And what about the things this deal brings? Never underestimate the power of political will.Najaribu kuhesabu drama za tokea 2017 hadi Leo naona nimepoteza hesabu yake! Haya kila lakheri Twiga company!
Usawa wa zitto ni Migebuka. Haya makemia aachane nayo kabisa .Mzee wa Miga yeye kwenye mahame aliko anafutuka tu kula kulala
..nadhani viongozi wanadanganya.
..hakuna mtu aliyesema ule ulikuwa mchanga sawa na unaochimbwa maeneo mengine.
..kwa uelewa na kumbukumbu zangu ule ulikuwa ukiitwa mchanga wenye dhahabu. baadaye ukapata jina jipya la makinikia.
..wakati mwingine VIONGOZI wanadanganya na kupotosha kitu ambacho siyo sahihi.
Kumbuka pia kufanya kosa ni sehemu ya kujifunza!Kwa hiyo hawa jamaa walikuwa wanajibebea tu.
Ina maana wale waliokuwepo kabla ya Mzee baba walikuwa wameridhika au walikuwa sehemu ya mpango?
Mwisho wa siku unabaki kujiuliza "hivi hawa jamaa walituonaje?" maana hii haina tofauti na Mtu kukuchapia Mkeo.
Tanzania sio moja. You can take that to the bankNani amesema Tanzania sio moja? Hii statement inaonyesha inferiority complex! Wewe jenga tu hoja zako kama zina nguvu za hoja basi zitasimama!
Hizo trillions za ma Profesa Mruma na Ossoro zimefia kwenye majadiliano ambayo yamefikia mwafaka kwa kutiliana saini za makubaliano.
Msingi wa majadiliano yoyote ya maana unajengwa katika msingi wa mutual concessions and compromises.
Kama serikali ingetaka kuzipata hizo pesa basi ingeenda mahakamani ambako msingi wake ni take or lose.
Utauliza kwa nini serikali haikwenda mahakamani? Serikali haikwenda mahakamani kwa sababu ya hekima ya kisiasa. Ninaposema hekima za kisiasa nina maana kuwa, kesi kama hizi ambazo ni transnational litigation zinachukua muda mrefu sana kumalizika na kuna uwezekano mpaka muda wa awamu ya tano ungeisha bila hukumu ya kesi hiyo kutolewa.
Kilichofanyika ni concessions and compromises kwa pande zote.
mitale na midimuMsemajiUkweli,
Mkuu kwa waliokimbia hisabati unaweza kudhani ni fedha nyingi sana. ila kwa sababu suala la makinikia halikuruhusu factbased public discussion bado hata likiisha halitakuwa na valuable lessons learned.
Mfano kwa Content ya madini waliyosemaga Acacia, tena wakatoa mafafanuo Public.
Kwa hicho kiasi ni sawa hata kwa hesabu za hao acacia na baada ya kukaguliwa na gov agencies.
Kwanza sio za siku moja, ni tangu zilipozuiwa (aggregate).
Pia Hapo hawajatoa gharama ya kuzalisha hizo products za kiasi hicho.
Hiyo figure kisiasa ni ya kushtusha ila kwa kurudi kwenye details unaweza kukuta mzungu kaongea lugha ileile aliyokuwa anasema na watafiti wakiserikali waliipinga.
tuzidi kujifunza kwa ukaribu zaidi ili tuone nani yuko sahihi.
Waliambiwa mapema lakini ujuaji mwingi kumbe ujinga mtupu...ukisikiliza hotuba ya Prof.Kabudi ni kwamba makubaliano haya yametokana na "hisani" na "huruma" ya mabeberu wa barrick.
..Prof.Kabudi anakiri kuwa alishindwa. Kuna wanasheria walikuwa wameweka msimamo.
..sasa hiyo maana yake ni kwamba serikali ilikuwa haina hoja zenye uzito wa kisheria dhidi ya accacia na barrick.
..CCM ndiyo waliotuingiza ktk hasara na fedheha hii. Wao ndiyo waliopitisha sheria mbaya za madini na nishati. Ni serikali za CCM ndizo zilizosaini mikataba mibovu ya kinyonyaji.
..Kwa miaka kadhaa CCM na mawakala wao walikuwa wakitetea mikataba mibovu ya madini.Walipaswa kuamka mapema na siyo miaka 20 baadae.
Jamani Tungeacha kumjadili huyo Mshamba, alinikela sana alivyoenda Afrika kusini kumshauri yule Mjinga akamate ndege yetu kule Canada kwa sababu ambazo ni za kutunga.
Sasa kama uko misungi kwa nini usilime hata bustani ya mbogamboga ili kuondokana na ugumu wa maisha!Karibu Wilayani Misungwi Mkuu.. hiyo ID isikutishe
Kuna baadhi ya watu ni kuachana nao kwa sababu watakupotezea muda wako! Hawajui kama ni wajinga lakini kikubwa zaidi hata kuelewa unachokiandika kwao ni mtihani!Sijui kama unajibu kulingana na hoja au unajibu kulingana na hisia?
Hatutaweza kufanya mjadala na wewe, tufanye hivi wewe upo sahihi mimi na tunaosifia jitihada za serikali kwenye sakata la madini hatupo sahihi.
Mwisho wa mjadala.
Dollar milioni 280?Wakati akiongea na shirika la habari ya Uingereza liitwalo Reuters, Mkurugenzi wa Kampuni ya Barrick Gold amesema Makontena ya Makinikia yaliyozuiwa na serikali ya Tanzania Bandarini Dar es Salaam yana thamani ya Dola za Kimarekani milioni 280 ambapo ni sawa na takribani shilingi za Kitanzania bilioni 647.
Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa wako mbioni kutekeleza makubaliano ya mkataba waliokubaliana na serikali ikiwa ni pamoja na kuilipa serikali ‘’kishika uchumba’’ cha thamani ya dola milioni 300.
‘’Tunavyoongea kwa sasa tumeanza mchakato wa kuyasafirisha Makinikia na baadaye tutailipa serikali ya Tanzania dola milioni 100’’, Mkurugenzi Mark Bristow alisema.
Alimalizia kwa kusema, ‘’Kwa sasa tuko mbioni kuanza tena uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu baada ya kuufunga kutokana na amri ya serikali kuzuia usafirishaji wa Makinikia’’.
Kwa mnaojua lugha ya Kiingereza mnaweza kusoma hapa:
1) Usijenge hoja kijumla jumla! Ni viongozi gani na chama gani? Nisaidie kunitajia!1. Tuchague viongozi wa Chama kingine chenye Sera na viongozi tofauti.
2. Tuandike Katiba ya Wananchi ili mikakati na vipaumbele vya maendeleo viwekwe sawa.
3. Tutafute haki,maridhiano na kuepuka visasi kama Taifa.
4. Tujenge nchi bila ubaguzi wa dini,kikabila,kikanda,kivyama na aina nyingine za ubaguzi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani hiyo barabara Barrick wamesema watajenga na kuboresha zingine ili kujenga uhusiano wa karibu na jamii/watu wanaozunguka migodi!Watoe basi kiasi fulani kijenge barabara ya geita- kahama kupitia kakola kwa kiwango cha lami nitawashukuru sana sana
Mkuu;Mambo yanayofanyika gizani ni vigumu kuyatolea maneno.
Naona umevijaza viwanda nyumbani. Elimu bure na mvua za kutosha, gari zipo Dubai zinakujaWauze tunuliwe Noah Zetu. Bahati nzuri nina watoto 7, mke house gal hivyo kwangu tutapaki Noah 10.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hela ndogo sana hiyo kwa nchi we dogo, usidanganyike na hizo figure, sisi tunaofanya analysis tuona tumepigwa tayariNi hizo ripoti ndizo zimekuwa msingi wa majadiliano na kufikia muafaka!
Unaweza kuziita kwa jina lolote upendavyo lakini ukweli wake ni kuwa Mkurugenzi wa Barrick Gold amesema thamani ya makontena yaliyoko bandarini Dar yana thamani ya dola milioni 280.
Unajua wamesafirisha makontena mangapi kabla ya haya kuzuiwa pale bandarini? Ukiyajua ndio utafahamu kama ripoti ya Prof Mruma na Ossoro ni proffessorial rubbish.