Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa NEC, Dkt. Mahera apumzishwe haraka, anaweza kutupeleka kwenye matatizo makubwa

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa NEC, Dkt. Mahera apumzishwe haraka, anaweza kutupeleka kwenye matatizo makubwa

Kama raia huru wa kitanzania naomba kutoa ushauri kwa vyama vyote vya siasa nchini hasa upinzani, kwakua huyu mkurugenzi wa NEC anaonesha mahaba ya wazi wazi kwa chama tawala CCM, toeni tamko la pamoja kutoa masaa 72 kwa mamlaka kumuondoa huyu mkurugenzi na lasivyo mchukue hatua stahiki.

Records zinaonesha kua huyu bwana alikua ni mwanachama wa CCM na bado anaendeleza mahaba yake. NEC ni Chombo senstive sana siyo cha kubebwa bebwa tu tusije tukaishia pabaya.

Naomba kuwasilisha!
 
Mkuu leo Magufuli asingekuwa rais.. tulishaahidiwa IST zile za makinikia, achilia mbali laptop.. lakin tupo tunafanya kazi. Kuna 50m kila kijiji lakini kwenye mikutano yetu wala yake hatujawahi kumuuliza. Maana alichomekea tu.

Tusiwe ni mihemko hemko tu ya mambo madogo, wakurugenzi kuitwa dodoma hata kama ni kweli wale si waajiriwa wa serikali,kama rais anaongea na wafanya kazi wake tatizo ni nini?
Tatizo ni kipindi hiki cha uchaguzi.
 
Sio kwamba inasemekana, huyo jamaa ni kada kindaki ndaki wa CCM.
Amempigia kampeni Magufuli humohumo: “Watanzania wanahitaji Rais anaejali maisha yao kama ujenzi wa barabara na miundo mbinu si Rais atakaeuza madini yao”.
 
Hii tume ambayo msingi wake mkubwa ni double standards...Tundu Lissu asiende tuone kitakochofanyika. Hii tume ambayo yenyewe haina maadili...ninewupe kama pamba. Wametoa hukumu gani kwa wagombea ubunge na udiwani wa chadema kwa muda huu wote. There are all working in tandem with all the deds to ensure that winner is Magufuli...
NEC kwa Lissu itazidi kujidhalilisha tu. Lissu ni akili Kubwa.
 
Hajishtukii mwenzake Jaji Kaijage kajikalia kimya tu yeye ndo analopoka hovyo. Keshaingia kwenye records za wenye dunia na saivi wanamfuatilia 24/7. Andelee kujifanya mjinga hajui kinachokuja mbele yake

Ni analopoka au anaropoka?
 
Tume walishampanga mshindi wao wa mfukoni Sasa hili nyomi na muamko mpya nchi nzima wa kumkataa shetani na kazi zake zote inawaumiza Sana vichwa.

Mwaka huu Safari Ni mbili kwenda Chato au The Hague, Lisu sio Lowasa.
 
Msinikumbushe 2012 mambo yaliyoleta vurugu Kenya hadi kuzaa Katiba yao mpya, Mkurungezi anaulizwa nani kashinda URAIS yeye anasema hana uhakika kama ni Raila ama Uhuru Kenyatta!!
 
Mahera kachemka mapema sana,ashapwaya hafai kuendelea kushikilia nafasi hiyo.
 
Ila mkurugenzi kajaaa upepo mno kama vile yeye ni mgombea wa urais
Huenda hayo ni maelekezo aliyopokea kwa sababu amekuwa na pressure sana na ukimwangalia vizuri utagundua kashindwa kubalance maelekezo na nafasi yake katika Tume, ametoka off-road kabisa na kujikuta ameivaa nafasi ya mgombea. Ni hatari sana.
 
Kila ninapomsikiliza huyu Mkurugenzi napata wasiwasi kabisa na uwezo wake wa kuifanya tume ya uchaguzi ikafanya haki. Kwanini isichukuliwe kuwa yeye ndiye chanzo cha hizi engua engua?

Huyu si watu wengi wanamtuhumu kuwa ni kada wa CCM? Si ndio kuna tuhuma kuwa alikua kwenye list ya Wakurugenzi Makada wa CCM iliyoandaliwa na Bibi Chacha Wangwe na Fatma Karume?

Kwani wagombea kutunishiana misuli na kukejeliana majukwaani nyakati za kampeni si kawaida?

Kwenye uchaguzi huwezi kupanga kusikiliza unayoyataka wewe, hakuna kitu cha namna hiyo labda ugombee wewe pekee yako.

Huyu bwana ajifunze kwenye tume za kina nani Damian Lubuva. Alitukanwa sana mzee Lowassa lakini hatukuona mtu akiitwa kwenye kamati za maadili.

Nimemsikiliza mara nyingi mwenye vikao vyake na vyombo vya habari inaonekana ni mtu asiyekipenda kabisa CHADEMA na mgombea wake.

Huyu tusipoangalia anàweza kuleta matatizo makubwa nchini siku za usoni. Awe makini sana NEC ni chombo kinachotazamwa na Jumuiya zote za kimataifa, asiongee kama bado yupo Arusha DC.

Amesikika akisema kila kila wakati kuwa tume haishinikizwi kutoka nje, hii kauli inalenga nini hasa? Ni nje ya wapi inataka kuishinikiza tume na kupitia nani?

Nasikitishwa na upinzani wa nchi yetu kwanini wasingeshinikza huyu bwana aondolewe kwenye tume kabla ya uchaguzi? Wanamuamini kwa kiasi gani kutokana na kauli zake hizi?
Ambaye hamtaki Mkurugenzi Dk. Mahera aache kugombea.
 
Back
Top Bottom