Mkurugenzi wa Bandari alikuwa sikio la kufa lisilosikia dawa

Hana nia hiyo, hata kama angekuwa na uwezo wa "kuvunja" kama unavyomshauri.

Vyombo hivyo, kama ilivyo kwa vyombo vingine vyote, kama polisi, uhamiaji, n.k., wapo hivyo kwa sababu vinatimiza matakwa yake.
Sasa yeye atavivunja kwa sababu gani, kama vinatimiza anayoyataka yeye?

Vyombo hivyo viko hivyo, kwa sababu vinaelewa matakwa wa anayevimiliki. Hivyo vyombo vingekuwa ni mali ya wananchi, vingekuwa na utendaji tofauti na vinavyofanya sasa hivi.
 
Anayefanya vetting naye anatakiwa afanyiwe vetting.
Nani atamfunga paka kengele!!??
Suluhisho ni kupiga chini vyombo vyote vya vetting kwanza ili tupate wachujaji wazuri.
Mkuu 'residentura', naomba unisome hapo juu.

Hivi vyombo hata vikivunjwa leo hii (najuwa hakuna kiongozi mwenye uthubutu huo kwa sasa), vitakavyoundwa tena vitafanya yale yale ya vile vilivyovunjwa, kwa sababu bado vitakuwa chini ya mfumo uleule mbovu.
Kwa hiyo, nasema, haitoshi kuvivunja, bali kinachotakiwa ni kuunda mfumo mpya kabisa unaosimamia vyombo hivi badala ya kuwa vinamfanyia kazi mtu mmoja kwa matakwa yake.
 
Lakini pia usisahau, kuna walio tayari kuweka maisha yao chini ya nchi yetu, Tanzania.

Kwa hiyo usiangalie upande mmoja unakosimamia wewe.
 
Bila kuunda upya TISS, PCCB, TanPol na TPA yenyewe,kamwe tusitegemee bandari kuinufaisha nchi.
Hata tukiuunda upya hao watu bado watakua wale wale kina mchechu, kadogosa, mafuru, gerson Msigwa, kidata, nape, makamba, aweso, mbarawa n.k
Watu hawatatoka mbinguni. Labda serikali ipogwe chini ije serikali mpya ya chama kingine pengine kutakua na watu wazuri
 
Kuunda upya ni pamoja na kuondoa vya zamani ndugu Memento .
Ndugu Kalamu kaandika vyema hapo juu.
Hizi taasisi zinatakiwa ziwe kwa ajili ya wananchi na nchi,sio kwa ajili ya uongozi uliopo madarakani.
 
Binafsi Bora ninunue kitu kwa gharama kubwa ila pesa yangu iende Serikalini.

Pamoja na kwamba watu wanasema pesa zinapigwa huko ukweli ni kwamba zinazopigwa hazizidi hata 15% ..

Nachojua pesa hupotea zaidi Serikalini kwa mipango mibovu na vipaombele visivyojibu mahitaji ya watu directly but hilo nalo ni la mda tuu,lazima tulipe Kodi maana hakuna shortcut ya Huduma kuboreshwa bila pesa.
 
Huyo mkurugenzi atakuwa katoza ushuru mizigo ya wenye chama, wenye nchi na wala mema ya nchi.

Mkurugenzi atakayedumu badarini kwa sasa lazima awe ni yule anayepitisha bure mizigo ya wenye nchi, wenye chama na wala mema ya nchi
Sasa nimeelewa kumbe ndio maana Kakoko alikaa sana bandarini na yule mwenzake wa Tanroad bwana mfugale kwa kuwa michongo yote ya upigaji ya bwana mkubwa walihakikisha haikwami.
 
Umeandika; na 'it makes sense' kwa mtu mwenye akili makini.

Sasa tufanye hivi: Pawepo na serikali inayojitahidi kulinda maslahi ya hawa watumishi wake. Iondokane na dhulma hizo ulizozitaja humo ndani.

Bado wizi/uzembe utakuwepo kwa baadhi kama siyo wote kama hakuna hatua za ziada kukomesha/kupunguza hali hiyo.

Sasa fanaya hivi: Serikali iweke utaratibu unaofahamika wazi kabisa, bila ya kuficha kitu. Kama wewe ni mtumishi huko serikalini, na ukabainika unakorofisha kwenye kazi zako; hutaonewa, sheria itapewa nafasi yake ifanye kazi. Baada ya hapo umeonekana una makosa ya kuhujumu nchi yako. Shaba ni haki yako moja kwa moja.

Katika tulipofikia na tunakokwenda, binafsi sitapinga hatua hiyo ikichukuliwa kupunguza haya tunayoyaona yakiendelea mwaka baada ya mwaka na yanazidi kuongezeka.

Hebu nipe mrejesho juu ya fikra zako kuhusu pendekezo hili.
 
Huyo mkurugenzi atakuwa katoza ushuru mizigo ya wenye chama, wenye nchi na wala mema ya nchi.

Mkurugenzi atakayedumu badarini kwa sasa lazima awe ni yule anayepitisha bure mizigo ya wenye nchi, wenye chama na wala mema ya nchi
Kwni mama si anaupiga mwingi na kukomesha mataga na sukuma gang?
 
Unatumbukiwa wakt ukikuwa una kunya mkwanja wa mikini 34 kwa mwezi hv nikitoka pale naitaji kaz gani
 
Bila kuunda upya TISS, PCCB, TanPol na TPA yenyewe,kamwe tusitegemee bandari kuinufaisha nchi.

Tatizo ni kubwa zaidi ya taasisi hiyo, tatizo ni rasilimali watu wenye uwezo wa maono kuendesha operesheni. Wakiingia wanaanza kushangaa waanze wapi, waishawishi serikali vipi na wapate mabadiliko chanya yapi ktk muda mfupi kwa kutumia ujuzi ambao upo ktk makaratasi ya ripoti.
 
Tatizo ndio lipo hapa.
We huoni kuwa hata sasa karudisha watu wale wale wa miaka 8 nyuma?

Kidata - TRA, Mchechu Nhc, Mramba Tanesco, mafuru hazina n.k

Wakati alipaswa kutafuta sasa watu wapya ambao pengine hawana mizizi ndani ya hizo taasisi ili kujaribu kuziunda upya.
 
Kimsingi ni kugumu mzee, unalambishwa mabuyu ya asali hadi unapagawa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ huyu anahonga million 2OO mwengine mara kaja na 3OO mara shwaa kuna fogo anakumwagia 6OO hahahah hivi kuna mtu anaweza akaruka hio mitego πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

[emoji23][emoji23] hakuna atakaeacha
Kama traffic tu anapokea mpaka buku
Itakuwa mtu anaambiwa zile nyumba mbili za masaki nakubadilishia Hati miliki kesho ila hiyo meli isikaguliwe ok [emoji23][emoji23]
Hata mke atatoa [emoji23]
 
[emoji23][emoji23] hakuna atakaeacha
Kama traffic tu anapokea mpaka buku
Itakuwa mtu anaambiwa zile nyumba mbili za masaki nakubadilishia Hati miliki kesho ila hiyo meli isikaguliwe ok [emoji23][emoji23]
Hata mke atatoa [emoji23]
Hahahahahahahah vita ya uchumi ni ngumu sana hasa rushwa ya hela ndefu inapoingia kwenye muviπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…