Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Media ya Dar24 kupitia ukurasa wake wa Insta wameweka tangazo la kupotelewa na Mkugenzi wao ambaye amatoweka toka tar 31/10/2024.
Wasiyojulikana wameamka tena?!
==
Dar24 Media inautaarifu umma kupotea kwa Mkurugenzi wake Maclean Mwaijonga.
Mara ya mwisho kuonekana ni wakati akitoka ofisini majira ya saa 11 jioni ya Tarehe 31. 10. 2024 DATAVISION INTERNATIONAL LTD Mikocheni karibu na Rose Garden.
Mkurugenzi wetu ambaye pia ni Mtendaji wa DataVision hana kawaida ya kutorudi nyumbani lakini mpaka sasa hapatikani.
Wakati akitoka Ofisini alikuwa na gari aina ya Toyota Prado nyeusi yenye namba za usajili T 645 DEE.
Tunaomba msaada wa Vyombo vinavyohusika na Wanahabari kwa pamoja zitusaidie kupaza sauti ili kumpata Kiongozi wetu na utakapomuona yeye au gari yake tupe taarifa kwa namba hii 0713249003.
====================
UPDATES...
UFAFANUZI WA DATAVISION INTERNATIONAL
Akizungumza na JamiiForums, Mkurugenzi wa Biashara wa DataVision INTERNATIONAL, MacMillan George amesema:
Hakuwa na kawaida ya kutorejea nyumba na kutopatikana kwenye simu, mkewe alivyoona hivyo usiku akaanza kutafuta ndugu na jamaa akiulizia, ilivyofika Asubuhi watu wake wa karibu pamoja na familia tukasambaa kwenye Vituo vya Polisi na Hospitali nako hatukufanikiwa kumpata.
Saa Tatu Asubuhi tukaenda kuripoti Kituo cha Polisi cha Oysterbay, wakasema ikipita Saa 24 turudi kwa ajili ya kufungua jadala lakini nao wakaanza jitihada za kumtafuta.
Muda mfupi uliopita Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni RCO amekuja na timu ya makachelo sita, baada ya kuchukua maelezo yetu nao wanafuatilia maeneo aliyopita baada ya kutoka kazini.
Pia Polisi wanaendelea kuwasiliana nao watu ambao Mwaijonga aliwasiliana nao siku ya mwisho kabla ya kupotea pamoja na kuangalia ‘footage’ zilizopatikana.
ALIKUWA NA UGOMVI AU MKWARUZANO NA MTU?
Polisi pia wametuuliza hizo taarifa kati yetu hakuna hata mmoja aliyekuwa na taarifa hizo au kujua chochote kama suala hilo lipo.
Mwaijonga sio mtu wa ugomvi, sio mtu wa kubishana na wala sio mfuasi wa mambo ya mpira kiivyo au Siasa labda kama kuna suala lake binafsi.
Pia, soma: Mkurugenzi wa Dar 24 apatikana Kigamboni