Mkurugenzi wa Dar 24 apatikana Kigamboni

Mkurugenzi wa Dar 24 apatikana Kigamboni

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Kamanda Mulilo amezungumza kuthibitisha hili kuwa kijana amepatikana kigamboni.

Alionekana hayuko vizuri wakampeleka hospitali, vipimo vikaonesha yuko vizuri, hana madhara yoyote.

Amesema alikuwa na watu anaofahamiana nao wakiwa na mazungumzo ya kibiashara, alipewa kinywaji, baadaye akapoteza fahamu, alivyozinduka walimzungusha kwa muda na baadaye kumuacha sehemu.


Haya maelezo yanatolewa hata hayaeleweki, kama vile yameungwaungwa. Nyie mnaonaje Wakuu?



Pia soma: Mkurugenzi wa Dar24 Media Maclean Mwaijonga apotea, hajulikani alipo
 
Habari ndio hiyo.nitawaletea kwa urefu.
Screenshot_20241102-223345_1.jpg
 
Watu wenye hasira kali wameamua kumsihi Mwenyezi Mungu asikae kimya zidi ya hali ijayo endelea .
Watu wanamsihi Mwenyezi Mungu kila mtu kwa imani yake afanye jambo na Dunia ipate mrejesho.
Mungu anawapenda sana watanzania atasikia dua na maombi ya watoto wake na kuuatendea kazi haraka.
 
Wapunguze kuteka raia wasio na hatia
!
Wapunguze au waache kabisa ?!
Kuteka ni kosa, ni kinyume na sheria.
Kuteka ni dhuruma ya haki za binadamu.

Hata kwa wenye hatia wanazo haki za kufikishwa kwenye vyombo vya dola mahakamani kwa kujibu wa Katiba waloapa kuifuata kwa kushika vitabu vitakatifu.
Na mahakama ndio inayoweza kumtia mtu hatiani baada ya kujiridhisha kwa ushahidi usio shaka.
 
Hiyo spirit ya utekaji inapelekea kushuka chini uraini na watu ambao maisha yamewatenda wanaweza kuiga huo ukatili wa kuteka na kuua.
Ni hatari mno.
Halafu inaleta simanzi na huzuni kwenye jamii miongoni mwa wananchi.
 
Back
Top Bottom