Hivi huyu aliokotwa wapi na kupewa hiyo nafasi? Tume ilihitaji mtu kama Prof Assad,
Wanunuzi na akina nani na wakishayanunua wanayauza wapi? Je, makampuni yanayochimba madini kama vile Barrick, Buzwagi, etc yanamilikiw na nani?kila mkoa una soko la madini ambapo wachimbaji hupeleka kwa ajili ya kuuza, haya masoko aliyaanzisha JPM baada ya sakata la makinikia
Kawadanganye wazee wa mwaka 47 huko enzi za azimio la ArushaHuwezi kuwa na uraia pacha hapa Tanzania. Ana passport ya ulaya huyo
Kwani mgombea wa chama changu ametoa tuhuma gani? Mkurugenzi asituoneeHuyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?
Mkurugenzi wa NEC anaposema kuwa watanzania hawataki mtu atakayetorosha madini nje, kwani inaihusu nini NEC?
Kweli nimeamini hawa NEC siyo wa kuwachekea hata kidogo. Hata hii engua ya wagombea wa upinzani inafanywa kimkakati na inaonekana wazi wazi.
Magufuli amevuruga mifumo mingi huru ya maamuzi. Hii nchi inakoelekea siko hata kidogo.
View attachment 1583150
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Huyu jamaa ana vituko.... yeye kazi yake ni kuwa refa wa mtangange, sio kusema mashabiki wanataka kuona magoli na kanzu
Mkuu nchi hii inaendeshwa KIDIKTETA sana we acha tu!Ukiona mtu yoyote ni mteule wa Magufuli, ujue moja kwa moja anafuata atakacho na sio sheria zitakavyo. Na ukienda kinyume tu cha matamanio yake, hata kama unasimamia sheria lazima akuondoe.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!
Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao
Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa
Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera
==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC
Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.
Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.
Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.
Mkuu nchi hii inaendeshwa KIDIKTETA sana we acha tu!
Lissu ajikite kwenye sera sio vibweka
Lissu kuongelea swala la wafanyakazi kwanini limuume kama sio kada huyu?