Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Uchaguzi 2020 Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC: Watanzania hawataki mtu atakayeuza madini yao kwa wageni nje

Mkurugenzi waTume ya uchaguzi hawezi kutusemea watanzania, eti Watanzania hawamtaki mtu atakayeuza madini yetu nje...... alikutana wapi na hao Watanzania?

Si ndio hapo sasa, kwani mpaka sasa yanauzwa wapi kama sio nje. Amepanick mpaka anajichanganya. Hiki kikao cha hizi siku mbili, naona Magufuli kawatishia ile mbaya, ndio maana Polepole na yeye jana katokea anaongea kwa jazba ile mbaya.
 
Lissu ajikite kwenye sera sio vibweka
Mkurugenzi mwenyewe ndio huyu?
IMG-20200928-WA0002.jpg
 
[emoji1][emoji1] hata wakati wa ukoloni hatukua na tume ya hovyo kiasi hiki.

Tatizo la mahera ni ushamba..
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, amesema watanzania wanataka Afya iliyoimarika, barabara nzuri, miradi ya umeme, elimu bora hawataki blah! Blah!

Amesema watanzania hawataki viongozi watakaochukua madini yao na kwenda kuyauza kwa wageni nje, watanzania wanataka viongozi watakaotetea madini yao

Ameyasema hayo alipokuwa anazungumza kumuandikia barua Tundu Lissu ili kutoa maelezo dhidi ya tuhuma za uongo anazotuhumiwa kuzitoa

Amesema Tundu Lissu amekuwa akitangaza matusi, tuhuma na kudanganya wafanyakazi badala ya kutangaza sera


==
YALIYOZUNGUMZWA KWENYE VIDEO YA MKURUGENZI WA UCHAGUZI NEC

Kwa mamlaka ya kisheria Tume iliyonayo, tayari imemuandikia Barua Mh. Tundu Lissu ya kumuita katika Kamati ya Maadili ya Kitaifa ili aje kutoa maelezo na ushahidi wa kile alichokisema katika mkutano wake huko Musoma.

Kwa mara nyengine tena Tume inawasihi Wagombea wa Vyama vyote kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kulinda amani ya nchi yetu, katika kipindi cha kampeni kilichobaki kwa kujali muda wa kampeni, ratiba za kampeni na kuepuka matusi, sababu unatumia muda mwingi kutangaza matusi badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kutangaza tuhuma badala ya kutangaza sera, unatumia muda mwingi kuwadanganya Watanzania na wafanyakazi badala ya kutangaza sera.

Watanzania sasa hivi wanataka Afya iliyoimarika, Watanzania sasa hivi wanataka barabara nzuri, Watanzania sasa hivi wanataka miradi ya umeme, Watanzania sasa hivi wanataka elimu bora, Watanzania hawataki bra bra. Watanzania sasa hivi wanataka viongozi ambao watalinda madini yao, sio viongozi watakaokuja kuchukua madini yao na kupeleka kwa wageni nje.
 
Angejua huu ni ushahidi tosha ICC
Huyu mkurugenzi mkuu wa NEC anaitisha vyombo vya habari na kusema eti watanzania wanataka mtu atakayelinda madini yao, atakayewajengea vituo vya afya, atakayewajengea mabarabara, atakayewaletea umeme. Kwani haya yanaihusu NEC?

Mkurugenzi wa NEC anaposema kuwa watanzania hawataki mtu atakayetorosha madini nje, kwani inaihusu nini NEC?

Kweli nimeamini hawa NEC siyo wa kuwachekea hata kidogo. Hata hii engua ya wagombea wa upinzani inafanywa kimkakati na inaonekana wazi wazi.

Magufuli amevuruga mifumo mingi huru ya maamuzi. Hii nchi inakoelekea siko hata kidogo.

View attachment 1583150
 
Hadi hapa wameshanonyesha wanampango wa kuiba.
Mungu wangu sio kwa kujisahau huku ...hii evidence mambo yakienda vibaya itamuweka pabaya mno...
Bila kutaraji kajionesha rangi zake halisi
 
Hayo anayoyaongea ndiyo kazi ya Tume? Mbona anaiweka Tume kwenye nafasi ya hatari sana? Yaani Tume inawalazimisha wagombea kitu cha kuongea? Watanzania wanajua wanachotaka kusikia na kila Chama kina ya kwake ya kujinadi kwa wananchi na Wananchi ndiyo wataamua.

Kwani madini yetu huwa yanauzwa wapi? Tume inahusika vipi na utekelezwaji wa Ilani za vyama? Mbona haijaongea kitu kuhusu aliyejisifu kuwanyima wananchi maendeleo kwa kutomchagua na kuahidi kuendelea kuwanyima kama hawatomchagua?

Mpaka hapo Tume imeshapoteza uhalali wake wa kusimamia uchaguzi huu na naiona kwamba kuwa ndiyo chanzo cha vurugu nchini.
Wameshapoteana.
JamiiForums-756288788.jpg
 
Inaonekana naye aliitwa dodoma akafokewa
Tunaposema Lissu ni hatari ndio muelewe. Mkurugenzi wa uchaguzi kachanganyikiwa na kuanza kunadi sera kama kichaa. Sasa kama kibaraka hofu yake ni dhahiri namna hii ‘bosi’ wake ana hali gani?

Hii sio aibu, ni fedheha!
 
ICC list

1. Bashiru
2. Polepole
3. Mahera
4. ...
Hii ni dalili ya wazi kuwa ndani ya kambi ya CCM na watawala wameshapanic sana, Magu keshalegea kulegea sana, Bashiru anawatisha tu wanaCCM, PolePole anavurumisha matusi, Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ameingia kupiga kampeni!!

Lissu kamatia hapo hapo, endelea kupiga spana tu.
 
Mahera Ni kilaza Sana yaani ajui hata Sasa yanauzwa kwa wageni. Apande jukwaani aokoe jahazi. Lisu bado anapiga Kanda ya ziwa ngome yao ndo wamepoteana hivi vipi akishuka huku waliozulumiwa korosho zao je si kibetrii kitakata Moto.
 
Mwenyekiti wa Tume kaonyesha rangi zake mapema.

Hii ni hatari sana kwa mustakabari wa nchi yetu.

Mwenyekiti kashindwa kuficha hisia zake na kujipambanua kuwa yuko upande wa chama chakavu.
 
Back
Top Bottom