Prof Koboko
JF-Expert Member
- Aug 15, 2020
- 350
- 2,550
Kila ninapomsikiliza huyu Mkurugenzi napata wasiwasi kabisa na uwezo wake wa kuifanya tume ya uchaguzi ikafanya haki. Kwanini isichukuliwe kuwa yeye ndiye chanzo cha hizi engua engua?
Huyu si watu wengi wanamtuhumu kuwa ni kada wa CCM? Si ndio kuna tuhuma kuwa alikua kwenye list ya Wakurugenzi Makada wa CCM iliyoandaliwa na Bibi Chacha Wangwe na Fatma Karume?
Kwani wagombea kutunishiana misuli na kukejeliana majukwaani nyakati za kampeni si kawaida?
Kwenye uchaguzi huwezi kupanga kusikiliza unayoyataka wewe, hakuna kitu cha namna hiyo labda ugombee wewe pekee yako.
Huyu bwana ajifunze kwenye tume za kina nani Damian Lubuva. Alitukanwa sana mzee Lowassa lakini hatukuona mtu akiitwa kwenye kamati za maadili.
Nimemsikiliza mara nyingi mwenye vikao vyake na vyombo vya habari inaonekana ni mtu asiyekipenda kabisa CHADEMA na mgombea wake.
Huyu tusipoangalia anàweza kuleta matatizo makubwa nchini siku za usoni. Awe makini sana NEC ni chombo kinachotazamwa na Jumuiya zote za kimataifa, asiongee kama bado yupo Arusha DC.
Amesikika akisema kila kila wakati kuwa tume haishinikizwi kutoka nje, hii kauli inalenga nini hasa? Ni nje ya wapi inataka kuishinikiza tume na kupitia nani?
Nasikitishwa na upinzani wa nchi yetu kwanini wasingeshinikza huyu bwana aondolewe kwenye tume kabla ya uchaguzi? Wanamuamini kwa kiasi gani kutokana na kauli zake hizi?