Mkurugenzi wa Bandari alikuwa sikio la kufa lisilosikia dawa

Mkurugenzi wa Bandari alikuwa sikio la kufa lisilosikia dawa

Tiss wapo, PCCB wapo kwanini watu wanafeli? Mh. Rais tumia vyombo vyako vizuri kufanya uwekezaji Kuna vyombo vinakurubuni Sana nikushauri Mh. Vunja Tiss na PCCB then baada ya mwaka utaona changes kubwa IGA S.A & others utaona walifanikiwa kwa kufanya changes kwa kuvunja hizi Taasisi na kuunda upya naongea kwa uzoefu
Hana nia hiyo, hata kama angekuwa na uwezo wa "kuvunja" kama unavyomshauri.

Vyombo hivyo, kama ilivyo kwa vyombo vingine vyote, kama polisi, uhamiaji, n.k., wapo hivyo kwa sababu vinatimiza matakwa yake.
Sasa yeye atavivunja kwa sababu gani, kama vinatimiza anayoyataka yeye?

Vyombo hivyo viko hivyo, kwa sababu vinaelewa matakwa wa anayevimiliki. Hivyo vyombo vingekuwa ni mali ya wananchi, vingekuwa na utendaji tofauti na vinavyofanya sasa hivi.
 
Anayefanya vetting naye anatakiwa afanyiwe vetting.
Nani atamfunga paka kengele!!??
Suluhisho ni kupiga chini vyombo vyote vya vetting kwanza ili tupate wachujaji wazuri.
Mkuu 'residentura', naomba unisome hapo juu.

Hivi vyombo hata vikivunjwa leo hii (najuwa hakuna kiongozi mwenye uthubutu huo kwa sasa), vitakavyoundwa tena vitafanya yale yale ya vile vilivyovunjwa, kwa sababu bado vitakuwa chini ya mfumo uleule mbovu.
Kwa hiyo, nasema, haitoshi kuvivunja, bali kinachotakiwa ni kuunda mfumo mpya kabisa unaosimamia vyombo hivi badala ya kuwa vinamfanyia kazi mtu mmoja kwa matakwa yake.
 
Hakuna vita ngumu duniani kama vita dhidi ya Rushwa ya Pesa.
Yaani karne hii watu wanaishi kutafuta pesa halafu wewe unapewa kazi ya kuwazuia.
Watu wako tayari kupoteza kazi, kupoteza mke, kupoteza watoto, kupoteza marafiki, kupoteza madaraka, kusaliti nchi ili tu apate pesa. Wengine wapo tayari kufa.
Lakini pia usisahau, kuna walio tayari kuweka maisha yao chini ya nchi yetu, Tanzania.

Kwa hiyo usiangalie upande mmoja unakosimamia wewe.
 
Bila kuunda upya TISS, PCCB, TanPol na TPA yenyewe,kamwe tusitegemee bandari kuinufaisha nchi.
Hata tukiuunda upya hao watu bado watakua wale wale kina mchechu, kadogosa, mafuru, gerson Msigwa, kidata, nape, makamba, aweso, mbarawa n.k
Watu hawatatoka mbinguni. Labda serikali ipogwe chini ije serikali mpya ya chama kingine pengine kutakua na watu wazuri
 
Hata tukiuunda upya hao watu bado watakua wale wale kina mchechu, kadogosa, mafuru, gerson Msigwa, kidata, nape, makamba, aweso, mbarawa n.k
Watu hawatatoka mbinguni. Labda serikali ipogwe chini ije serikali mpya ya chama kingine pengine kutakua na watu wazuri
Kuunda upya ni pamoja na kuondoa vya zamani ndugu Memento .
Ndugu Kalamu kaandika vyema hapo juu.
Hizi taasisi zinatakiwa ziwe kwa ajili ya wananchi na nchi,sio kwa ajili ya uongozi uliopo madarakani.
 
Binafsi Bora ninunue kitu kwa gharama kubwa ila pesa yangu iende Serikalini.

Pamoja na kwamba watu wanasema pesa zinapigwa huko ukweli ni kwamba zinazopigwa hazizidi hata 15% ..

Nachojua pesa hupotea zaidi Serikalini kwa mipango mibovu na vipaombele visivyojibu mahitaji ya watu directly but hilo nalo ni la mda tuu,lazima tulipe Kodi maana hakuna shortcut ya Huduma kuboreshwa bila pesa.
 
Huyo mkurugenzi atakuwa katoza ushuru mizigo ya wenye chama, wenye nchi na wala mema ya nchi.

Mkurugenzi atakayedumu badarini kwa sasa lazima awe ni yule anayepitisha bure mizigo ya wenye nchi, wenye chama na wala mema ya nchi
Sasa nimeelewa kumbe ndio maana Kakoko alikaa sana bandarini na yule mwenzake wa Tanroad bwana mfugale kwa kuwa michongo yote ya upigaji ya bwana mkubwa walihakikisha haikwami.
 
Naona hauelewi kitu mkuu iko hivi unapoanza kazi unakua na uadilifu wako ila unapokua unaendelea na kazi unaanza kua corrupt mambo mengi haswa yanachangiwa na serikali yenyewe
1. kimsingi mishahara ya serikali sio mikubwa kivile..na watu wanakutegemea wa kutosha lakini mwisho wa siku unakuja dhulumiwa mwishoni na serikali hio hio
2. Sera mbovu za serikali kuhusu kustaafu i.e umefanya kazi miaka 30 tuseme una akiba ya 100m huko kwenye pension utapewa 33m halafu hio 67m utakua unagaiwa kidogo kidogo kama pension ukifariki hio pension watoto wako au wategemezi hawaji kupewa inakua imeisha sasa niambie wewe umeona kuna fursa ya kupiga i.e 2m kila siku mzee utaiacha hio ulete huo uadilifu wako ? Upo sehemu labda umekaimu tu nafasi i.e kwa miezi 5 au 6 hapo unapiga huo mpunga mambo mengine Mungu atasaidia...
3.Pia unapofanya kazi serikalini kimsingi hakuna tuzo wala recognition wala acknowledgement yoyote utapata kwa jambo lolote lile kufika hatua za mbali inategemea na "technical know who" kwaio unaweza ukafanya mambo kwa nia njema tu ila ukikosea sehemu ndogo tu mzee utasimamishwa kazi..takukuru watakuja kwako kupindua pindua nyumbani kwako kukuharass na maswala kadha wa kadha baadae ukibahatika i.e miaka 2 unarudi kazini ushapotea kwenye ramani unapelekwa huko namanyere...😀😀😀😀
Umeandika; na 'it makes sense' kwa mtu mwenye akili makini.

Sasa tufanye hivi: Pawepo na serikali inayojitahidi kulinda maslahi ya hawa watumishi wake. Iondokane na dhulma hizo ulizozitaja humo ndani.

Bado wizi/uzembe utakuwepo kwa baadhi kama siyo wote kama hakuna hatua za ziada kukomesha/kupunguza hali hiyo.

Sasa fanaya hivi: Serikali iweke utaratibu unaofahamika wazi kabisa, bila ya kuficha kitu. Kama wewe ni mtumishi huko serikalini, na ukabainika unakorofisha kwenye kazi zako; hutaonewa, sheria itapewa nafasi yake ifanye kazi. Baada ya hapo umeonekana una makosa ya kuhujumu nchi yako. Shaba ni haki yako moja kwa moja.

Katika tulipofikia na tunakokwenda, binafsi sitapinga hatua hiyo ikichukuliwa kupunguza haya tunayoyaona yakiendelea mwaka baada ya mwaka na yanazidi kuongezeka.

Hebu nipe mrejesho juu ya fikra zako kuhusu pendekezo hili.
 
Huyo mkurugenzi atakuwa katoza ushuru mizigo ya wenye chama, wenye nchi na wala mema ya nchi.

Mkurugenzi atakayedumu badarini kwa sasa lazima awe ni yule anayepitisha bure mizigo ya wenye nchi, wenye chama na wala mema ya nchi
Kwni mama si anaupiga mwingi na kukomesha mataga na sukuma gang?
 
Unatumbukiwa wakt ukikuwa una kunya mkwanja wa mikini 34 kwa mwezi hv nikitoka pale naitaji kaz gani
 
Bila kuunda upya TISS, PCCB, TanPol na TPA yenyewe,kamwe tusitegemee bandari kuinufaisha nchi.

Tatizo ni kubwa zaidi ya taasisi hiyo, tatizo ni rasilimali watu wenye uwezo wa maono kuendesha operesheni. Wakiingia wanaanza kushangaa waanze wapi, waishawishi serikali vipi na wapate mabadiliko chanya yapi ktk muda mfupi kwa kutumia ujuzi ambao upo ktk makaratasi ya ripoti.
 
Yaani bandari hii inataka kila sehemu iwe inajitegemea peke yake na bosi wake
Naona Bandari ni mzigo mkubwa kuiongoza maana ina ingiza mabilioni na kuna wakubwa wamo kwenye kula hapo na bidhaa ama zao au shared au ni marafiki wakubwa na wanaoingiza mizigo na wanawabeba

Bandari ina mambo haswa na hakuna wa kuiweza hata ukijifanya unajuwa utanyooshwa uwe kama wao penda usipende utacheza ngoma yao
Ndio hapo utaambiwa huna kazi kumbe umebanwa mahali
Kimsingi ni kugumu mzee, unalambishwa mabuyu ya asali hadi unapagawa 😀😀😀 huyu anahonga million 2OO mwengine mara kaja na 3OO mara shwaa kuna fogo anakumwagia 6OO hahahah hivi kuna mtu anaweza akaruka hio mitego 😂😂😂
 
Kimsingi ni kugumu mzee, unalambishwa mabuyu ya asali hadi unapagawa [emoji3][emoji3][emoji3] huyu anahonga million 2OO mwengine mara kaja na 3OO mara shwaa kuna fogo anakumwagia 6OO hahahah hivi kuna mtu anaweza akaruka hio mitego [emoji23][emoji23][emoji23]

[emoji23][emoji23] hakuna atakaeacha
Kama traffic tu anapokea mpaka buku
Itakuwa mtu anaambiwa zile nyumba mbili za masaki nakubadilishia Hati miliki kesho ila hiyo meli isikaguliwe ok [emoji23][emoji23]
Hata mke atatoa [emoji23]
 
[emoji23][emoji23] hakuna atakaeacha
Kama traffic tu anapokea mpaka buku
Itakuwa mtu anaambiwa zile nyumba mbili za masaki nakubadilishia Hati miliki kesho ila hiyo meli isikaguliwe ok [emoji23][emoji23]
Hata mke atatoa [emoji23]
Hahahahahahahah vita ya uchumi ni ngumu sana hasa rushwa ya hela ndefu inapoingia kwenye muvi😂😂😂
 
Back
Top Bottom