Mkurugenzi wa JKCI, Prof. Janabi asema magonjwa ya moyo yataongezeka kutokana na ukuaji wa uchumi

Usilete ubishi wa kitoto! Kitaa Watanzania wanaishi maisha yanayothibitisha tuna uchumi wa kati?

 
Usilete ubishi wa kitoto! Kitaa Watanzania wanaishi maisha yanayothibitisha tuna uchumi wa kati?
Ndio yanathibitisha
Baadhi ya Sababu Zangu Ndio hizo

Wewe Sababu Zako za Kukataa Ziko Wapi !?
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Mkuu hivi husikii vilio vya Watanzania kuhusu uchumi kuanguka? Unaishi chini ya jiwe hadi vilio vya Watanzania usivisikie? Fungua macho na akili yako Mkuu!



Ndio yanathibitisha
Baadhi ya Sababu Zangu Ndio hizo

Wewe Sababu Zako za Kukataa Ziko Wapi !?
[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kadri uchumi unavyokua na watu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa hayo kwa sababu watu wanakuwa na fedha za kununua vyakula vingi sambamba na matumizi ya usafiri binafsi” amesema Prof Janabi.
[emoji818][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827]
 
Miprofesa uchwara yenye miphd holders uchwara. Sasa kuna uchumi gani unakua?

mkuu maisha yakikuchanganya sana shika mkondo mwingine,vinginevyo kila sehemu utakuwa unapuyanga kama hapa.
 
Prof Janabi kaongea vizuri sana.

Ni either watu hawajamuelewa ama wameamua kupinga kwa makusudi.

Chukua mfano mdogo tu wewe kwanini kabla ya kupata kazi nzuri na marupurupu mbona ulikuwa mwembamba sana na sasa umekuwa bonge tena na kitambi juu.
Ukitafakari haya utamuelewa Prof kwa urahisi sana.

Uchumi unapokuwa(hajamaanisha kwamba uchumi umekua yeye kaongelea general rule) kwamba kwa kadiri uchumi wa nchi ama familia hata wa mtu mmoja mmoja unapokuwa watu wana switch kwenda kwenye

1.Vyakula hasa junk foods
2.Hawatotembea tena watatumia usafiri binafsi na hata wa jumuiya na wakati ule pengine angelitumia baiskeli ama kutembea kwa miguu.
3.watu hawatofanya mazoezi tena kwa kuwa wana nyenzo rahisishi.

Hii ni sawa na teknolojia inavyokuwa ndio
1.Maradhi ya kuambukiza yanapungua na kuzaliwa maradhi sugu kama kansa, presha, sukari na magonjwa ya moyo.
2.Watu kuacha kutembea na kupanda baiskeli na wanahamia kwenye magari, ofisini wanakaa kwenye viti vya kuzunguka siku nzima, majengo yamewekwa lift badala ya ngazi nk

Ukiwa unasoma maelezo ya Prof kishabiki ama kimrengo hutomuelewa ila kazungumza jambo la ukweli kabisa.
 
Asilimia zaidi ya 80 ya watanzania wako vijijini wanalima kwa jembe la mkono daily, sasa hebu nisaidie hayo maisha mazuri kutokana na uchumi kukua yako wapi? Hivi hao wati wa mijini ambao ni asilimia 20 au less Wana magari wote, mishahara mikubwa etc?
 
Ni sahahi, nahii inatokana na life style, sababu suala la Balance Diet TZ halipo kabisa, watu watazidi kubugia misosi inayohatarisha kupata Presha ya kupanda, Kisukari, kansa nk
.,.Kuna ukweli wa namna Fulani katika. Hili. Angalia Kasi ya Watu kula Chipsi Kuku wa Kisasa, ambavyo vinapikwa kwenye Mafuta matupu ambayo unapovila yanaishia mwilini mwako, angalia Kasi ya watu kula Baba, kitimoto, mkate kwenye Blue and na Kadhalika.

Jiulize we we mwenyewe binafsi...Mara ya mwisho ni lini ulikunywa chain kwa mihogo ama viazi vitamu vya kuchemsha???

Mara ya mwisho ni link ambapo ulifanya Nazi ndogo tu ya kukitoa jasho, kama kupanda ngazi had I ghorofa LA Tatu tu ilipo Ofisi yako na ukaacha Lifti??
Jiulize.....
 
 

Kwa maelezo ya prof kasema magonjwa ya moya yanaongezeka

Hata kama ni wa 20 tu wapo mjini kama mwanzo watu watano tu ndo walikuwa wanaugua magonjwa ya moyo na sasa wanaugua Watu 9 huoni kama kuna ongezeko hapo?
 
Miprofesa uchwara yenye miphd holders uchwara. Sasa kuna uchumi gani unakua?
Kashindwa kuelezea vizuri mbona uchumi ukikua ndo watu wanakua na uwezo wa kua na uwezo wa kununua vyakula vizuri kutokua na msongo wa mawazo kufanya mazoezi .
Angesema labda life style ingeeleweka vizuri

Naona kauli imetoka ili kufurahisha awamu
 
Angesema life style maana kuna wenye hela na wanazingatia sana balance diet...matunda kwa sana mbogamboga na mazoezi sana
 
Kashindwa kuelezea vizuri mbona uchumi ukikua ndo watu wanakua na uwezo wa kua na uwezo wa kununua vyakula vizuri kutokua na msongo wa mawazo kufanya mazoezi .
Angesema labda life style ingeeleweka vizuri

Naona kauli imetoka ili kufurahisha awamu

Awamu ipi tena? Si tulishamshukuru Mungu kwa kutusikia na kutuondolea!
 
Angesema life style maana kuna wenye hela na wanazingatia sana balance diet...matunda kwa sana mbogamboga na mazoezi sana
Wewe mwenyewe ushasema "kuna wenye hela wanazingatia" kumbe ni kundi fulani la wenye hela ndio linazingatia. Tunarudi palepale maana mwenyewe hakusema wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…