Kama upo serious kuwasaidia Watoto wa marehemu peleka hii barua makao makuu ya Polisi Dar kitengo cha fraud, peleka barua nyingine kwa DCI.
Kisha nenda wizara ya Ardhi Dar omba kuonana na kamishna wa Ardhi, mueleze hii scenario yote na mumpe maombi ya kufunguwa CAVEATE.
Hiyo CAVEAT ikitolewa hakuna Nyumba wala Ardhi ya marehemu inayoruhusiwa kuuzwa mpaka mkae sawa.
Mwisho kaeni kikao cha familia badilisheni Msimamizi wa mirathi andaeni muhktasari pelekeni hiyo Mirathi mahakama ya juu pale Temeke Chang'ombe one stop center, kuna majaji kabisa pale.