kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 11,190
- 24,620
Hii nchi inanuka uonevu kila mahali, sasa kosa la huyu ninini.....Samia suluhu utalipa kwa haya unayowafanyia watanzani....Jeshi la polisi la TZ ni jeshi la hovyo kuwahi kutokea duniani...
George Mahigu Seni, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala (Director of Finance and Administration) NIDA, alikamatwa na Polisi tarehe 15 Desemba 2025 akiwa Arusha kikazi, na kusafirishwa Dodoma kwa mahojiano. Baada ya tukio hili, kuhojiwa sasa ameambiwa na mkuu wake wa kazi asiende kazini bila hata kupewa barua yoyote rasmi. Sababu, alichapisha maneno yafuatayo kwenye WhatsApp group ya marafiki SHYCOM.
Maneno ya George Mahigu:
1.Siasa ndiyo kila kitu Mtani. Kinacho sababisha yote haya hata kama hatutaki ni ukosefu wa Siasa Bora, Uongozi Bora na Demokrasia thabiti. Huko kwingine kote maji kwenye kinu.
2.Kwamba ni sawa mwanamke aliyeogopa anapigwa risasi mgongoni?
Kwamba ni sawa kijana asiyekuwa na chochote mkononi kupigwa risasi?
Kwamba ni sawa kufanya mauaji ya halaiki kinyama namna ile?
Kwamba ni sawa kuwatoa vijana ndani wakiangalia mpira na kuwalaza chini na kuwapiga mmoja baada ya mwingine?
Siungi mkono watu kuharibu mali za umma na za binafsi na hata kufanya fujo tu.
Lakini kwa picha ambazo zilionekana siku ya tarehe 30 kabla hata hii ya CNN si sawa nguvu iliyotumika.”
3.Kaka!!!
Mtan usilete siasa ktk issue serious… mnakuwaje na shida ya maji km mna mto, Rufiji,
Ruvuma,Kagera,Ruvua,Rukwa. Ziwe Victoria,Tanganyika,nyasa,eyas,nk..mna mvua ya wastan kwa mwaka, baadhi ya maeneo maji yapo chini…justify hapo mtan?? ”