Mkurugenzi wa taasisi ya saratani ya Ocean road ataja kuzaa watoto wachache kama chanzo cha saratani

Mkurugenzi wa taasisi ya saratani ya Ocean road ataja kuzaa watoto wachache kama chanzo cha saratani

Mung Chris

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
3,474
Reaction score
4,007
Imeelezwa kuwa kuzaa idadi ndogo ya watoto ni chanzo cha ugonjwa wa saratani ya matiti kwa wanawake.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk Julius Mwaiselage ameyasema hayo leo wakati akielezea mafanikio ya taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne.

Amesema aina hiyo ya saratani inashika nafasi ya pili kwa kuwa na wagonjwa wengi huku waathirika wengi wakiwa katika mkoa wa Dar es Salaam.

Amesema wanawake wengi wa Dar es Salaam wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa huo kutokana na kuzaa watoto wachache tofauti na ilivyo kwa wanawake wa mikoani.

“Ukizaa watoto wengi wakanyonya kuna uwezekano wa kupunguza hivyo vichocheo, huku mjini wanawake wako hatarini zaidi kwa sababu wanazaa watoto wachache,” amesema.

Dk Mwaiselage amezitaja sababu nyingine kuwa ni kutonyonyesha kwa muda unaostahili, matumizi ya pombe, unene uliopitiliza na kutofanya mazoezi.
*******

Nimejiuliza tena: Ni nani atakaye jitokeza kutubainishia chanzo cha mtu kupatwa na ukichaa kuwa unatokana na maisha mgumu hivyo kukosa fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto na kuwapa mahitaji muhimu na ya msingi, mwanamke anashauriwa azae watoto wakutosha kuepuka chanzo cha saratani ila badae hatakwepa kuwa anaongea mwenyewe barabarani kwa kukosa mahitaji muhimu ya familia yake.

Nini kifanyike kuepuka saratani ya matiti na kuepuka kuongea peke yako barabarani kama kichaa.
 
Endapo watoto wachache watakuwa 3 basi nafikiri kuna haja ya kuwanyonyesha hadi wafikie miaka 2 na nusu swala la matiti kulala kama socks lisikusumbue sana maana unakwepa saratani ya matiti.
 
Walau 5. ila nahisi huyu bwana anataka awatibue kina dada huku akiwa na agenda ya siri ya kutaka waijaze dunia, si unajua tena lazima awaogopeshe kidogo. wengine wasipoambiwa na daktari wanakuwa wabishi sana.
Na wengi wanaanzia wangapi? Aruba?
 
Walau 5. ila nahisi huyu bwana anataka awatibue kina dada huku akiwa na agenda ya siri ya kutaka waijaze dunia, si unajua tena lazima awaogopeshe kidogo. wengine wasipoambiwa na daktari wanakuwa wabishi sana.

Mimi siamini kama kuzaa watoto wachache ndo moja ya sababu ya hiyo saratani!
 
Huyu anamuunga mkono magufuli kuzaa watoto wengi kwa kutumia elimu yake ya udaktari, CCM inataka kuharibu nchi
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Back
Top Bottom