Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Mkurugenzi TRC Kadogosa njoo JamiiForums ujibu tuhuma za kinachoendelea kwenye treni ya SGR

Wapi watendaji wa chura kiziwi wakafanya vizuri?
 
Kwani utaratibu umewekwa kwa ajili ya Kadogosa? Kila mtu aliye na maslahi na treni hiyo kwa vyovyote inabidi aunge mkono hatua zozote zitakazotolewa kwa lengo la kuutunza mradi huo. Kwanza SGR ikienda na utaratibu huu itakuwa ni zoezi zuri kwa wanaotarajia kupanda ndege especially kwa safari za nje ya nchi, maana kuna watu wakiambiwa kimiminika au fluid kinachozidi container ya mililita 100 hairuhusiwi kwenye ndege, huwa hawaelewi logic yake. Sasa walazimishwe kuzoea, sababu watazijua wakizitafuta
Kwani treni ndiyo ndege, mtanzania ukimwambia avue viatu anapoingia ndani ya ndege atakuelewa kwa sababu ya mazoea ya uswazi.
 
Leo umeamkaje ndugu?.

Kwani chakula cha nje na maji ya nje yana tofauti gani?.

Nanunua chupa ya maji na cake hapo dukani la stesheni, vitu hivyo hovyo ndivyo vinauzwa humo ndani ya treni tofauti yake nini kwenye usalama?.

Nadhani hiyo siyo logic, ungesimama na issue ya watu kuweka pombe kwenye chupa sawa ila siyo hicho ulichoandika NO!.
Hata kuweka pombe ndani ya chupa ya maji si tatizo, unywaji wa pombe ndani ya treni ni halali vinginevyo wasingeweka baa ndani ya treni.
 
Kinachoendelea kwenye makatazo kwa abiria wanaopanda treni ya SGR ni kuonesha ushamba na ulimbukeni.

Hili la kukataza mifuko yenye zipu maarufu kama shangazikaja na maji ya kunywa chupa moja! Na vitu vingine visivyokuwa na athari kwa abiria wengine.

Tanzania Railways Corp
Athari za kuteua watu wasiokua compitent kusimamia taasisi compitent.
 
Dah, sasa mkuu kuingia na Konyagi ni kosa tena. Huo ni usafiri wa kawaida tu sema tuna ulimbukeni tu. Niliona treni moja huko Japan (SGR), kuna route yake moja wakulima na wafugaji wanaingia na mbuzi, kondoo, maparachichi, kuku nk.
Mule ndani konyagi si zipo

Ova
 
Hata kuweka pombe ndani ya chupa ya maji si tatizo, unywaji wa pombe ndani ya treni ni halali vinginevyo wasingeweka baa ndani ya treni.
Sasa kila mtu akija na kinywaji chake vile vya kwenye treni nani atanunua?.
 
Back
Top Bottom