Mkurugenzi wa Rita Tunaomba uchunguzi cheti cha kifo No 100000203415(MOSHI)/ tangazo la kifo BD 0668249(Dar)Marehemu kafia dar kaishi dar +mirathi mo

Poleni sana.

Kwa sasa, japo hujazungumzia, inawezekana huyo bwana alikwishateuliwa na Mahakama kuwa msimamizi wa mirathi. Kama jibu ni NDIYO, basi cha kufanya ni rahisi tu, ni kufanya maombi mahakamani ya kuomba utenguzi wake kama msimamizi wa mirathi. Sababu za utenguzi ni kukosa uaminifu na kupata usimamizi wa mirathi kwa udanganyifu.

Nani afanye hayo maombi ya kupinga uteuzi? Mtu yoyote yule mwenye maslahi na mali za marehemu, hapa anaweza kuwa mtoto yoyote au watoto wote kwa pamoja. Wataomba jamaa atenguliwe na wawekwe wao, au wawekwe wao pamoja na huyo msimamizi au awekwe KABIDHI WASII MKUU WA SERIKALI (Administrator General).

Suala la kuweka caveat ni muhimu, ingawa kisheria hata msipoweka caveat, jamaa hataweza kuuza mali (viwanja vilivyosajiliwa) pasipo uwepo wa fomu ya warithi kukubali kuuza kiwanja hicho (Heir Consent form) ama sivyo aghushi saini zao, hata mnunuzi atakua mjinga kununua kiwanja bila muhtasari na kuona ridhaa ya wanufaika wa mirathi (warithi).

Kwa kuwa haya ni mambo ya kisheria ni muhimu kuyashughulikia kisheria kuliko kiutawala (administratively) kama hivi. Wasiliana nami kwa 0713368153 nikupe huduma ya kisheria warithi wapate haki zao.

Pia soma andiko langu hili kuhusu mirathi na wosia, Kwa nini mtoane Roho kwa mali alizoacha baba? Ijue Sheria ya MIRATHI, WOSIA na Usimamizi wa mali zitokanazo na Mirathi
 
-marehemu amekufa na natural death
na sio kansa ya kibofu
kama tangazo la kifo la kinondon hospitali linavyosoma
Hapa hakuna udanganyifu uliofanyika. Natural death ni kifo chochote kilichotokea kwa ugonjwa, ghafla nk pasipo sababu za nje. Ikiwa mtu atafariki dunia kwa ajali, kuuawa basi sababu ya kifo itakuwa ni UNNATURAL, maana sio kifo cha njia ya kawaida. Hawaandiki ugonjwa wa marehemu au details za kilichosababisha kifo katika cheti cha kifo bali katika Tangazo la kifo. Kwa kuandika NATURAL, RITA wapo sahihi mkuu.
 
well advs ntakucheki mkuu nikishakutananao jtatu asbh
 
Ni mahakama tu ndio inaweza kusema Fulani hana kesi ya kujibu.

Kujibu si lazima uwe mshtakiwa, unaweza kuwa shahidi muhimu wa kuthibitisha forgery.

Tena inatakiwa barua atakayoandikiwa DCI copy ipekekwe Takukuru DSM upanga upande wa Ilala.
Mkuu thx much for advs Jtatu tunaanza naki kote naamini Mungu atawasimamia
 
Kwel Jf kisima Cha maarifa 🤓 naona nondo zinashushwa balaa thanks 🙏🙏
wako wengi wanateseka haswa na hizi mahakama ndogo hawana msaada pa kuanzia unaishia msimamzi kuenjoy moaka anakufa ndio maana kyna kabila moja yaan uinyeshe dalili ya dharau mali za marehemu miezi mitatu mingi unajifia mwenyewe wala awakugusi
 
Kuna umuhimu wa kuanza kuandika mambo yetuu mapema jamani msitese watoto kama hivi mmmh ....
 
naweza kuwa sikupingi
cha mama yangu wameandika ugonjwa sasa pengine n vip wa huko,,...
 
Hili Suala ni simple sana na huko kwa mkurugenzi wa RITA unazunguka bila ulazima. Tafuta mwanasheria mzuri hapo Moshi nq ushahidi/vielelezo mkalimalize mahakamani. Huyo msimamizi atasimamishwa/ kutenguliwa na kisha taratibu zitaanza upya.
 
Caveat ina muda gani kuisha?Au haina mda kuisha mda wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…