Mkurugenzi wa Shell: Mgogoro wa nishati utakuwa kipimo cha umoja wanachama EU. Bei yapanda mara 30(3,000%)

Mkurugenzi wa Shell: Mgogoro wa nishati utakuwa kipimo cha umoja wanachama EU. Bei yapanda mara 30(3,000%)

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mkurugenzi wa Shell, Ben Van Beurden ameitahadharisha Ulaya inaweza kuhitaji kugawanya nishati kwa miaka kadhaa kwani mgogoro uliopo una kila dalili ya kudumu zaidi ya kipindi kimoja cha baridi.

Maoni ya Mkurugenzi huyo anaeongoza kampuni kubwa zaidi barani Ulaya ya mafuta na gesi yanafatia baada ya Urusi kupunguza zaidi kiwango inachopeleka Ulaya na kufanya bei ya gesi kufikia kiwango cha juu zaidi kwenye historia na kuhatarisha mdororo wa uchumi.

"Mgogoro wa nishati utakuwa kipimo cha umoja wanachama EU ambapo Serikali zitalazimika kuchagua jinsi ya kufanya viwanda muhimu viendelee kuzalisha" Alisema Van Beurden

Serikali za Ulaya zinakabiliwa na janga la nishati kutokana na vita ya Urusi na Ukraine kutokana na Urusu kupunguza gesi ambapo wanasiasa wa Ulaya wanatuhumu hatua hiyo kama 'Kuifanya Gesi silaha'

Bei ya gesi imepanda kwa kasi wiki iliyopita na kufikia Euro 343 kwa megawatt, wanyabiashara wanajitahidi kuwahi gesi wakati Ulaya inaelekea kipindi cha baridi.

Bei hiyo ni zaidi ya mara 30(Ongezeko la 3,000%) ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita na zaidi ya mara kumi ya bei zilizopo Marekani kwa sasa.

CHANZO: Financial Times
 
Back
Top Bottom