TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

TANZIA Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabasi ya Sauli, Solomoni Mwalabhila afariki dunia

Pale Tukuyu ushirika na mmiliki wa landmark aliwahi kuishia jamaa anaitwa sauli,alihusika Sana kuwanadi akina professa mwakyusa kipindi Niko Tukuyu,je siyo huyu aliyefariki?
 
UMenichekesha sana ila binaadamu wana katabia ka wivu its natural
Watu wana chuki na matajiri kupita kiasi.
Akifa tajiri hapa jf kila mmoja anakuja kashfa yake
Tuna chuki halisi za kiafrika, wengi hapa hawaamini kama mtaani kuna fursa za kutafuta pesa.
Watu wanaamini utajiri unapatikana kichawi, magendo au madawa ya kulevya, imani ambayo siyo sahihi.
 
NI MAJONZI MAANA KRISTO KATUFUNDISHA HURUMA HAYO YA MALI ZA KICHAWI SIJUI KUKU KUDONOA MAHINDI SISI HATUJUI MAANA NI ISHU ZA ROHONI TUSIHUKUMU.

NENO MOJA NI TUMEJIANDAAJE SISI TULIO HAI

BWANA YESU AWAPE NGUVU FAMILIA YA MAREHEMU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU
 
Tumepokea taarifa ya ajali ya gari ndogo ambapo mmiliki wa Mabasi ya kampuni ya Sauli Luxury Solomoni Mwalabhila amefariki dunia kwenye ajali hiyo. Tunatoa pole sana kwa Kampuni ya Sauli Luxury.

Ajari ya barabarani imeondoka na roho ya mmiliki wa mabasi ya Sauli Luxury siyo mbali sana na ilipopata ajari basi yake mapema mwaka huu Kibaha na kuwaka moto na yeye pia mmiliki ajari imemwondoa maeneo ya Mlandizi leo hii asubuhi akiwa na gari binafsi

Atakumbukwa kwa kuleta upinzani wa huduma na kufikisha abiria kwa haraka kampuni zake kwa wasafri wa nyanda za juu kusini.

Hasa kwa sisi wanazi wa Scania tutamkumbuka sana mwamba kwa kuziheshimisha Scania road.

Rest in peace Mwilabila Sauli


Pole kwa familia;aliisha imarisha biashara yake na kuteka soko la usafiri wa mabasi Mbeya-Dar.Haya mabasi ni maarufu kama Abood ya Morogoro au adventure ya kigoma-Dar.kwamba mpaka yajae kwanza yenyewe ndiyo mabasi mengine yatapata abiria.Mfanyabiashara wa pili mkubwa ninayemfahamu kutokea mbeya kufa kwa ajali ya Gari ndogo baada ya Yuke Kisangani mwenye maduka ya spares kariakoo.
 
Hiv serikali haijawahi kuwaza kuipanua Morogoro road at kila mwaka km 30 tu...mwaka huu mnaishia mlandizi, ujao chalinze, ujao Bwawani, mwingine mikese, mwingine Morogoro...

Wamaweza ila hawajaamua tu
Wataamua lini mkuu?! Tunapoteza Nguvu Kazi Nyingi
 
Hiv serikali haijawahi kuwaza kuipanua Morogoro road at kila mwaka km 30 tu...mwaka huu mnaishia mlandizi, ujao chalinze, ujao Bwawani, mwingine mikese, mwingine Morogoro...

Wamaweza ila hawajaamua tu
Mi pia nina mawazo kama ya kwako.
Barabara ya Morogoro imezidiwa sana.
Madereva wengi hasa wale wa masafa marefu wanaendesha wakiwa wamechoka sana.
Lakini mara kwa mara namsikia ndugu Kafulira anapigia debe kampuni binafsi zijenge barabara za aina hiyo kwa kulipia.
Kwanini tulipie wakati tuna serikali, inayokusanya kodi zetu.
Serikali ijenge hata km 50 kwa mwaka.
 
Haya maisha!! Yaani unapamba unatafuta mali mambo yananyooka ghafla unatwaliwa unaacha Kila kitu.
Roho ya marehemu ipate rehema kwa Mungu apumzike kwa amani
 
IMG_20240804_153658.jpg
 
Hapo kweli lazima wakusumbue na wameona hela unayo lazima wakuchekeche kila hatua
Na hilo tukio sio moja, yupo rafiki yangu naye miezi kama mitatu hivi iliyopita gari yake ilidakwa ikitorosha madini.

Japo yeye hakuwepo kwenye scene ila aliwekwa sello, alikuja kutoka lakini mpaka leo hiyo gari yake bado hajarudishiwa.
 
Back
Top Bottom