibu,” alisema.

Kwa mujibu wa maelezo ya shahidi, utaratibu wa Mfuko ni kuwa maombi ya mkopo yaidhinishwe na Kamati ya Mkopo ya Mfuko, mkopaji kulipia asilimia 5 ya mkopo kabla hajapatiwa mkopo pamoja na kulipiwa kodi gari jipya la kiongozi kwa asilimia 100.

“Sera ya mikopo ukurasa wa 10 inasema mkopo huo outalipiwa asilimia 5 kabla mkopaji hajapatiwa. Utaratibu huu haukufuatwa,” amesema.

Bw. Mafwiri ameeleza kuwa wakati mfuko unalipia kodi ya gari la Bw. Khisombi, gari hilo halikuwa jipya kama Sera ya Mfuko huo inavyoelekeza. Ushahidi wa shauri hilo Na. 5 la mwaka 2022 umekamilika na kufungwa kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Baraza hilo.

Baraza la Maadili lililoanza vikao vyake vya uchunguzi Septemba 6, 2022, limekwisha sikiliza malalamiko mengine kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongizi wa Umma dhidi ya Bw. Godfrey Chibulunje aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu katika Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Hoseah Kashimba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF) na Bi. Beatrice Lupi, Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

Baraza hili linaloongozwa na jaji (Msf) Ibrahimu Mipawa na wajumbe Bw. Peter Ilomo na Bi Suzan Mlawi linafanya uchunguzi wa wazi kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (5) na 29 (6) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma (Sura 398).

Chanzo: Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Marejesho anafanya?
 
Nchi hii hela za mafao za watu wanazitumbua sana

Ova
 
Back
Top Bottom