PreGE2025 Mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogosa aahidi milioni 10 kwa ukarabati wa Kanisa Parokia ya Kome

PreGE2025 Mkurugenzi wa TRC Masanja Kadogosa aahidi milioni 10 kwa ukarabati wa Kanisa Parokia ya Kome

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
418
Reaction score
550
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa ameahidi kutoa milioni 10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Muhashamu Askofu Flaviani Katindi Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita, kwa kushirikiana na Baba Paroko Padri Japheth Masalu wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome kwa ajili ya ukarabati wa jengo la parokia hiyo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

1743578144572.png
 
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa ameahidi kutoa milioni 10 kwenye harambee iliyoandaliwa na Muhashamu Askofu Flaviani Katindi Kasala wa Jimbo Katoliki la Geita, kwa kushirikiana na Baba Paroko Padri Japheth Masalu wa Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima Kome kwa ajili ya ukarabati wa jengo la parokia hiyo.


Chanzo cha mapato hayo ni wapi hasa?

Katika nchi hii kuna ULAZIMA mkubwa sana kwa Sasa wa kubadilisha Katiba ya nchi pamoja na Sheria zingine zote kabisa na kuweka Vifungu vya Sheria vitakavyowazimisha Watumishi wa Umma wote kabisa kutangaza hadharani kila Mwaka kwenye Magazeti ya Serikali (Government Notices) kuhusu Mali zao zote kabisa wanazomiliki, Vyanzo vya Mapato yao, Matumizi ya Mapato yao kwenye masuala kama haya ya kuchangia harambee, na kuweka Wazi kabisa kuhusu Viwango vya Fedha za Kodi walizolipa kwa Mwaka wote.

Hii itasaidia sana katika kuweka wazi masuala ya Uadilifu wa Wahusika kuhusu Rushwa sambamba na kutengeneza Mazingira ya Uwazi katika Utendaji kazi huko kwenye Serikali.

Yawezekana kabisa Mambo kama haya ya kuchangia harambee nyuma yake kuna masuala ya Rushwa, Ufisadi, na biashara haramu ya Utakatishaji wa Fedha
 
Pesa za harambee wanazitoa wapi?
Unapewa kadi moja yenye fomu ukachangishe kwa marafiki zako

Hujawahi shiriki harambee wewe?

Mshamba wa Harambee wewe

Yeye kwenye fomu aweza changia milioni moja hizo zingine akachangisha watu wengine lakini anahesabika yeye ndie katoa
 
Mshenzi tu huyu Kuna watu wanadai mamilioni trc wastaafu mpaka wanakufa hawajawahi kulipwa chochote Leo masanja anajidai kusaidia makanisa
 
Yawezekana kabisa Mambo kama haya ya kuchangia harambee nyuma yake kuna 'mchezo mchafu' wa masuala ya Rushwa, Ufisadi, na biashara haramu ya Utakatishaji wa Fedha
Mwambini Lisu wenu aache ubahili hizo hela za tonetone aende achangie huo ujenzi wa kanisa

Hawezi kupiga yowe tu ohh maaskofu hawaniskilizi nikiongea

Wakati maaskofu wakiongea kuwa tuna harambee anajifanya kuziba masikio kama hasikii kabisa anakuwa kiziwi ghafla

Anataka wao wamsikilize yeye ila yeye asiwasikilize wao ikiwemo harambee zao

Kwanza hivi huko kwenye tone tone.Lisu kachangia shilingi ngapi?
 
Unapewa kadi moja yenye fomu ukachangishe kwa marafiki zako

Hujawahi shiriki harambee wewe?

Mshamba wa Harambee wewe

Yeye kwenye fomu aweza changia milioni moja hizo zingine akachangisha watu wengine lakini anahesabika yeye ndie katoa
Kwanini asiwachangishe watu ili wafidie hasara iliyoingiza shirika lake?
 
Mashirika yanayoitia hasara Serikali bora yangeendeeshwa na Interns tu. Unaitwa mkurugenzi wa super loss making machine 😂😂
 
Ataenda kutoa hizo hela ila atasema Mama ndio wa kumshukuru kwa kutoa hizo fedha.

Kwa kifupi, lazima Mama atatajwa na kusifiwa wakati wa kukabidhi hizo hela.

Mpango mkakati.

Kampeni zinaendelea
 
Wapendwa abiria wa Treni ya TRC, tunakaribia steshenii ya kisangiro, abiria mnaoshukia steshenii ya kisangiro mjiandae kushuka na tunawatakia kila la Khair
 
Back
Top Bottom