Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Hivi huyu aliokotwa wapi na kupewa hiyo nafasi? Tume ilihitaji mtu kama Prof Assad,

Ukiona mtu yoyote ni mteule wa Magufuli, ujue moja kwa moja anafuata atakacho na sio sheria zitakavyo. Na ukienda kinyume tu cha matamanio yake, hata kama unasimamia sheria lazima akuondoe.
 
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?

Mkurugenzi wa NEC anaposema kuwa watanzania hawataki mtu atakayetorosha madini nje, kwani inaihusu nini NEC?

Kweli nimeamini hawa NEC siyo wa kuwachekea hata kidogo. Hata hii engua ya wagombea wa upinzani inafanywa kimkakati na inaonekana wazi wazi.

Magufuli amevuruga mifumo mingi huru ya maamuzi. Hii nchi inakoelekea siko hata kidogo.

View attachment 1583150
Kwani mgombea wa chama changu ametoa tuhuma gani? Mkurugenzi asituonee
 
Ukiona mtu yoyote ni mteule wa Magufuli, ujue moja kwa moja anafuata atakacho na sio sheria zitakavyo. Na ukienda kinyume tu cha matamanio yake, hata kama unasimamia sheria lazima akuondoe.
Mkuu nchi hii inaendeshwa KIDIKTETA sana we acha tu!
 
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!

Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa

Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera


==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC

Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.

Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.

Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.

Asimfundishe mgombea cha kusema kwenye kampeni wala asianze kupigia kampeni CCM. Abakie na huo ukada wake kila mtanzania anayejitambua anajuwa kwamba tume inapendelea CCM tangu mwanzo kabisa
 
TUME ya uchaguzi haina mamlaka ya kisheria ya kumuita mgombea katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa, Mkurugenzi wa Uchaguzi anapozungumza mamlaka ya kisheria inapaswa amalize kwa kutaja kifungu kamili na jina la sheria husika inayompa yeye au TUME mamlaka hayo.

Kamati ya Maadili ya Kitaifa, TUME ina uwezo wa kwasilisha malalamiko tu mbele ya kamati na sio kumuita mgombea, hii ni kwa mujibu wa aya ya 5.4 ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na madiwani ya mwaka 2020.

Screen Shot 2020-09-28 at 10.05.00 AM.png


Kwa mujibu wa aya 5.2.2 ya Maadili ya Uchaguzi 2020, Kamati ya Kitaifa inaundwa na watu wengi ikiwa na mjumbe wa kutoka TUME ya uchaguzi ambaye ndiye mwenyekiti wa Kamati, sasa bwana Mahera amejitokeza katika vyombo vya habari kama Mkurugenzi wa Uchaguzi na sio mwenyekiti wa kamati ya Maadili ya Kitaifa (kama ni mjumbe huko), ambayo inafanya jambo zima kuwa batili. TUME ina idara ya Sheria, ni aibu kufanya madudu ilhali watu wanalipwa mshahara na wanashindwa kushauri ipasavyo, huku ni kuchezea kodi zetu

Screen Shot 2020-09-28 at 10.05.27 AM.png
 
Mimi kimsingi sikubalian na matamshi ya mkurugenz wa NEC kwasababu tayari ameonyesha dalili ya upendeleo fulani kwenye uchaguzi huu,kwani yeye amekuwa mgombea tayari? Na ni wa chama gan? Amejuaje kuwa kuna mgombea atapeleka madin nje ya nchi? Ni vizuri wazee wa chi hii wakaa pamoja na huyu mtu wakamkemea kwa matamshi yake haya wala haya afya kwa mustakabali wa uchaguzi huu.tayari ana personal interest kwa chama chake.naomba tusifike huko tafadhalini kabisa tuwe huru na haki kwa vyama vyote.
 
halafu kuna mtu anaamini hii ni tume huru ?
Tume huru inafanya kampeni za ccm hadharani?
Ndio maana tunasema kila siku hakuna tume huru ya uchaguzi Tz, hii tuliyo nayo ni Nec-ccm kama zilivyo; uvccm au uwt
 
Kazungumza kama nani, mpiga ramli, mfanya research (watanzania wanataka nini?), mwanachama wa chama fulani, mpiga kampeni, mpiga debe au msimamizi wa uchaguzi ?, Na amefanya uchunguzi kwamba kuna watu watauza madini nje ?, na kwa sasa hayo madini hatuyauzi tunayala au tunayatumia wenyewe?
 
Back
Top Bottom