Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Nimepanda leo asubuhi, everything was fine, kitu kibaya nilichoona kuna wahudumu wamevaa sare wengine wamevaa kama vichaa, kuna mwanamke alipita kavaa makoti matatu na sketi ndefu huku anaongea kwa sauti nikajua ni chizi, nilikuja kugundua ni muhudumu alipopita huku anasukuma tray, yale mavazi sio ya hadhi muhudumu wa ile treni hata daladala,
Japo nimemuona mmoja tu ila hiyo hali sikuiona kipindi treni inaanza kazi,
Hili nalo mkalitizame
 
Baa ya kwenye treni inauza gongo pia? Ingekuwa ni fujo sasa. Watu wafuate utaratibu ambao mimi kwangu sioni shida
"Watu wafuate utaratibu ambao mimi kwangu sioni shida"! Mbona unanichanganya, wewe ndiye Kadogosa mwenyewe au ndio wale wa hiyo hela tuma kwa namba hii!
 
"Watu wafuate utaratibu ambao mimi kwangu sioni shida"! Mbona unanichanganya, wewe ndiye Kadogosa mwenyewe au ndio wale wa hiyo hela tuma kwa namba hii!
Kwani utaratibu umewekwa kwa ajili ya Kadogosa? Kila mtu aliye na maslahi na treni hiyo kwa vyovyote inabidi aunge mkono hatua zozote zitakazotolewa kwa lengo la kuutunza mradi huo. Kwanza SGR ikienda na utaratibu huu itakuwa ni zoezi zuri kwa wanaotarajia kupanda ndege especially kwa safari za nje ya nchi, maana kuna watu wakiambiwa kimiminika au fluid kinachozidi container ya mililita 100 hairuhusiwi kwenye ndege, huwa hawaelewi logic yake. Sasa walazimishwe kuzoea, sababu watazijua wakizitafuta
 
Shida watu wanaingia na konyagi badala ya maji
Nikiingia na konyagi shida inakuwa ni nini kwani?

Hii nchi ina watu wanaitwa takukuru na wanalipwa kabisa mishahara hivi hawana akili ya kutosha kuona kwamba kuna hujuma zinafanyika kuharibu hii kazi ili watu watumie mabasi badala ya treni??
 
TRC inaendeshwa kizeee sana .
fikiria pale morogoro kuna kidaraja kimejengwa ili kuweza kufanikisha ushushaji na upandaji kwa pamoja kukiwa na treni mbili kwa wakati mmoja. sasa kwa mfano treni ya Dar -dom asubuhi inalazimika kusubiria abiria kwa zaidi ya dakika kumi maporini huko wakati ingeweza ikajikongoja na kuja kushusha abiria kwenye kile kinjia cha overpass na ikaendelea na safari.
Steshen ya Dodoma ndani kuna eneo limetenga kwa ajili kupaki treni mbili ambapo upande wa pili watu wanashuka au kupanda kwa kupitia underpass, lakini mpaka leo hakuna reli iliyotandazwa pale, ni kama wamejikadiria kuwa hakuna abiria wakuweza lazimisha treni mbili zipishane kwa wakati mmoja.
TRC wanafeli kabla ya kuanza, kitu wamechokariri ni kuwa watafanya biashara kwenye mizigo wakati uhalisia hata kwa abiria wangeweza tengeneza hela kuliko wanavyofikiria.
tukianza sasa kukagua posho hapo unaweza kuta inazidi mapato
 
UWT sijui kama una akili, wanapozuia kuingia na vyakula maanake kwenye train au ndege hakuna vyakula? usalama wa vyakula vya nje unaujua?
Leo umeamkaje ndugu?.

Kwani chakula cha nje na maji ya nje yana tofauti gani?.

Nanunua chupa ya maji na cake hapo dukani la stesheni, vitu hivyo hovyo ndivyo vinauzwa humo ndani ya treni tofauti yake nini kwenye usalama?.

Nadhani hiyo siyo logic, ungesimama na issue ya watu kuweka pombe kwenye chupa sawa ila siyo hicho ulichoandika NO!.
 
Kadogosa Anataka tuingie kwenye treni na briefcase halafu atulazimishe tunywe maji anayotaka yeye.
Mimi kwanza sinywi maji ya dukani. Maji nachemsha mwenyewe na ndio natembea nayo.
Ina shida na kadogosa

Ongelea TRC kasogosa hakagui mabehewa
 
Mimi shida yangu ipo kwenye kutuzia kusafiri na silaha tunazozimiliki kisheria kabisa. Airport wameweka utaratibu tukifika kunakabidhi kwa maafisa wa polisi tunasafiri vizuri tu na tukifika mwisho wa safari tunarudishiwa silaha zetu. Uongozi wa Trc hebu angalieni hilo.
 
Back
Top Bottom