Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Kinachoendelea kwenye makatazo kwa abiria wanaopanda treni ya SGR ni kuonesha ushamba na ulimbukeni.

Hili la kukataza mifuko yenye zipu maarufu kama shangazikaja na maji ya kunywa chupa moja! Na vitu vingine visivyokuwa na athari kwa abiria wengine.

Tanzania Railways Corp
Tupunguze lawama,
Safari ya saa 1.49 Dar-Moro unapanda na chakula cha nn? Exceptionals kwa mama wenye watoto na wagonjwa ipo what else tunahitaji?

Tukiruhusu hayo mengine sisi tunajijua, tutaishia kujifutia mabaki ya chakula kwenye viti na mabak mengine tutatupa chini ya siti.

Bado ustaarabu kwetu ni somo gumu, wacha twende hiv kwanza!
 
Hizo biashara si za shirika na wanaouza hawalipi kodi wala hawatoi risiti.
 
Tupunguze lawama,
Safari ya saa 1.49 Dar-Moro unapanda na chakula cha nn? Exceptionals kwa mama wenye watoto na wagonjwa ipo what else tunahitaji?

Tukiruhusu hayo mengine sisi tunajijua, tutaishia kujifutia mabaki ya chakula kwenye viti na mabak mengine tutatupa chini ya siti.

Bado ustaarabu kwetu ni somo gumu, wacha twende hiv kwanza!
Hicho chakula kimeingiaje humu!
 
Punguza ujuaji, sisi watu weusi tuna matatizo. Hizi treni hata huko kwa wenzetu wamachinga wanaingia kuuzia abiria vitu.
Mkuu mimi sijaleta ujuaji.
Naandika kwa msisitizo tukubali tukatae Tanzania raia tunapenda sana kulalamika tena saaanaaaa.
Kama huwezi kupanda SGR panda mgr diesel deluxe locomotive.
Katika hivyo vitu kuna jambo la kulalamika mkuu!??
Zote ni trivial complains.
Mambo madogo kulalamika aisee watanzania tuna safari ndefu sana.
Punguzeni kulalamika.
Halafu pia sisi sio watunzaji wa miundombinu hata uchembe.
Kama isipowekwa sheria za udhibiti miundombinu itachakaa mapema hutoamini.
Nilisafiri juzi tu hapa kurudi Dar kutoka Morogoro,sehemu ya kuwekea vitu kile kimeza cha mbele ya kiti mtu anafosi aweke pale mtoto ambadilishe pampers!!
Ushaambiwa pale kisikae kitu kizito na hadi kutangaza wanatangaza.
Mtu ana tissue kamaliza kula haitoshi anapangusa kwa kiti.
Punguzeni kulalamika kwa mambo yasiyo na tija mkuu.
 
Acha kujifanya tajiri, hiyo shangazikaja tatizo lake ni nini!
Mkuu sijajifanya tajiri hata kidogo najijua mimi masikini tu.
Ndio maana nikaongea kauli jumuishi ya kuwa "tusipoangalia tutabaki kuwa masikini kwa kulalamika".
Kila kitu sio lazima ukilalamikie.
Kwani kuna hasara gani wewe unapata ukiwa na begi tofauti na shangazi kaja??
Huoni unalalamika pasipo na mashiko mkuu!?
Lalamika kwa kitu unachoona kinakukandamiza.
 
Masanja Kungu Kadogosa Tafadhali Njoo Na Msemaji Wenu Mtutoe Ukakasi
 
Mkuu mimi sijaleta ujuaji.
Naandika kwa msisitizo tukubali tukatae Tanzania raia tunapenda sana kulalamika tena saaanaaaa.
Kama huwezi kupanda SGR panda mgr diesel deluxe locomotive.
Katika hivyo vitu kuna jambo la kulalamika mkuu!??
Zote ni trivial complains.
Mambo madogo kulalamika aisee watanzania tuna safari ndefu sana.
Punguzeni kulalamika.
Halafu pia sisi sio watunzaji wa miundombinu hata uchembe.
Kama isipowekwa sheria za udhibiti miundombinu itachakaa mapema hutoamini.
Nilisafiri juzi tu hapa kurudi Dar kutoka Morogoro,sehemu ya kuwekea vitu kile kimeza cha mbele ya kiti mtu anafosi aweke pale mtoto ambadilishe pampers!!
Ushaambiwa pale kisikae kitu kizito na hadi kutangaza wanatangaza.
Mtu ana tissue kamaliza kula haitoshi anapangusa kwa kiti.
Punguzeni kulalamika kwa mambo yasiyo na tija mkuu.
Rudi kwenye hoja kuu,why ukataze maji nusu lita mtu kabeba ndani ya kibegi chake ili ameze dawa au kwa shida zake? Kwa nini ufosi mtu lazima anunue kwako why?? Kwanza vimaji hivyo kwenye Buses wengi wanatoa bure plus soda na biskuti..
 
Kadogosa si Ni msukuma.
Msukuma na ushamba Ni Kama uji na mgonjwa.
Anataka tuingie kwenye treni na briefcase halafu atulazimishe tunywe maji anayotaka yeye.
Mimi kwanza sinywi maji ya dukani. Maji nachemsha mwenyewe na ndio natembea nayo.
Kabila limeingiaje sasa hapo?
 
Rudi kwenye hoja kuu,why ukataze maji nusu lita mtu kabeba ndani ya kibegi chake ili ameze dawa au kwa shida zake? Kwa nini ufosi mtu lazima anunue kwako why?? Kwanza vimaji hivyo kwenye Buses wengi wanatoa bure plus soda na biskuti..
Nilichoongea hakipo nje ya hoja.
Hizo ni taratibu zimewekwa na wala hazina ukinzani wowote na hazina madhara yeyote.
Buku inakushinda kununua maji umeze dawa!??
Yani sheria ndogo tu ya kutokuingia na maji unapiga kelele!??
Huo ni uchawi typically.
 
Dah, sasa mkuu kuingia na Konyagi ni kosa tena. Huo ni usafiri wa kawaida tu sema tuna ulimbukeni tu. Niliona treni moja huko Japan (SGR), kuna route yake moja wakulima na wafugaji wanaingia na mbuzi, kondoo, maparachichi, kuku nk.
Ipo ile ya zamani watumie mkuu, Japan watu ni wastaarabu huku mtu anaingia amelewa mara anataka akojoe kwenye seat na usumbufu mwingi sn
 
Acha kujifanya tajiri, hiyo shangazikaja tatizo lake ni nini!
Ni ushamba tuu unawasumbua ...nimeshapanda ndege mara kadhaa na abiria wenye shangazi kaja. Take it from me kwenye hiyo SGR wakija wazungu 10 na mizigo yao ikiwemo shangazi kaja wanaenda Dodoma hutaona wakiwazuia, wanawaogopa
 
Kuna watu wapo sensitive sana na maji pamoja na chakula kwa ujumla. Najiuliza, hayo maji yanayouzwa ndani hakuna namna wahuni wakawa wanauza maji feki mwisho wa siku watu wakaugua matumbo? Wabongo tunajuana! Pesa mbele kwanza!
Swala la maji ya kunywa ni very sensitive, wangeruhusu angalau chupa moja ya 500ml au 1000 kwa kila abiria.
 
Unatofautishaje maji na Konyagi iliyowekwa kwenye chupa ya maji.... Au wanapaswa kufungua na kutaste kama ni maji kweli..

Maji yapo ndnai ya Train.... Lazima tukubali kufata utaratibu. Mbona izo lawama hamzileti upande wa ndege, wakati taratibu zinafanana.
Kwa hiyo,unalinganisha ndege na train?
 
Pppp0lp0llpp
Ipo ile ya zamani watumie mkuu, Japan watu ni wastaarabu huku mtu anaingia amelewa mara anataka akojoe kwenye seat na usumbufu mwingi sn
Lakini hata reli ya kati tulikuwa tunauziwa pombe from Dar to Mwanza. Unakata third class unakwenda kaa zako behewa la kuuziwa vinywaji (buffet). Hao wasumbufu wanashughulikiwa tu.
 
Back
Top Bottom